hodogo
JF-Expert Member
- Mar 11, 2012
- 238
- 93
Nakubaliana nawe, ila sema tu mtizamo wangu ni lile la umuhimu wa kuweka formality ya consent kutoka vyama vya upinzani. Mi nionavyo inaweza hata ikawa na impact ya kuwatia moyo serikali kwa upande mmoja, lakini pia kuwapa signal waliopo upande wa pili kwamba katika hili wanashindana na taifa lote kwa ujumla wake, na siyo kipande kidogo cha taifa kama ambavyo wanaweza kuwa pengine wanawaza.
Kimsingi uko sawa. Lakini nakusihi ukumbuke serikali inavyokuwa na kigugumiizi kuukubali ushauri mzuri uunaotolewa na kambi ya upinzani. Ni vizuri kuonesha kimataifa mshikamano wetu kama Taifa, lakini hili nahisi likisemewa na kila chama, wengine hawana simile wataanza kushinikiza tena kwa maandamano kuchukua hatua. Mi naamni kuna diplomasia ya chini kwa chini itafanyika hasa litakapokuwa jambo hilo linapelekwa kwenye hatua za mwishomwisho kuelekea mstari wa mbele. Hapo utasikia tamko la kambi rasmi ya upinzani!