Ntemi Kazwile
JF-Expert Member
- May 14, 2010
- 2,182
- 307
Kuna watanzania wengi sana wanaonewa na kunyanyaswa na wawekezaji kutokana na wawekezaji kubebwa na watawala.
Katika hali ya kawaida, siyo kawaida mtu aende nchi ya ugenini halafu akawafanyie dhihaka wenyeji wake pasipo kuwa na sehemu ya kujikinga vinginevyo lazima atafukuzwa ama kufungwa bila kupoteza muda.
Masharti ya kupewa visa katika nchi yeyote ni pamoja na kuheshimu sheria za nchi unayotembelea, na ni nadra kero za mgeni mmoja kusubiri rais wa nchi ndiye azishughulikie, kuna idara ya uhamiaji, kuna idara za kazi na kuna mkuu wa wilaya ama mkoa ambaye anatarajiwa atatue matatizo haya madogo madogo, kama rais ndiye atatemewa kusuruhisha migogoro ya aina hii basi kuna tatizo kubwa sana la kiutendaji na tuna kazi ya kufika tunakokwenda.
Wananchi wa Mtibwa wamenyanyaswa na meneja yule kwa miaka sasa mbele ya watoto, watawala wao na mizimu ya watawala wao bila hata watawala kuonyesha dalili za kuishughulikia kero ile. Kwa sababu watawala sasa wanawahitaji wakulima masikini wale wameondolewa shetani yule ambaye nina imani atarudi (kama siyo yeye basi mdogo au kaka yake) tarehe 1 December 2010 mara baada ya watawala kumaliza shida yao ya sasa na atakaa kwa raha mstarehe akifidishia muda ambao hakuwepo (wakati wa kampeni).
Njia pekee ya kuhakikisha wageni wa namna hii hawarudi kamwe ni kuitoa serikali iliyoko madarakani ili wakae pembeni wajifunze kama ambavyo wenzao wa Kenya, Malawi, Zambia, Japan, n.k walivyofanya na wajipange upya wakiwa kama wapinzani.
Hatutaki watawala wanao sikiliza/tatua kero zetu wakati wa kampeni tu na miaka inayobaki wanatuacha kama watoto yatima huku wakigawana rasimali na uridhi wetu na wageni (wawekezaji) bila hata chembe ya aibu.