Mgombea Udiwani wa CCM mbaroni kwa kugawa pombe usiku

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,506
41,016
Taarifa nilizopokea usiku huu (majira saa 5: 23) na kuthibitishwa na
Mbunge wa Chadema Jimbo la Ilemela Haines Kiwia, zinadai Mgombea
Udiwani kwa tiketi ya CCM Jacksoni Masamaki ametiwa mbaroni akiwa
katika zoezi la kugawa Pombo ili kuwashawishi wapiga kura. Imeelezwa
kwa sasa mgombea huyo amepelekwa kituo cha polisi Kirumba. Nitaendelea
kufuatilia kwa kina.

Source: Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi, Kanda ya Ziwa
 
Hiyo rushwa kuisha CCM, ni mpaka waliopo wafe wote, wazaliwe wapya!!
 
Bado ni tuhuma tuwe makini kuhukumu kama ilivyowahi kusikika kwamba Godbless Lema aliwahi kuwa jambazi. Propaganda za kisiasa ni nyingi kama kapelekwa polisi tuwe na subira kujua kwamba ni kweli au hapana
 
Taarifa nilizopokea usiku huu (majira saa 5: 23) na kuthibitishwa na
Mbunge wa Chadema Jimbo la Ilemela Haines Kiwia, zinadai Mgombea
Udiwani kwa tiketi ya CCM Jacksoni Masamaki ametiwa mbaroni akiwa
katika zoezi la kugawa Pombo ili kuwashawishi wapiga kura. Imeelezwa
kwa sasa mgombea huyo amepelekwa kituo cha polisi Kirumba. Nitaendelea
kufuatilia kwa kina.

Source: Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi, Kanda ya Ziwa

Hii ni habari njema kwa wapenda haki na mabadiliko lakin binafsi naona kama ni Danganya toto! Tatizo kubwa litakalotokea ni kuthibitisha kuwa Pombe hiyo ilitolewa ili kurubuni wapiga kura (kama Rushwa). labda tujiulize, kwani kuwa kwenye kampeni kunamzuia mgombea kuendelea kunywa pombe kama ni mnywaji, (na kawaida ya wanywaji si mnazijua)

Na kama ni kweli hawa watu waliomkamata walikuwa serious na kazi yao, ni kwa nini wasingewakamata na wale walionunuliwa Pombe? Sheria inasema aliyetoa na aliyepokea wote wametenda makosa
 
Taarifa nilizopokea usiku huu (majira saa 5: 23) na kuthibitishwa na
Mbunge wa Chadema Jimbo la Ilemela Haines Kiwia, zinadai Mgombea
Udiwani kwa tiketi ya CCM Jacksoni Masamaki ametiwa mbaroni akiwa
katika zoezi la kugawa Pombo ili kuwashawishi wapiga kura. Imeelezwa
kwa sasa mgombea huyo amepelekwa kituo cha polisi Kirumba. Nitaendelea
kufuatilia kwa kina.

Source: Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi, Kanda ya Ziwa

mwingine huyu hapa:

428179_407844965908383_100000486493679_1614236_843641567_n.jpg
 
Bado ni tuhuma tuwe makini kuhukumu kama ilivyowahi kusikika kwamba Godbless Lema aliwahi kuwa jambazi. Propaganda za kisiasa ni nyingi kama kapelekwa polisi tuwe na subira kujua kwamba ni kweli au hapana

Ndio hivyo mama mwenzenu amekamatwa na kupewa mkong'oto juu,hutaki unaacha.
 
Kaazi kweli kweli, hivi ukiwahonga wapiga kura kwa pombe halafu wakalewa unaanzaje kuwaomba kura?? Mtaelewana kweli??

Kweli magamba.com wamebanwa kote kote... Kuanzia Meru, Kiwira hadi Kirumba!
 
Mods. unganisha hii post na ile inayosema alipata kichapo baada ya kukutwa akigawa pombe maana ni huyu huyu inawezekana amekuja na nguvu ya pesa...
amedanganywa
 
jamani ee tuspotoshwe na watu wasiotaka maendeleo hizi tuhuma si za kweli hata kidogo,ndo maana hata alie positi hii habari hakuweza kuikamilisha kwa undani,hii inatokana na siasa majitaka ambazo ni za kumchafua mtu, mgombea udiwani wa ccm kata ya kirumba bw.jackson masamaki hayuko mbaroni na hajafanya kitendo hicho.Kwaiyo ndugu zanguni tuweni waungwana katika kipindi hiki cha kampeni tusiposti kitu kwa mapenzi ya mioyo yetu bali tupositi ukweli.
 
Back
Top Bottom