Mfumo wa Majimbo(Counties) vs Mikoa na Wilaya, upi wenye gharama kubwa katika kuendesha Serikali?

Chama Cha Democrasia na Maendeleo CHADEMA kinajaribu kuutambulisha mfumo wa Majimbo kuwa yamkini ndiyo majibu ya ustawi wa jamii yetu, binafsi nakubaliana nao tena naupenda sana kama ilivyo kuwa wakati wa manyang'au wa kizungu tulikuwa na mfumo huo. Shida ina kuja wahafidhina kuupinga kwa nguvu kuwa utatugawa ila kuna nchi zimefanikiwa na zina matatizo makubwa ya ubaguzi NIGERIA na KENYA zimefanikiwa na sasa zinasitawi vizuri sana. CHADEMA sasa wana sera ya hivi tunafikiri ni mzuri kwa mazingira yetu? maana ugatuzi huu wa madaraka unaleta maendeleo mapema kipimo KENYA imefanya vizuri sana, sasa tusemezane ni mzuri au utaleta bias miongoni mwa Majimbo ambayo hayana rasmali na sijui kama yapo yako kumi bara na visiwani na yatafanya kazi vizuri kwenye mfumo wa serikali moja. Ni mawazo tu wakuu kwa upeo wangu wa UPE Alamuski

Kweli umejitambulisha vizuri kuwa wewe ni UPE......hii nchi haitaweza piga hatua kuwa na watu wafinyu wa akiri kama wewe...... Topic yako yenyewe ni biased na inalengo hasi...... Si ni afadhari hao Chadema wamekuja na soln ya kile umeshindwa.......
 
Kaka sijui kwa nini ila Tanzania naiweka karibu na Kenya pia NIGERIA imefanya vizuri maana sasa ndo nchi yenye uchumi mkubwa Africa
 
Mfumo wa serekali sa majimbo ni bomba sana, japo hata wensetu wa kenya hawajauelewa fisuri but kuna baadhi ya maeneo umeansa kuonyesha mafanikio makubwa mfano Machakosi county
 
Chama Cha Democrasia na Maendeleo CHADEMA kinajaribu kuutambulisha mfumo wa Majimbo kuwa yamkini ndiyo majibu ya ustawi wa jamii yetu, binafsi nakubaliana nao tena naupenda sana kama ilivyo kuwa wakati wa manyang'au wa kizungu tulikuwa na mfumo huo. Shida ina kuja wahafidhina kuupinga kwa nguvu kuwa utatugawa ila kuna nchi zimefanikiwa na zina matatizo makubwa ya ubaguzi NIGERIA na KENYA zimefanikiwa na sasa zinasitawi vizuri sana. CHADEMA sasa wana sera ya hivi tunafikiri ni mzuri kwa mazingira yetu? maana ugatuzi huu wa madaraka unaleta maendeleo mapema kipimo KENYA imefanya vizuri sana, sasa tusemezane ni mzuri au utaleta bias miongoni mwa Majimbo ambayo hayana rasmali na sijui kama yapo yako kumi bara na visiwani na yatafanya kazi vizuri kwenye mfumo wa serikali moja. Ni mawazo tu wakuu kwa upeo wangu wa UPE Alamuski
kwani hata nchi zisizo na rasilimiali hazipendi kuitwa nchi?Mbona nchi za ulaya nyingi tuu hazina rasilimali..ila zimesambaza raia wao nje wakifanya miradi mingi sana kwa faida ya nchi yao..hujajiuliza Switzerland wanauza saa,cheese,chocolate, utalii, mabenki..etc ila wanasaidia nchi hadi km India,china brazil etc..majimbo nayo yatatakiwa kuwa na mikakati kibao ya kujikwamua,na wanaweza kopa ktk jimbo jirani,au ktk serikali kuu..km wanazidi suasua ..wanapewa masharti na mipango ya kimaendeleo watakayotakiwa ifanya ili wapewe misaada na mikopo....majimbo yanaweza ku specialize ktk kila kitu ....ili wawe na huduma au bidhaa tofauti kwa soko la nchini au nje.
 
Mfumo wa serekali sa majimbo ni bomba sana, japo hata wensetu wa kenya hawajauelewa fisuri but kuna baadhi ya maeneo umeansa kuonyesha mafanikio makubwa mfano Machakosi county

Yap kuna yule gavana wa Machakos Mr Mutunga kitu kama hicho amezindua plan ya mji mpya wa Machakos ukikamilika ule mji utakuwa zaidi ya Nairobi.Ni matunda ya mfumo mpya wa serikali ya majimbo.Sisi Watanzania tuendelee kulala na kuwaza kufanya ufisadi tu basi,Hatuna vision wala hatufikirii kitu chochote,tupo tupo tu kama machizi vile.We liangilie tu Bunge la Katiba na hoja namna zinavyojadiliwa mle ndipo utakapojua akili za Watanzania zilivyo mbovu,Yaani watu akili na fikra zao zinaangalia nyuma badala ya kuangalia mbele.
 
Serikali ya majimbo ni nini? Ni mfumo wa serikali ambapo sehemu flani ya madaraka na mamlaka kutoka serikali kuu yanahamishiwa katika serikali za majimbo. Katika mfumo wa serikali ya majimbo Gavana anachukua nafasi ya mkuu wa mkoa,na anachaguliwa na wananchi kwa njia ya kura.

Faida kubwa ya utawala wa majimbo ni kwamba moja, unasaidia kuondoa urasimu katika upatikanaji wa huduma za kijamii;

Pili unasaidia kuchochea kasi ya kimaendeleo katika ngazi ya majimbo kupitia ushindani wa kimaendeleo unaokuwepo baina yao;

Tatu unasaidia kukuza demokrasia ya kweli kwavile mfumo wa serikali unatoa fursa kwa vyama vya upinzani kutawala serikali za majimbo na hatimaye kuonyesha ubora wa sera zao;

Nne unasaidia kuondoa urasimu katika eneo la uwekezaji kwavile shughuli za uandikishaji wa makampuni na viwanda vya wawekezaji wa kigeni vitafanyika ndani ya majimbo husika badala ya kufanyika Dar es salaam pekee na hivyo kuharakisha kasi ya maendeleo ya majimbo yao na taifa kwa ujumla;na tano unatoa fursa kwa majimbo husika kuzitumia rasilimali zinazopatikana humo kwa shughuli za kimaendeleo ya majimbo hayo.

Hizo ni faida chache ninazozijua za serikali ya majimbo,unaweza kuongezea.
 
Serikali ya majimbo ni nini? Ni mfumo wa serikali ambapo sehemu flani ya madaraka na mamlaka kutoka serikali kuu yanahamishiwa katika serikali za majimbo. Katika mfumo wa serikali ya majimbo Gavana anachukua nafasi ya mkuu wa mkoa,na anachaguliwa na wananchi kwa njia ya kura.
Faida kubwa ya utawala wa majimbo ni kwamba moja, unasaidia kuondoa urasimu katika upatikanaji wa huduma za kijamii;pili unasaidia kuchochea kasi ya kimaendeleo katika ngazi ya majimbo kupitia ushindani wa kimaendeleo unaokuwepo baina yao;tatu unasaidia kukuza demokrasia ya kweli kwavile mfumo wa serikali unatoa fursa kwa vyama vya upinzani kutawala serikali za majimbo na hatimaye kuonyesha ubora wa sera zao,nne unasaidia kuondoa urasimu katika eneo la uwekezaji kwavile shughuli za uandikishaji wa makampuni na viwanda vya wawekezaji wa kigeni vitafanyika ndani ya majimbo husika badala ya kufanyika Dar es salaam pekee na hivyo kuharakisha kasi ya maendeleo ya majimbo yao na taifa kwa ujumla;na tano unatoa fursa kwa majimbo husika kuzitumia rasilimali zinazopatikana humo kwa shughuli za kimaendeleo ya majimbo hayo.
Hizo ni faida chache ninazozijua za serikali ya majimbo,unaweza kuongezea.

Unapoamua kutoa elimu jifunze kuonyesha faida na hasara au madhala ikiwezekana kwa mifano. Halafu unatoa mapendekezo au unawaachia unaowafundisha wajadiri na kukuliza kama wana cha kukuliza.
 
Kwa nchi zetu hasa afrika ambazo bado hazijakomaa kisiasa na maendeleo ya kulegalega naona mfumo wa majimbo sio mzuri,kasababu, kama ulivyosema gavana anachaguliwa na wananchi ni sawa, watu wanamchagua mtu wanaemtaka,pia jimbo linakua na baraza lao la maamuzi ya kimaendeleo.

MADHARA TAKE.
(1)-Jimbo moja kuwa na maendeleo kuliko lingine, hii inasababishwa na jimbo moja kuwa na vyanzo vyanzo vya mapato kuliko lingine mfano, Mfano leo hii maeneneo yenye migodi ingekua na majimbo wangeomba hata kutaka kujitenga kwasababu wanajua mali wanazo.

(2) gavana anaweza kujilimbikizia mali yeye na jamaa /familia yake na Rais asiweze kumuadabisha, mfano, mozee itumbi kongo, kabila anashidwa amfanyeje anabaki kulalamika tu.

(3)usalama wa nchi na eneo husika kuwa mdogo, kwasababu jimbo litakua na malighafi mfano almasi, gesi, nk. Gava anaweza kupata vishawishi kutoka kwa watu wasioitakia nchi maendeleo, au kutoelewana kwa baadhi ya makundi kwasabu ya kuchota mari na ndio mwanzo wa machafuko.
KENYA NI NCHI MNAYOIPA SIFA KILA SIKU KUWA INA UCHUMI MKUBWA AMBAYO GDP YAKE NI NZURI UKIGAWANYA KWA PER CAPITAL INCOME PIA NI NZURI LAKINI HUWEZI KAMINI I MIKOA MITATU TU KATI YA MINANE NDIO INAYOPATA MILO YA KULIDHISA KWA SIKU.KUNA NJAA HUWEZI KUAMINI. TOFAUTI NA HAPA KWETU MIKOA ISIOZIDI MI5 INALISHA NCHI NZIMA.

WAKUU WA MIKOA.
UBAYA WAKE.
(1)-RAIS anamchagua mtu anaempenda, hii inasababisha asikilize maamuzi ya aliemteua tu hatakama ni mabaya.

(2) -wananchi hawana uhuru wa kuchagua mtu wanaemtaka, hii inasababisha mkuu huyo mambo mengi ayaendeshe hata kwa ubabe alijivuni kwa alie mchagua.

FAIDA ZAKE.
(1) -RAIS anauwezo wa kumtengua wakati wowote kama ataenda kinyume .

(2)-ulinzi na usalama wa raia utalidhisha kwa asilimia kubwa maana kila mkuu anasimamia usalama wa eneo lake.

(3)- ushawishi wa kujitenga na nchi inakua ni vigumu ktk nchi, maana itakua lahisi kungundulika na kuweza kutenguliwa haraka.

(4)-shughuli za maendeleo zinaenda kwa mpango maalumu kutoka ngazi ya juu hadi ngzi ya chini hasa kielimu, ulinzi nk.kwa hiyo sio lahisi kujihusha na ufisadi mkubwa bila ya kugundulika.

(5) ni lahisi kuwaunganisha wananchi na kuwapa elimu ya jambo fulan linapotokea kama vile magonjwa, kutoelewana kwa makundi ya watu au kabila fulani nk.
(6)- sheria kalibu zote zitakua zinafanana tofauti na mfumo wa majimbo unaweza ukaenda jimbo moja likawa na shelia tofauti na lingine.(kama utakua na cha kuongeza sio mbaya).
Pia fanya uchunguzi mwenyeweu uone kalibu nchizote duniani zenje mfumo wa majimbo ndio zenye vita kwa sasa. Kwa kukuongezea tu, ikitokea Tanzania leo imeingia kwenye mfumo huu wa majimbo Matatizo ya vulugu au kutaka kujitenga yataanza hasa kwa watu wa maeneo ya kwenye gess nyingi (kusini) na kwenye Tanzanite (kaskazini)

KWA MM NAONA MFUMO WA MIKOA BADO NI BORA KULIKO WA MAJIMBO. KTK NCHI ZETU ZINAZOENDELEA.
 
Safi sana Teknolojia. Lakini nasikitika kwamba katika nchi yetu tuna kawaida ya kushtuka baadaye sana. Watakwambia majimbo yataleta ukabila au vita. Hilo ndiyo jibu la haraka kwa wanaofahamu kila kitu katika nchi hii. Wengine wanasema kuna mikoa itaachwa nyuma sana kwa sababu ya raslimali chache; kama vile kwa sasa mikoa yote iko sawa kimaendeleo! Hata mimi naamini kwamba Tanzania ni nchi kubwa sana; na pengine kuitawala kwa kutumia mfumo wa sasa (Kutoka ikulu ya Magogoni) ndiko kunakochelewesha maendeleo katika maeneo mengi.
 
This is not a lecture hall/room.I have simply set a tone for the discussion on the structures, designs and systems of the government. It is just an open-ended topic.
Unapoamua kutoa elimu jifunze kuonyesha faida na hasara au madhala ikiwezekana kwa mifano. Halafu unatoa mapendekezo au unawaachia unaowafundisha wajadiri na kukuliza kama wana cha kukuliza.
 
Back
Top Bottom