Mgogoro wa Umeya Bukoba: Mangula ageuka mbogo; awataka wasiomtaka Amani kurudisha kadi

Tiger One

JF-Expert Member
Apr 11, 2012
568
310
Juzi Makamu Mwenyekiti CCM bara Ndg Mangula aligeuka mbogo katika kutatua mgogoro uliokuwa unalindima katika halmashauri ya Bukoba mjini kiasi cha kuhatarisha uhai wa chama hicho wilayani humo.

Mangula aliwataka wale wote wanaompinga Meya Ndg Aman warudishe kadi za chama na hakuna hata mmoja alothubutu kurudisha kadi. Ndo hapo Mangula akwambia Aman atakuwa meya wa hapo mpaka uchaguzi ujao na hakuna mjadala.

Je Bukoba kumetulia kwa maamuzi hayo ya kibabe ya Mangula? Je Kagasheki na kundi lake wameridhika?

Ngoja tujionee.

=================
updates

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Philip Mangula, amekivuruga chama hicho mjini Bukoba kutokana na uamuzi wake wa kuwalazimisha madiwani wao kuondoa tuhuma walizoziwasilisha kwa mkurugenzi wa manispaa hiyo dhidi ya Meya Anatory Amani.

Mgogoro huo umeshika kasi baada ya madiwani wanane wa CCM kuungana na wenzao wawili wa CUF na kusaini hati ya kumtaka Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Hamis Kaputa, aitishe kikao cha dharura cha kumjadili na kumng'oa meya huyo akidaiwa kutumia vibaya madaraka yake na kuiingiza halmashauri hiyo kwenye miradi ya kifisadi.

Kutokana na vuta ni kuvute hiyo, CCM ilimtuma Mangula kwenda kutanzua mgogoro huo, kwa kujaribu kukutana na pande zote mbili kabla ya kikao cha madiwani kuitishwa na kumng'oa Amani kwa kura.

Hata hiyo, Mangula ambaye aliwasiri mjini Bukoba juzi asubuhi na kufanya kikao na madiwani na wajumbe wa kamati za CCM Wilaya ya Bukoba na mkoa, anadaiwa kutumia ubabe kuwazima madiwani kuachana na hoja yao kwa madai kuwa walikiuka kanuni za chama, hivyo wanachokifanya ni usaliti.

Tanzania Daima ilidokezwa kuwa uamuzi huo uliwavuruga madiwani hao kiasi cha wengine kutishia kujiengua uanachama, kwa kile walichodai kuwa ni kiongozi huyo kuegemea upande mmoja kutaka kumlinda Meya Amani.

"Kwa mujibu wa kanuni zetu za halmashauri, ili kutimiza haja ya kumtaka mkurugenzi kuitisha kikao cha dharura kujadili ajenda fulani ni lazima hati hiyo ya tuhuma iwe imesainiwa na madiwani wasiopungua wanane," alisema mtoa habari wetu.

Aliongeza kuwa hoja ya Mangula kudai kwamba madiwani hao walikiuka kanuni kwa kukisaliti chama wakiungana na wapinzani si ya kweli, kwani tayari idadi yao ilikwisha kukidhi haja bila sahihi za wenzao wa CUF.

Taarifa kutoka mjini humo zilisema kuwa katika kujaribu kuzima mgogoro huo, Mangula alifanya kikao na Halmashauri Kuu (NEC) ya Wilaya ya Bukoba jana na kuwataka madiwani hao waondoe tuhuma zao dhidi ya meya huku akitishia kuwa asiyekubaliana na uamuzi huo arudishe kadi yao.

Badala yake kikao hicho kiliamua iundwe tume ya kuchunguza tuhuma hizo itakayokuwa chini ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali mstaafu Fabian Massawe, ambaye hata hivyo anatajwa ---- kinara wa washirika wa Amani, wanaohaha kuhakikisha ang'olewi.

"Tumekubaliana mgogoro huu umalizike haraka lakini baadhi ya wajumbe hawakuafiki hatua iliyofikiwa, maana kuna waliokuwa wamekuja na kadi zao wakitishia kuzirejesha kwa Mangula endapo zingefanyika njama za kumwandama Mbunge wetu, Balozi Khamis Kagasheki, anayesimamia hoja ya kung'olewa meya," alisema.

Kuzimwa kwa hoja ya madiwani hao kumeibua hofu ya kutofanyika kwa kikao cha madiwani wote kilichotarajiwa kuketi Janauri 28, mwaka huu, kutokana na ajenda ya kumjadili meya Amani kutokuwapo tena.

Alipoulizwa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Salapioni Rujugulo, kama kikao hicho kitafanyika, hakukubali wala kukataa, badala yake alihoji, kama ajenda haipo kikao ni cha nini?

"Sijasema kama hakitakuwapo, ila wewe unaniuliza majibu, umesema CCM wameondoa ajenda, sasa kawaulize wao, sisi tunafanya mambo tofauti na wao, hivyo siwezi kuwasemea," alijibu kiongozi huyo.

Wakati hali ikiwa hivyo ndani ya CCM, waasisi wa hoja ya ufisadi huo wa miradi, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wameweka msimamo mzito wa kuhakikisha meya huyo anang'olewa kwa manufaa ya wananchi.

Msimamo huo umetolewa na makao makuu ya chama hicho taifa chini ya Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa, ambaye ametoa maelekezo mazito kwa madiwani wao na viongozi wa chama Manispaa ya Bukoba.

Katika maagizo hayo, CHADEMA kimewataka madiwani wake kutorudi nyuma katika msimamo wao wa kupinga ufisadi unaofanywa na Meya Amani katika utekelezaji wa miradi hiyo.

Mangula alilazimika kuingilia kati mgogoro huo baada ya kikao cha madiwani wa CCM kushindwa kufikia muafaka kuhusu sakata hilo, kutokana na Meya Amani kukimbia akisingizia kuumwa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Meya huyo ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kagondo, alikuwa ajadiliwe na kikao hicho cha madiwani wa CCM ili kuamua kama ang'oke mwenywe au asubiri kura za kikao cha baraza la madiwani.

Amani alitumia sababu hiyo na kuondoka kikaoni muda mfupi baada ya katibu wa kikao, Ashura Hassan na msaidizi wake, Hilde Blandus, nao kuondoka kwa visingizio kama hivyo.

Pamoja na kudai kuugua, Amani aligoma kuwapatia wajumbe mihtasari ya kikao cha kamati ya siasa ya wilaya kilichopita akidai katibu wake aliondoka nazo.

Madiwani wanane wa CCM akiwamo Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki na wengine wawili wa CUF walitia saini hati ya kumtaka mkurugenzi wa halmashauri hiyo aitishe kikao cha dharura ili kumng'oa meya huyo.

Hoja ya kumng'oa meya iliibuliwa hivi karibuni na Balozi Kagasheki, ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, akiunga mkono msimamo wa CHADEMA, kupinga miradi ya uuzwaji wa viwanja zaidi ya 5,000 na ujenzi wa soko la kisasa.

Kagasheki aliapa mbele ya wapiga kura wake kuwa hayupo tayari kusutwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, kutokana na mikataba ya siri yenye harufu ya kifisadi aliyoisaini Amani kwa kificho bila kuwashirikisha madiwani wenzake.

Taarifa za ndani zinadai kuwa rushwa imetembezwa kwa baadhi ya madiwani wa vyama vyote ili kuwarubuni wasipige kura ya kumng'oa meya.

Baadhi ya vigogo wa serikali akiwamo mkuu wa wilaya na mkoa, mwenyekiti na katibu wa chama tawala Mkoa wa Kagera, wamekuwa wakifanya kila juhudi kumnusuru Amani asing'olewe, jambo lililowatia shaka Wana CCM wakidai viongozi hao wanakumbatia ufisadi na kukichafua chama chao.

Mgogoro huo ulikwishamfikia Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Kanali Massawe anadaiwa kujaribu kutaka kumshawishi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa Ghasia, aingilie kati.

"Massawe anahaha kumnusuru meya lakini sisi tunaangalia salama ya chama chetu mbele ya upinzani kwenye uchaguzi ujao. Huyu alijaribu kumpigia simu Ghasia lakini waziri huyo alimtaka ampelekee malalamiko kwa maandishi akisema hafanyi kazi kupitia simu," alisema.

Halmashauri hiyo ina madiwani 24, watatu wa CUF, wanne wa CHADEMA na 17 wa CCM. Ili kupitisha uamuzi huo wa kumuondoa meya, ni lazima robo tatu ya madiwani, yaani 16, wapige kura ya kuunga mkono hoja hiyo.

Miongoni mwa madiwani waliosaini hati ya kutaka kuitishwa kikao cha kumng'oa meya huyo ni Naibu wake, Alexander Ngalinda (Diwani wa Kata ya Buhende) na Yusuf Ngaiza (Kashai), ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Manispaa ya Bukoba.

Safi mangula...siasa bila ubabe haiendi popote...ona cdm wanabembelezana na waasi kwenye chama halafu waasi wenyewe watoto
 
Sasa hapa ndio propaganda za MaCCM zinapoonekana mfu. Wakifanya haya kina Mbowe inaonekana ubabe. Haya waseme na hili.
 
Juzi Makamu Mwenyekiti CCM bara Ndg Mangula aligeuka mbogo katika kutatua mgogoro uliokuwa unalindima katika halmashauri ya Bukoba mjini kiasi cha kuhatarisha uhai wa chama hicho wilayani humo.

Mangula aliwataka wale wote wanaompinga Meya Ndg Aman warudishe kadi za chama na hakuna hata mmoja alothubutu kurudisha kadi. Ndo hapo Mangula akwambia Aman atakuwa meya wa hapo mpaka uchaguzi ujao na hakuna mjadala.

Je Bukoba kumetulia kwa maamuzi hayo ya kibabe ya Mangula? Je Kagasheki na kundi lake wameridhika?

Ngoja tujionee.

Mangula ni CHADEMA huyu....anatuharibia CCM chama chenye demokrasia
 
Wakae chini waongee ili kumaliza mgogoro. Si vizuri kuacha watu wakiwa na kinyongo.
 
Kagasheki kashindwa, sasa kama ana ubavu aanze mapambano mengine na Mangula.
Alidhani ana uwezo wa kumtoa meya kwa pesa yake anayowaonga wale madiwani wajinga wa ccm na cuf na sasa kesi imeshaamuliwa.
Aliye na ubavu afanye kama Mangula alivyosema. Arudishe kadi au waende kinyume na maagizo ya chama wachomolewe kwenye chama.
Amani amelamba dume. Ndio sababu aliwakimbia wenzie kikaoni. Alijua kuna utetezi mbele yake. Ninachoweza kusema nampongeza kwa utulivu aliokuwa nao siku zote za mgogoro huu. Wakati wenzie walitumia vyombo vya habari kumpaka matope kwa unyenyekevu alikaa kimya akipigana vita hii. Bravo Amani. Piga kazi. Achana na Kagasheki. 2015 Tunaomba uweke jina kupambana nae sie tutakupa ubunge. teh teh teh teh teh teeeeeeee
:whistle::becky::madgrin::nimekataa
 
Wakae chini waongee ili kumaliza mgogoro. Si vizuri kuacha watu wakiwa na kinyongo.

Hamna kinyongo. Wale madiwani ni njaa tu inawasumbua. Wala hakuna wa kunyanyua mdomo tena. teh teh teh teeee:A S 11: :glasses-nerdy:
 
Kagasheki na meya now Mangula? then itakuwa Mwigulu na Nape. Kama hauna cheo, CCM in wenyewe
 
Kagasheki kashindwa, sasa kama ana ubavu aanze mapambano mengine na Mangula.
Alidhani ana uwezo wa kumtoa meya kwa pesa yake anayowaonga wale madiwani wajinga wa ccm na cuf na sasa kesi imeshaamuliwa.
Aliye na ubavu afanye kama Mangula alivyosema. Arudishe kadi au waende kinyume na maagizo ya chama wachomolewe kwenye chama.
Amani amelamba dume. Ndio sababu aliwakimbia wenzie kikaoni. Alijua kuna utetezi mbele yake. Ninachoweza kusema nampongeza kwa utulivu aliokuwa nao siku zote za mgogoro huu. Wakati wenzie walitumia vyombo vya habari kumpaka matope kwa unyenyekevu alikaa kimya akipigana vita hii. Bravo Amani. Piga kazi. Achana na Kagasheki. 2015 Tunaomba uweke jina kupambana nae sie tutakupa ubunge. teh teh teh teh teh teeeeeeee
:whistle::becky::madgrin::nimekataa

vipi alizungumzia pia issue ya uraia ya amani na favor ya kagasheki
 
Hii ndiyo CCM, kaenda kawasikiliza,kaamua.CDM unawafukuza then unawachafua.shauri enu
 
huyo KAGASHEKI Hataki MEYA ye nani? au ni hivyo vijisenti vya PEMBE ZA NDOVU ndiyo vinampa kiburi ss wameamua na yeye kumlipua c unaona pembe china mara namanga na ss makuyun zote zimeshikwa kiburi yake itaisha 2 wengoja wakati ukifika atatuambia hizo PEMBE zilizokamatwa ziko wapi? anajifanya kujisahaulisha we mwache wakati utafika na haya yote ajibu kwa mudibu wa sheria.
 
Huku uwezi kuwaona wakina Ritz chama wanaongea lolote. teh teh teh teh:shut-mouth:

Mkuu makamanda wanamwaga pumba za kila aina tupo tunapitia; Mangula anaondoa siasa za makundi tunataka CCM moja kama madiwani wetu wana malalamiko dhidi ya diwani mwenzao ambaye ndio meya tunataratibu zetu za kichama na hizo ndizo anazotaka zifuatwe. CCM ni chama na ndiyo sababu tunafanya mambo kichama; haiendeshwi kwa nguvu za baba mkwe.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Karibu Monduli na jisikia uko nyumbani, tafadhali!
 
Mkuu makamanda wanamwaga pumba za kila aina tupo tunapitia; Mangula anaondoa siasa za makundi tunataka CCM moja kama madiwani wetu wana malalamiko dhidi ya diwani mwenzao ambaye ndio meya tunataratibu zetu za kichama na hizo ndizo anazotaka zifuatwe. CCM ni chama na ndiyo sababu tunafanya mambo kichama; haiendeshwi kwa nguvu za baba mkwe.

Chama
Gongo la mboto DSM
chama so, nani yuko sahihi magula au wale madiwani?
Je wasipotii amri na wakaendelea na azma yao ya kumuondoa meya ndani ya council nini itakuwa hatima yao? maana hili nalo lawezekana!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom