Mfumo wa uhamisho utumishi portal ni kero na kikwazo kikubwa kwa watumishi wa umma

Ntemii

JF-Expert Member
May 25, 2022
290
525
Wakuu natumai mu wazima

Tangu kuanzishwa kwa mfumo wa kidigitali wa uhamisho kwa watumishi wa umma, lengo likiwa kupunguza urasimu na paperwork katika kufanikisha suala la uhamisho kwa watumishi.

Pamoja na lengo hilo zuri mfumo huu tangu uanze umekua ni kero na kizungumkuti cha hali ya juu kwa watumishi wanaoomba uhamisho mbalimbali kupitia mfumo huu.

Watumishi wanaoomba uhamisho wa kubadilishana ili mfumo uweze kukubali maombi yao lazima wote wawe wa kada moja na daraja moja kiutumishi tofauti na hapo mfumo hauwezi kubali maombi yao, kwamfano tabibu daraja la 2 hawezi badilishana kituo cha kazi na tabibu daraja la 1, hili suala ni kikwazo sana kwa watumishi wa idara moja na kada moja kupata nafasi hii ambapo kabla ya mfumo huu hili suala liliwezekana.

Licha ya changamoto nyingi za kimfumo ikiwepo server kuwa down kila mara, kutokupata incoming request, kusema ukweli utumishi muweke wazi kama mfumo umewashinda basi turudi kwenye analogia kuliko haya mateso mnayowapatia watumishi wa umma.
 
Serikali ya samia haipendezi kuona watumishi mnahama kaeni huko huko mtekeleze ilani,mama kizimkazi anaupiga mwingi sana
 
Nadhani tangu mfumo wa ESS uanze kutumika rasmi tar 01/09/2023,hakuna mtu ambaye amefanikiwa kuhama,kama wapo basi ni idadi ndogo sn
Mtumishi kuhama ni haki yake,na kiukweli mfumo ni mzuri lkn madam wanaoukontroll ni binadamu,ubaya wake ndo unapoanzia hapo,kibaya zaidi zaidi na watumishi walewale wolokuwa wananufaika na kitu kidogo ili mtu ahame
OMBI: wizara zinazohusika na utoaji vibali vya uhamisho,watoe tathmini mapaka sasa watumishi wangapi wamehama kupitia mfumo wa ESS walojinasibu kuwa itakuwa inachukua mda mfupi mtumishi kuhama
Nawasilisha
 
Back
Top Bottom