Mfanyakazi wa Kampuni ya Mwananchi Communications apigwa risasi

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
cccc.jpg

MFANYAKAZI wa Kampuni ya Mwananchi Communications, Patrick Pella amevamiwa na majambazi wenye silaha na kupigwa risasi, kujeruhiwa na kisha kuporwa fedha zake jana mchana maeneo ya Tabata-Relini jijini Dar.

Pella anadaiwa kuporwa kiasi cha Sh. Mil 2 alizokuwa nazo akiwa ametoka kuzichukua kwenye mashine ya kutolea fedha (ATM) Tawi la NMB liliyopo jirani na Azam TV, Barabara ya Mandela.

http://goo.gl/XYUO3N

================================

Watu wasiojulikana wamempiga risasi moja ya mkono na kumpora fedha kiasi cha Sh2milioni mfanyakazi wa Kampuni ya Mwananchi Communication Limited, Patrick Pera mara baada ya kutoka kuzichukua katika benki ya NMB tawi la Mandela jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo limetokea leo mchana katika kituo cha mafuta cha Oil Com kilichopo katika eneo la Tabata Relini wakati Pera alipokuwa amepakia kwenye pikipiki huku akiwa na idadi hiyo ya fedha kutoka benki

Akizungumza na tovuti hii akiwa katika hospital ya Amana jijini Dar es Salaam kabla ya kuhamishiwa katika hospital ya Taifa ya Muhimbili, Pera ambaye ni Mhariri msaidizi wa habari za kwenye mtandao amesema alifika katika benki hiyo majira ya saa nane ili kuchukua kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya matumizi muhimu.

Amesema baada ya kuandikisha fomu na kupatiwa fedha hizo alitoka nje ya benki hiyo na moja kwa moja alielekea kwa waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda ili kukodi kwa lengo la kuletwa ofisini kabla ya kwenda kukabidhi fedha hizo kwa kaka yake.

Amesema waendesha bodaboda walianza kutupiana mpira huku kila mmoja akitaka mwenzake ampeleke ndipo kijana mmoja alipoamua kumpakia.

Amesema kabla ya kufika ofisi za MCL wakiwa kwenye kituo cha mafuta cha OIL Com walitokea vijana wengine wawili waliokuwa na pikipiki na kumuamrisha atoe fedha alizokuwa nazo.

Amesema aliwauliza kuwa wao ni wakina nani, ndipo walipomuonyesha bastola na akaamua kuwapatia fedha hizo, lakini kama hiyo haitoshi wakaamua kumpiga risasi moja mkononi.

Tovuti ya mwananchi iliyokuwepo katika hospitali ya amana iliambiwa kuwa risasi iliyopigwa mkononi mwa Pera imesaga mfupa hivyo anahamishiwa kwenye Hospital ya Muhimbili kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji kwa kuwa hospital hiyo haina uwezo wa kufanya hivyo.

Aidha Jeshi la Polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba uchunguzi umeanza mara moja kwa kumshikilia na kumuhoji kijana wa Bodaboda aliyekuwa anamuendesha Pera alipokuwa akitokea benki.
 
RUCCI

Hhii habari ipo kwenye tovuti ya MCL, imechapishwa kama ifuatavyo...

Last edited by a moderator:
Pole kwa shambulio na uvmizi ila Mashine za ATM za NMB kiwango cha mwisho ni 1 Milion hapo kuna pepesa pepesa sentensi!!!!!!
 
...

Amesema aliwauliza kuwa wao ni wakina nani, ndipo walipomuonyesha bastola na akaamua kuwapatia fedha hizo, lakini kama hiyo haitoshi wakaamua
kumpiga risasi moja mkononi.

Tovuti ya mwananchi iliyokuwepo katika hospitali ya amana iliambiwa kuwa risasi
iliyopigwa mkononi mwa Pera imesaga mfupa hivyo anahamishiwa kwenye Hospital ya Muhimbili kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji kwa kuwa hospital hiyo haina uwezo wa kufanya hivyo.

pole yake..apone arudi kwenye majukumu,maana mkono wake ndio kula yake
 
Jamani Jamani,ccm Ikiendelea Kuongoza Tutakwisha Wote Kabisa Si Suala La Mchezo,kwanza Police Wenyewe Ndo Majambazi Namba Moja,sijui Hatima Yetu Watanzania Kwenye Serikali Dhaifu Hii Ya ccm.
 
Mshaara wa Mhariri ni kihasi gani wakuu? Tar 19 mfanyakazi kuwa na mil 2 kwenye account? Wanalipwa sh ngapi kwa mwezi?
 
Yaani alikuwa ametoa hela mil 2 akampe kaka yake ,LAKINI yeye akaamua kwenda nazo ofisini ¿? Hapo naomba sijaelewa !
 
View attachment 228068

MFANYAKAZI wa Kampuni ya Mwananchi Communications, Patrick Pella amevamiwa na majambazi wenye silaha na kupigwa risasi, kujeruhiwa na kisha kuporwa fedha zake jana mchana maeneo ya Tabata-Relini jijini Dar.

Pella anadaiwa kuporwa kiasi cha Sh. Mil 2 alizokuwa nazo akiwa ametoka kuzichukua kwenye mashine ya kutolea fedha (ATM) Tawi la NMB liliyopo jirani na Azam TV, Barabara ya Mandela.

#BreakingNews:-Mfanyakazi wa Kampuni ya Mwananchi Communications apigwa risasi | MISHE MISHE ZA MWAFRIKA

Inside job.
 
Sasa hivi tumeshikika kwa kuponea hatuna ukienda polisi unaenda kuongeza hasara,kwa mganga ndo hasara zaidi
 
Hujaisoma vizuri taarifa hii!! Kwenye taarifa yao MCL, wapi wamesema kuwa hizo pesa zimetoka kwenye ATM?, Mbona wamesema alijaza form ndani na kuchukua hiyo pesa!
Ni kweli nilisoma mistari miwili ya para 2 za mwanzo sikwenda mbali, nakiri nimekurupuka kumbe alijaza fomu na kupewa kiasi hicho nafuta kauli.
 
Yaan kama 2m mtu anapigwa risasi kwa hali hii miaka michache mbele mtu hata ukiwa unatembea na laki 3 yakupasa uwe makini hauchelewi kuonyeshewa mkwaju uzitoe zote
 
Back
Top Bottom