Elections 2010 Mgombea CHADEMA Apigwa Kinyama - Arusha

Wambugani

JF-Expert Member
Dec 8, 2007
1,757
276
Mgombea CHADEMA apigwa kinyama

na Violet Tillya, Arusha


MGOMBEA udiwani kwa tiketi ya Chama Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kata ya Mjini Kati, Salumu Seif Simba, amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha - Mount Meru, baada ya kushambuliwa kwa kipigo kikali na askari akiwa mahabusu katika Mahakama Kuu ya mkoa huo.

Inadaiwa mgombea huyo alifikishwa katika mahakama hiyo jana, baada ya kushitakiwa kwa kosa la kufanya fujo katika stendi ya mabasi kwa kugoma kulipa ushuru wa maegesho ya gari lake alilokuwa ameliegesha katika stendi hiyo.

Akizungumza kwa taabu na Tanzania Daima jana katika wodi aliyolazwa akiwa hospitalini hapo, alidai baaada ya kufikishwa mahakamani, baadhi ya askari waliokuwa zamu ambao amedai anawatambua kwa sura, walimzonga wakitaka awapatie sh 20,000 ili wasimweke mahabusu.

Alisema yeye alikataa kutoa kiasi hicho, kitendo kilichosababiwa abebwe mzobemzobe na askari wapatao wanne, waliomwingiza mahabusu, huku mmoja wa askari hao akiamuru mahabusu wengine waliokuwa mahakamani hapo wampige.

“Mahabusu hao walinishambulia vikali lakini niliweza kuwazidi nguvu, ndipo askari hao waliingia mahabusu na kuanza kunishambulia tena kwa kunipiga huku wakinikaba koo hali ambayo ilisababisha nipoteze fahamu,” alisema.


SOURCE: Tanzania Daima 23/09/2010
 
Hivi si sheria inasema mtuhumiwa atapigwa na askari kama atagoma kwenda polisi? LHRC tusaidieni hapa. Huku sio kuvunja haki za binadamu?
 
Kama kavunja sheria hiyo haki yake bwana.'Enyi watu tiini mamlaka yanayowaongoza'
 
Kama kavunja sheria hiyo haki yake bwana.'Enyi watu tiini mamlaka yanayowaongoza'

Hivi kumbe kwa serikali hii ya CCM ukikataa kutoa rushwa, umevunja sheria! kumbe askari kumpiga mtuhumiwa akiwa chini ya ulinzi wao ndani ya kituo cha polisi ipo kwenye sheria! Du kwa mtindo huu sijui kipi ni haramu kwa serikali hii!
 
Nadhani ni nafasi sasa kuchukua hatua za kisheria na si hatua za kisiasa. Kama ni ukweli basi nadhani hao Polisi wamejipalia mkaa!
 
Back
Top Bottom