Mfalme Zumaridi, Mama huyu ni nani na kwanini Serikali imemuacha tu?

Jamani nawasalimia wote kwa kila mtu Na imani yake.
Kule jijini mwanza kumeibuka mwanamama mmoja anajiita Mfalme Zumaridi na Ana kanisa au sijui niseme nini, maeneo ya Nyegezi. Yeye haamini ktk Biblia au Quran yaani ni shidaa .Na Ana watu wengi kinoma Na wafuasi wake wanamsujudu na mpaka wengine wamekua Na alama Kama ya sigda.ukifuatilia clips zake utashangaa ya ni upinga kristo tupu. Wakazi wa Mza na waTz wote tuwe makini Na huyu mtu.

Download link Youtube mp3: HIKI NDICHO ALICHOSEMA MFALME ZUMARIDI
yupo wrong from the beginning,Hairuhusiwi mwanamke kuwa mchungaji,muhubiri,muinjiristi wala shemasi hawajawahi kuwepo kwenye biblia,kwa lugha nyingine mwanamke haruhusiwi kusimama madhabahuni na akawafundisha wanaume,wanawake sababu yeye si kichwa,yeye alidanganywa mwanzo
 
Manabii waliokuwepo,walikuja kwa ajili ya kuutambulisha ulimwengu juu ya uwepo wa Mungu.Walimaliza kazi yao na walirudi kwenye ufalme wa Mungu.Hakuna tena unabii mwingine.Hawa manabii wote wa sasa ni wapiga dili tu,wala siyo wachamungu.Ukiwafuatilia mambo yao utapatwa mshangao wa hali ya juu.
mfalme wavkike na nabii wa kike sio manabii wa kike. kuwa makini mkuu utaliwa
 
Kwa hiyo hayupo mwenye habari zake, za hata kule alikoanzia? Kuna mwingine Nyamanoro anajiita Nabii Rhoda
 
Kwanza umetumia vigezo gani kuita mrembo!!!,mama mtu mzima huyo anajichubua makeup ya njano kama binzari mikono myeusii.

Halafu hata hao samaki aliowazoa na kuwa wafusi wake sijui wana akili gani??hivi majitu yakoje lakini.hapa ndio huwa naona kweli shetani kazi yake ni nyepesi mno.
Akili za walokole wanazijua wenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Samahani huyo mungu mtu ameolewa?
Kwenu wapi weye? Mfalme tena mwanamume wa wanaume aolewe tena!!! Labda uliza hivi; Ameoa?? Mke wa mfalme huitwa "Malkia". Hata yule wa nyuki huitwa malkia ndo maana hutaga mayai baada ya kupandwa na madume nyuki. Sasa weye wataka "Mfalme" aoulewe?? Maajabu gani unatuletea.
 
Habari kutoka kanda ya ziwa kutoka Kanisa la huyu mama Nabii Zumaridi lililopo Mkuyuni mkoani Mwanza

Inaelezwa kwamba Nabii Zumaridi ameamua kuchukua mamlaka ya Mungu chini ya jua, kwamba anajiita Mungu, hali hiyo iliyopelekea kufikia hatua kwa Waumini wake pamoja na wafuasi wake kumwabudu, kumtukuza na kumsujudia.

Anavyofanya huyu mama si sawa kabisa, ifike mahala Serikali ichukue hatua kwa mambo kama haya ya upotoshaji huu.

Na kwanini wahanga wengi wa mambo kama haya ni wanawake..!

IMG_20190325_151315.jpeg
 
Back
Top Bottom