Wananchi wa kondoa sasa wamepata mgodi mpya wa Tumbelo ambao unatoa dhahabu kwa sasa.Jana nilitembelea maeneo hayo nikiwa nimeambatana na Mkurugenzi wa Halimashauri ya Kondoa pamoja na Muhasibu wa Halimashauri na Mwanasheria.Tukakuta shughuli za mgodini zikiendelea.Pamoja na kuendelea kwa shughuli hizo ila mgodi huu bado unachangamoto nyingi zikiwamo hali ya usalama mgodini,Afya na barabara mbovu.Serikali kama itawawezesha wachimbaji hawa wadogo basi itakuwa imelisaidia sana taifa hili.