Mfanyabiashara mwenye Uhitaji wa Frem na Una Mtaji

CONTROLA

JF-Expert Member
Sep 15, 2019
6,939
22,989
Yawezekana una mtaji na hujui wapi utapata frem au umeshatafuta sana frem lakini hupati Frem. Lakini sio tu Frem ila unahitaji Frem iliyo katike best location.

Huwa sinaga uchoyo katika kuinua mtu anae hitaji kuinuka,sasa nataka kumpa mtu Frem BURE kwa muda wa miezi 6.. Nasema only for 6 months fanya huku ukiwaza baada ya miezi 6 uende wapi au uhamie wapi.

Frem ninayokupa imeshafanyiwa Final touches za ubora wa Hadhi ya Mteja Wa hali ya juuu,ni Frem ya Gharama lakini kwasasa nmeifunga kwasababu zilizoingiliana.

Ni frem iliyolipiwa kodi ya miaka mi 3 kwa mwezi kodi ni 900,000 (laki 9) Nina sababu kwanini nataka msaidia mtu afanye biashara katika hii frem,maana kwasasa nimeifunga TU ipo na sina plans nayo mpka February next year.

Kuliko ni ifunge ikae tu,najua yupo mtu mahali anatamani kujaribu au kuanza biashara lakini Hajapata frem au Hana Pesa ya Frem,sasa kama wewe n mmoja wapo nakupa frem ili ujipime kama biashara unaiweza au huiwezi kwa muda wa miezi 6 TU. Baada ya hapo utakua ushakua mwenyeji naamini kuhama na wateja wako its easy.

Frem iko full branded kwa biashara
1.electronics
2.Emoney Service
3.Accessories
4.Many More

Kama unahisi biashara yako inacheza humo au ina relate na hivyo ruksa karibu,Biashara yoyote inayoweza fanyika kwenye duka kubwa lenye AC na Urembo wa maduka ya SINZA karibu.

Hii si kwa wale wenye biashara za NAFAKA,MADUKA YA MANGI,na wengineo...

Kama unahisi hii inakufaa au ni Fursa kwako Karibu PM.

Kwa mfanyabiashara tu.
 
Miezi 6 mtu aondoke mbona mtihani sana mkuu. Maana huenda pamoja na frem kuwa bure bado kuna masuala ya kodi , TRA n.k nayo mtu anakuwa ameingia. Baada ya miezi sita pengine asiwe amepata faida bado kwenye biashara yake. Japo ni msaada bado ni mtihani mkubwa kwa mtu baada ya hapo hajui aende wapi
 
Back
Top Bottom