Mfahamu Andreas Felipe Ballesteros Uribe Raia wa Colombia aliyekaa Keko mahabusu miaka 8 kwa kesi ya dawa za kulevya

Notorious thug

JF-Expert Member
Dec 29, 2021
2,817
10,595
Adres Felipe Ballesteros mzaliwa wa Colombia Bogota mwenye umri wa miaka 36 alikamatwa hapa nchini Tanzania mnamo August 2014 kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya aina ya Heroine akiwa amezifich kwenye pindo la suruali na kete nyingine akiwa amemeza.​
Adres Felipe Ballesteros ni Baba wa watoto wawili ambapo mmoja alimwacha akiwa na miaka 7 sasa 15 mwingine akiwa na miezi 4 sasa miaka 7 mke wake ni Marehemu alifariki mume wake akiwa mahabusu Keko hapa nchini.​
Baada ya kutokupatikana kwenye simu familia yake ilidhani ametekwa na maharamia hapa Afrika Mashariki kama anavyodai kaka yake Juan Carlos Uribe hadi mwaka 2016 walipofahamu amekamatwa na yupo nchini Tanzania ndipo alipofunga safari kutoka Colombia hadi Tanzania kuanza mapambano ya kumtoa mdogo wake.​
Katika mahojiano aliyoyafanya na Radio Colombia Adreas Felipe Ballesteros ananukulia akisema "Gereza la keko lina mahabusu zaidi ya 1,500 hamna chakula wala maji huku joto kali nyuzi 40 watu wana majeraha yanaoza huduma za matibabu hamna askari ni wakatili wanapiga sana mahabusu"​
Adreas Felipe Ballesteros anaendelea kusema alikuja Tanzania kushehereke siku yake ya kuzaliwa alikua aende visiwa vya Zanzibar ila kufika uwanja wa Ndege alikamatwa baada ya Visa yake kuonyesha anatokea Colombia na sababu kubwa ni Colombia kujulikana kama nchi inayohusika na usafirishaji na uuzaji wa madawa ya kulevya.​
Adreas Felipe anasema Mifumo ya haki Tanzania ni Katili na imejaa Rushwa Mawakili hawafuatilii kesi wanataka kupata fedha nyingi haswa wanapokuona wewe ni Ngozi nyeupe.​
Kaka yake Juan Carlos Uribe anarudi nchini Colombia mwaka 2021 na kurudi na mwandishi wa haki za binadamu na mbobezi wa usawa katika jamii na kuanza mpango mahususi wa kumnasua ndugu yao kutoka Keko baada ya majadiliano ya muda na DPP inashindikana kumtoa kutokana na uongozi anaodai ulikuwepo madarakani baada ya uongozi mpya kuingia madarakani wanaendeleza majadiliano na DPP mpya baada ya kupoteza hela nyingi kwa DPP wa zamani.​
DPP anamwambia Adreas Felipe Uribe kwamba anatakiwa alipe $25,000 au kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani ndipo Andreas Felipe Uribe anafanikiwa kuwasiliana na ndugu zake na kuanza harambeee ya kumchangia hela kupitia mitandao ya kijamii hususani Twitter na kufanikiwa kulipa kiasi hicho na kuachiwa huru.​
UPVTBNMR5ZEYVBDSCNPYFIIYQQ.jpg
Tras-preso-ocho-anos-en-Tanzania-Andres-Felipe-Ballesteros-llego-a-Colombia2.jpg
Tras-preso-ocho-anos-en-Tanzania-Andres-Felipe-Ballesteros-llego-a-Colombia1.jpg
_FDA0323.JPG
_FDA0325.JPG
Mume wangu.JPG
UF7I5QWEUZGZFPWJSHN4Q5CCQY.JPG
 
Sasa imagine hadi raia kama wa columbia ambao tunajua ni nchi ya ovyo km kwetu wanalalamika tz ni shida na wanaona bora kwao kuliko tz.

Hapo yupo keko gereza la kishua angepelekwa kilosa huko si ndo angesema yupo jihanam kabisa.

bongo nyoso..
 
Tena ashukuru mungu kuna Sheria ya plea bargaining huyu jamaaa angefia jela alikuwa na gram 958 alikutwa nazo kwenye suruali na nyingine alikuwa kameza ziilitolewa kwa njia ya choo maalum pale JNIA huyu alitumwa kuleta madawa ya kulevya bongo baada ya kushindwa kulipa deni alilokuwa anadaiwa huko kwao ,alikuwa anamdai akammwambia kama huwezi kunilipa deni langu nisafirishie mzigo wangu Dar es salaam.Ndio kukamatwa kwake.otherwise ni mtu poa tu na inaonekana lilikuwa ni ndio mara ya kwanza huko kwao Colombia ndugu yake aliwaaminisha kwamba anaonewa hapa Tanzania lakini alipohojiwa na kituo kimoja cha TV kila raia aliyechangia walimwita muongo wakihusianisha story yake ya kuja kutalii Tanzania kusherekea birthday akiacha familia.hata HIVYO ni maisha tu ni mtu poa tu mshikaji sana pale KEKO.
 
Back
Top Bottom