Mfahamu Camilo Cienfuegos wa Cuba!!

Alizaliwa Argentina kwenye mji unaoitvwa ROSARIO; nilibahatika kufika kwenye nyumba aliyozaliwa shujaa huyu tulipotembelea huko na marehemu R.i.P. Patrick Qorro!!
Kifo cha Camilo bado kinautata mpaka.hivi sasa, ukiwa katika mitaa ya zanja y fanta maeneo ya havana vieja mpka leo wana amini camilo alitolewa kafara , wengi wamasema kua camilo alikua kipenzi cha wengi na fidel alihofia pengine akamshinda umaarufu, mwalim wangu wa Judo mkazi wa san antonio de los.banyoz nae pia anaamiji camilo aliuwawa, ingawa wamekua hawaonge hadharani.
 
Kifo cha Camilo bado kinautata mpaka.hivi sasa, ukiwa katika mitaa ya zanja y fanta maeneo ya havana vieja mpka leo wana amini camilo alitolewa kafara , wengi wamasema kua camilo alikua kipenzi cha wengi na fidel alihofia pengine akamshinda umaarufu, mwalim wangu wa Judo mkazi wa san antonio de los.banyoz nae pia anaamiji camilo aliuwawa, ingawa wamekua hawaonge hadharani.
Ila naamini alipishana mtazamona Castro. Ingawa Che Guevara anapinga kuwa Castro na Camilo hawajawahi kuwa na tofauti.
 
Che Guevara alikuwa handsome
Potrait picture ya Che Guavara ndio picha inayoongoza kwa umaarufu ikifuatia picha ya potrait ya Yesu, yaani potrait ya Yesu ni maaruf zaidi ikifuatiwa na potrait ya Che Guevara, ndio maana Maadui zake walimuua na kumpoteza kabisa ili isijulikane amezikwa wapi kwani kuna watu walikuwa kama wanamuabudu
 
Mkuu haya mapinduzi ya cuba yalilenga nini hasa??na mchango wake duniani hasa kwa sisi weusi wa africa Ilikuwa ni nini???
Mkuu labda nikujibu kidogo sehemu ya mwisho ya maswali yako na kwa ufupi sana!!! Mapinduzi ya Cuba yamesaidia sana nchi za Afrika, achilia mbali misaada ya kijamii kama kujenga mashule, hospitali, nk lakini pia Wanamapinduzi wa Cuba wamemwaga damu sana katika ardhi ya Afrika kama nchini Cape Verde, Guinea Bissau, DRC ikiitwa Zaire wakati huo ambapo Che alikwenda kumsaidia marehemu Laurent Kabila. Lakini mchango kubwa wa Cuba ulikuwa katika vita za Angola ambapo jeshi la makaburu wa Afrika Kusini lilikuwa linamsaidia kibaraka Jonas Savimbi. WaCuba wakiwa upande wa serikali ya Angola waliwashinda makaburu na vibaraka wake kwenye vita Cuito Cuanavale 1986 na kuwarudisha nyuma mpaka ndani ndani ya koloni lao la Namibia. Hiyo ilikuwa Mara ya kwanza jeshi la makaburu kushindwa wazi wazi katika uwanja wa vita kusini mwa Afrika. Kushindwa huku kulisaidia sana serikali ya makaburu kuanza kufikiria namna ya kuleta mabadiriko kwenye siasa zake za ubaguzi wa rangi jambo lililotuletea kuachiwa huru Mandela na uhuru wa nchi ile katika misingi ya kura moja mtu mmoja. Hii ni kwa ufupi sana. Muhimu sana historia hii isisahaulike hata Mwl Nyerere aliwahi kunukuliwa akisema anajuta kwanini nchi za Afrika hazikutoa msaada wa kijeshi pale Angola ilipokwenda kuomba OAU wakati huo na badala yake WaCuba ndio waliojitokeza kuiokoa serikali halal ya watu wa Angola.
 
Mkuu haya mapinduzi ya cuba yalilenga nini hasa??na mchango wake duniani hasa kwa sisi weusi wa africa Ilikuwa ni nini???
Ungekuwa mhenga usingeuliza hili swali.Ila ngoja nikujuze.
Cuba imepigana vita vingi kukomboa nchi kadhaa zs Africa mfano Angola na Congo.
Che Guevara yeye mwenyewe na kikosi chake amepigana Congo kumsaidia Patrice Lumumba.
Cuba wametusaidia sana teknologia ya kijeshi,udaktari na ujenzi.
Shule ya sekondari Ruvu imejengwa na wacuba tukapewa bure.
Ni kanchi kadogo ka kikomunist lakini kalikuwa na teknologia ya hali ya juu kiasi cha kuitoa kamasi marekani.
Wamarekani walishajaribu kuivamia Cuba wakatolewa berenge.
Raisi wake marehemu Castrol alikuwa ni commando na field marshal ameshawahi kupona majaribio ya kuuwawa na Marekani mara 600
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom