Mfanyabiashara Ayubu Kiboko na mkewe washinda rufaa yao ya kusafirisha dawa za kulevya

We Ni kilaza,Sasa kwenda kumkamata mtuhumiwa bila ya kuwa na search warrant, na hati ya kuhozi Mali, hivyo vyote mwisho wa siku kuna sehemu ya kujaza balozi wa eneo husika ambae aliitwa kushuhudia upekuzi, au shaidi mwingine huru,
Kwaiyo hizo dosari mbili tu inatosha kuonyesha kwamba polisi huo unga waliendanao wao wenyewe!
Hata kama huyo kiboko kweli alikuwa anafanya hiyo biashara labda
Siyo kilaza kama unavyonidhania rafiki.

Katika comment yangu nimeambatisha na mifano hai ya raia waliokamatwa kitaa bila ya hizo nyaraka na mpaka tunavyoongea wapo mkusota.

Labda nikuulize wewe mwenye upeo, raia yeyote hawezi kufanya ukamataji kwa kukuta kosa likitendwa na mhalifu?

Tukimaliza kulijadili hili, turudi kwenye hii hukumu ya marejeleo.

Kwanza walifungwa kwa hakimu wa kwanza baada ya kujiridhisha kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo bila kuacha shaka yoyote.

Sasa kuja kumtoa kisa serch warrant, hapana hapo lazima kuna loop holes za kisheria bhana.
 
22 February 2022

KILO 250.7 ZA DAWA ZA KULEVYA ZACHOMWA MOTO MTWARA



Mamlaka ya kudhibiti na kupamabana na dawa za kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, Idara ya Usalama wa Taifa, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Mahakama, Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na Baraza la Taifa la Mazingira limeteketeza kwa moto jumla ya kilo 250.7 za dawa za kulevya kwa kutumia tanuri la moto katika kiwanda cha Dangote Mkoani Mtwara.


Dawa hizo zilizoteketezwa zinajumuisha kilo 51.7 za heroin na kilo 199 zenye mchanganyiko wa heroin na cocein Uteketezaji huo ni kutokana na amri ya Mahakama iliyotolewa katika kesi namba 2 ya mwaka 2018 kwenye kikao cha Mahakama Kuu kilichoketi mwishoni mwa mwezi oktoba na kumalizika Novemba 5, 2021 mbele ya Jaji Latifa Mansour.


Kesi hiyo iliwahusisha washtakiwa wawili ambao ni Sano Sidiki na Tukure Ally ambao wamehukumiwa kutumikia kila mmoja kifungo cha miaka 20 gerezani.

Zoezi hilo limefanyika kwa mujibu wa kanuni namba 14ya Kuthibiti na Kupambana na Dawa za kulevya ya mwaka 2016 za Sheria ya Kuthibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya namba 5 ya mwaka 2015.

Zoezi hilo limeongozwa na Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Bwn. Gerald Musabila Kusaya ambapo pia amewasihi wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Vyombo vinavyojihusisha na mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwa kutoa taarifa juu ya watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya nchini.

Source : Kusini Yetu Online TV
 

Februari 22, 2022​

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) yateketeza kilo 250.7 za dawa za kulevya​

NA GODFREY NNKO

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali leo Februari 22, 2022 imeteketeza jumla ya Kilo 250.7 za dawa za kulevya zikijumuisha kilo 51.7 za heroine na kilo 199 zenye mchanganyiko wa heroine na cocaine katika kiwanda cha saruji cha Dangote mkoani Mtwara.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Februari 22,2022 na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Bw.Daniel Kasokola.

"Uteketezaji huo ni kwa ajili ya kutekeleza amri ya Mahakama iliyotolewa katika kesi Namba 2 ya Mwaka 2018 kwenye kikao cha Mahakama Kuu kilichoketi mwishoni mwa mwezi Oktoba na kumalizika tarehe 5 Novemba 2021 mkoani Lindi mbele ya Jaji Latifa Mansour.


"Kesi hiyo iliwahusisha washtakiwa Sano Sidiki na Tukure Ally ambao wamehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 20 gerezani kila mmoja.
"Amri nyingine ya uteketezaji ilitolewa na Mheshimiwa Jaji Isaya Arufan tarehe 29 Novemba, 2021 kwenye kesi Namba 25 ya mwaka 2019 iliyowahusisha washtakiwa Mohamed Nyamvi na Ahmad Said Mohamed. Katika kesi hiyo washtakiwa hao walihukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 20 kila mmoja,"amefafanua.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, zoezi hilo limefanyika kwa mujibu wa Kanuni Namba 14 ya Kanuni za Kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya za mwaka 2016 za Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Namba 5 ya mwaka 2015.

Kanuni hiyo inaelekeza kuteketeza dawa za kulevya baada ya shauri kumalizika Mahakamani na kwa dawa za kulevya zenye tabia ya kubadilika au kuharibika endapo zitakaa kwa muda mrefu uteketezaji wake unaweza kufanyika kabla au wakati shauri husika linaendelea kusikilizwa Mahakamani.

"Ndugu wanahabari uteketezaji huu ni wa pili kufanyika hapa kiwandani. Itakumbukwa kuwa, tarehe 15 mwezi Juni mwaka 2021, ulifanyika uteketezaji mwingine uliojumuisha jumla ya kilo 355 za dawa za kulevya aina ya Methamphetamine.

Zoezi la uteketezaji limekuwa likifanyika katika viwanda vya Saruji kwa lengo la kuepuka dawa hizo kuharibu mazingira na kuathiri afya za watu.

"Uteketezaji huu umefanyika kwa uwazi mbele ya wadau wote muhimu wanaotambulika kisheria na kushuhudiwa na waandishi wa habari ili kuondoa dhana iliyojengeka kwa baadhi ya wananchi kwamba, baada ya dawa za kulevya kukamatwa kurejeshwa mtaani na kuuzwa tena.
"Mamlaka inatoa shukrani kwa wadau wote walioshiriki katika kufanikisha zoezi hili muhimu la uteketezaji. Kipekee inamshukuru mwekezaji wa kiwanda cha saruji cha Dangote kwa kuendelea kutupatia ushirikiano kwa kuruhusu zoezi hili kufanyika kiwandani hapa,"imefafanua taarifa hiyo.

Wakati huo huo, DCEA imewasihi wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa vyombo vinavyojihusisha na mapambano dhidi ya tatizo la dawa za kulevya kwa kutoa taarifa juu ya watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Mamlaka hiyo imesema kuwa, kupitia ushirikiano huo wanaamini kuwa, "tutaishinda vita hii na hatimaye kuifikia Tanzania yenye kizazi kisichotumia wala kushiriki kwenye biashara ya dawa za kulevya,"imeeleza.

Source : Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) yateketeza kilo 250.7 za dawa za kulevya
 
TOKA MAKTABA :

13 November 2020

MAPAMBANO DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA YATEKETEZWA DAR ...DPP ASIMAMIA HILO...



OFISI ya Mkurugenzi wa mashtaka (DPP) kwa kushirikiana na mamlaka mbalimbali za kisheria imeteketeza rundo la madawa ya kulevya yaliyotokana na kesi 15 zilizofikishwa mahakamani jijini Dar es Salaam.

Madawa hayo yaliyoteketezwa siku ya Alhamisi ya Novemba 12, 2020 Jijini Dar es Salaam ni pamoja na kilo 119.074 za heroin, kilo 3.93 za kokein na kilo 120 za bangi.

Akiongea na wanahabari wakati wa zoezi la kuteketeza madawa hayo, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Biswalo Mganga amesema kesi iliyokuwa kubwa zaidi miongoni mwa kesi hizo 15 ni kesi iliyowahusisha rais 12 wa Pakistani ambao wamehukumiwa miaka 30 jela na jahazi waliokuwa wakilitumia kuingiza madawa hayo limetaifishwa.

Source : MASHTAKA TV
 
28 March 2022

MAHAKAMA KUU YA RUFAA TANZANIA : Mfanyabiashara Ayubu Kiboko na mkewe Pilly Kiboko washinda rufaa yao dhidi ya hukumu ya awali

Kesi yenyewe :
Awali mwezi December mwaka 2020 Mahakama Kuu Divisheni Maalum : Mahakama ya Uhujumu Uchumi na makosa ya rushwa iliwaona wana hatia.

WhatsApp-Image-2020-12-18-at-18.25.13-660x400.jpeg

Mfanyabiashara Ayubu Kiboko na mkewe Pilly Mohammed wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kukutwa na Dawa za Kulevya aina ya Heroin Hydrochloride.

Wawili hao wamehukumiwa leo katika Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi maarufu kama Mahakama ya Mafisadi mbele ya Jaji Mfawidhi, Lilian Mashaka.

Awali katika hukumu hiyo ikiwa ni kesi ya Uhujumu Uchumi namba 13 ya mwaka 2018 Jaji Mashaka alisema kwamba ushahidi wa upande wa mashitaka umethibitisha kesi kwa mshitakiwa wa kwanza na wapili, hivyo mahakama inawatia hatiani kwa makosa wanayoshitakiwa nayo.

Jaji Mashaka alisema kuwa kwa maoni yake utetezi wa mshitakiwa wa Kiboko na mkewe uliunga mkono ushahidi wa Upande wa Mashitaka kutokana na kujichanganya kwa maelezo yao ya ushahidi.

“Mshitakiwa wa Kwanza na Wapili mlikuwa mnajua kwamba kulikuwa na Dawa za kulevya katika Stand ya Viatu,”

“Mshitakiwa wa Kwanza na Wapili mna makosa kama mlivyoshtakiwa na mna hatia kwa kukutwa na Dawa za Kulevya aina ya Heroin”

Katika kesi ya uhujumu uchumi namba 29/2018, Kiboko na mkewe wanadaiwa, Mei 23, 2018 eneo la Tegeta Nyuki Masaiti wilaya ya Kinondoni, walisafirisha dawa za kuĺevya aina ya heroin zenye uzito wa gramu.

...............................................

HUKUMU YA MAHAKAMA YA RUFANI TANZANIA 24 MARCH 2022:

APPEALS COURT​

RELEASES COUPLE OVER NARCOTIC DRUGS TRAFFICKING​

24-03-2022 0

Published By:LYDIA CHURI


By Faustine Kapama-Judiciary
THE Court of Appeal has ordered the release from prison businessman Ayubu Kiboko and his wife Pilly Kiboko who were sentenced to 20 years’ imprisonment for trafficking in 251.25 grammes of heroin hydrochloride, which are narcotic drugs.

Justices Dr. Gerald Ndika, Ignas Kitusi and Sam Rumanyika ruled in favour of the couple, the appellants, after allowing the appeal the two had lodged to oppose findings of the High Court’s Corruption and Economic Crime Division in Dar es Salaam.
“We allow the appeal and proceed to quash the convictions and set aside the sentences against the appellants.

Accordingly, we order that the appellants, Ayubu Mfaume Kiboko and Pilly Mohamed Kiboko, be released from prison unless they are held there for any other lawful cause,” they declared.

The justices granted one ground of appeal among seven the appellants had advanced, which challenged the decision of the High Court with effects that the search into their home which was conducted by a team of police officers from the Drug Control and Enforcement Authority (DCEA) was illegal.

“We are constrained to expunge the illegally obtained evidence, which, apart from the alleged prohibited substance and the certificate of seizure, included the other seized substances and the three motor vehicles,” they ruled.
The justices pointed out that the remaining evidence on record after discounting such evidence, including the seized alleged drugs, was too thin on its own to support the charge the appellants faced.

They said that the police powers of search and seizure are governed by section 38 of the Criminal Procedure Act (CPA) with Subsection (1) empowering police officer in charge of a police station ("OCS") to search or to issue a written authority to any police officer under him to carry out the search.

According to the justices, Subsection (2) comes in force when a search is executed upon a written authority and police officer who executes the search is required to report, as soon as practicable, the issue of the authority the grounds on which it was issued and the result of the search to a magistrate.

“This binding obligation is followed up by another imperious requirement under subsection (3) imposed on the officer in charge of the search, upon seizure of a thing, to issue a receipt acknowledging the (such) seizure, bearing the signature of the owner or occupier of the premises or relative,” they said.

The justices pointed out further that apart from section 38 of the CPA, sections 40 and 42 (1) (a) and (b) of the Act also regulate the conduct of searches, as section 40 provides that a search warrant may be issued and executed on any day and may be executed between the hours of sunrise and sunset.

However, the court may, upon application by a police officer or other person to whom it is addressed, permit him to execute it at any hour. Section 42 (1) (a) and (b) creates an exception to the overall requirement under section 38 (1) by providing for searches and seizures in cases of emergency.

In the case at hand, having revisited the evidence tendered during the trial, the justices noted that the police officer who lead the search team was not an OCS and had no requisite written authority (search order) from an OCS to carry out the search.

Furthermore, they said, the evidence does not suggest that the impugned search was executed as an emergency undertaking in terms of section 42 (1) of the CPA dispensing the requirement for a search order or warrant.

“We think that this is a classic case where police officers, believing that they were unshackled by the law and that they had a free hand, went ahead, entered into and searched suspects' home brazenly violating the law,” the justices said.
In the trial, Kiboko and his wife Pilly were charged with trafficking in narcotic drugs.

It was alleged that on May 23, 2018 at Tegeta-Nyuki in Kinondoni District in Dar es Salaam, the couple trafficked in heroin hydrochloride, which are narcotic drugs, weighing 251.25 grammes.

In the final analysis, we allow the appeal and proceed to quash the convictions and set aside the sentences against the appellants. Accordingly, we order that the appellants, Ayubu Mfaume Kiboko and Pilly Mohamed Kiboko, be released from prison unless they are held there for any other lawful cause.

Source : APPEALS COURT RELEASES COUPLE OVER NARCOTIC DRUGS TRAFFICKING
Aibu ya watunga kesi za kubumba.
 
Kwahyo unataka kusema kiboko alipohukumiwa miaka 20 mwanzo ,
Kesi yake ilitumika Sheria ipi mahakamani?
Kumtia hatiani?

Money talks mkuu,,
Ushahidi haukuchunguzwa vizuri, baada ya rufaa ikabainika ushahidi ulipatikana kwa njia za ‘kihalifu’, hivyo hauwezi kutumika mahakamani, hivyo wameshinda rufaa
 
My views kuna mapungufu kwenye ukamataji, vidhibiti na mamlaka zinahusiana na kesi zote kuanzia DCEA ambao wanatumia police kukamata, lakini mahakama zetu zinaaminika kiasi gani kutenda haki.

Its well known Koboko ni Kingpin lakini sheria imethibitisha kwamba kulikuwa na dosari katika ukamataji na ushahidi. Ila kama mwamba JPM angelikuwa hai sidhani kama rufaa ingetoka kama ilivyo.

Hisia zinazidi kutawala kwamba Kingpin Mwingine mzanzibari Haji Ally Khatibu alias Shkuba amemaliza kifungo huko Florida anapumzika kidogo Canada kwa familia yake ilipo kabla hajaanza mishe zake, Kingpin Chonji kwa uzito na akili aliyonayo soon atatoka, Candida aka Nsembo abdul huyu haipiti 2025 atakuwa uraiani, Mama Leyla Queenpin huyu kwa uzito alionao Kenya lazima nae atatoka.

Swali ni Why now ?
 
Ushahidi haukuchunguzwa vizuri, baada ya rufaa ikabainika ushahidi ulipatikana kwa njia za ‘kihalifu’, hivyo hauwezi kutumika mahakamani, hivyo wameshinda rufaa
Basi watatoka wote magerezani,,na kubaki wale wafungwa wa wizi wa kuku.

Pesa hupelekea ushahidi kuwa na matundu mengi Sana.
 
Basi watatoka wote magerezani,,na kubaki wale wafungwa wa wizi wa kuku.

Pesa hupelekea ushahidi kuwa na matundu mengi Sana.
Sasa kama huna pesa means hutaweza hata kuaniri wakili wa kukusaidia kushinda rufaa. Kunahitajika somesort of financial muscle kwenye kupata unachotaka, hata haki yako
 
yani polisi ghafla wakikuona una silaha za maangamizi umeingiza kwako wakaja kukukamata na kukupeleka mahakamani na ukutwe na silaha hiyo mbaya unaachiwa kwa kuwa police huwakuwa na search warranty.

Haya ni maajabu ya 8 ya dunia. mama kaupiga mwingi. wacha tukuimbie nyimbo ( mama mama huyo mama mama huyo mama mama huyo)
 
Hahaaaa na bado mkiambiwa nchi ilikua ikiamua kukupa kesi unapewa tu fasta mlikua hamuelewi, Polizirro ndio wanaongoza kwa kubambika watu madawa utadhani wao ni malaika na wataishi milele, sikubaliani na usafirishaji wa madawa ya kulevya lakini nakataa uonevu wa polisi kubambika watu Kesi, nadhani hata Shamimu na Mumewe Abdul watatoka soon,believe me.
Kiboko ni wakubambikizwa kesi kweli? Kama hujui nyamaza tu mkuu. Mpaka siku moja mtoto wako ukute anatoa makamasi kwa sababu ya huyu Kiboko ndiyo akili itakurudi.
 
  • Thanks
Reactions: amu
Kiboko ni wakubambikizwa kesi kweli? Kama hujui nyamaza tu mkuu. Mpaka siku moja mtoto wako ukute anatoa makamasi kwa sababu ya huyu Kiboko ndiyo akili itakurudi.
Maguu...kikubwa ifuatwe sheria ya ukamataji tuu..mbina wamepeleleza hadi kujua kuna madawa ndani..wanashindwa nini kufuata kanuni za ukamataji. Search warrant na ushahidi wake wote..mamana ndio sheria. Polisi wapunguze mazoea tuu katika kazi tuwapate na hatia.
 
Hahaaaa na bado mkiambiwa nchi ilikua ikiamua kukupa kesi unapewa tu fasta mlikua hamuelewi, Polizirro ndio wanaongoza kwa kubambika watu madawa utadhani wao ni malaika na wataishi milele, sikubaliani na usafirishaji wa madawa ya kulevya lakini nakataa uonevu wa polisi kubambika watu Kesi, nadhani hata Shamimu na Mumewe Abdul watatoka soon,believe me.
Kwa utetezi wako huu, moja kwa moja nawe ni mnufaika ama ni don la unga!

Kiboko ama Nsembo wabambikiwe kesi, are you serious?

Kwenye ukamataji wa Nsembo, alikamatwa kwenye paa ambapo alitengeneza"kichali" ndani ya tanki la maji huku mkewe akitetea kuwa mumewe hayupo kasafiri!

Kama ni raia mwema kwa nini ubuni mbinu za kukwepa vyombo vya dola?

Ina maana tuseme, serikali ya awamu ya5 wahalifu walichukua likizo kutenda makosa, hali iliyopelekea Polisi wakose kazi na kubuni mbinu ya kubambikia tu watu kesi?

Ubambikiaji upo sikatai, nalo ni kosa vile vile linalotakiwa kutungiwa sheria ngumu kukomesha uonevu kwa raia.

Lakini hili la ma king pin kupaza sauti kuwatetea ni kuinajisi vita tukufu ya madawa ya kulevya inayopiganwa na wapenda amani nchini.
 
30 March 2022
Ikulu Chamwino
Dodoma, Tanzania


RAIS AJIBU WAUZA UNGA KUACHIWA, AAGIZA "WATOTO WANAHARIBIKA, MMEWAACHIA WANAFANYA NINI?, FUATILIENI"



Mheshimiwa rais Samia Suluhu Hassan wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania atoa ushauri kwa vyombo vinavyohusika na kupambana na madawa ya kulevya yaani DCEA , TAKUKURU, DPP na Polisi muwe makini maana watu wanalalamika...
 
Kama kiboko katoka, basi nsembo na Yangayanga ni suala la muda tu
Kabisa....

Kiboko ametoka?!

Looh..wasiomjua watashabikia...Ila wanaomfahamu huyu kiumbe... Wanalia kilio Cha samaki...

Mbwimbwi ..utamwagwa vibaya ...yaani wamesharudi kuliko zamani!
 
Back
Top Bottom