Meseji ya mke wangu kwa mama yake inamtuhumu mama yangu kuwa ni mchawi

Uchawi ni siri kubwa kaka.... Kwa kuambiwa huwezi amini hasa kwa mama yako hapo usimuone mkeo mbaya Wala mama yako chunguza kwa unavyojua ww utapata ukweli.
Amina ndugu nitalifanyia kazi
 
Mama yangu hata kama mchawi anatakiwa ampende tu .
Dawa ya mchawi ni kuwa karibu naye.
Ukiona mwanamke anamsingizia mtu uchawi jua hampendi
Kweli mkuu japo busara inatakiwa
 
Hajakosea, bali wewe uko very harsh, kwa hiyo ameshauriwa aitume kwako kwa staili hiyo ili ujumbe ukufike.
Kuupata ushahidi wa kuwa mother ni mchawi ni ngumu, cha msingi kaa na mkeo.Mpe moyo juu ya hilo kwamba ujumbe umeupata na utaufanyia kazi.Isipokuwa, mwambie awe na amani kwa kuwa hata wewe(mleta mada) unauchukia uchawi.
Mwisho wa siku, endelea kusali/kuswali nae(kwa kadri ya imani yenu) pamoja ili aendelee kukuamini zaidi.
Amina mkuu asante kwa ushauri
 
Kwanza muonyeshe sms, halafu mwambie akuthibitishie pasi na shakayakuwa mamako ni mchawi, kabla hajajibu muulize kati ya wewe (mwanaume) na mama yake mzazi nani zaidi, kabla hajakujibu mwambie ni mama yake ndiye bora kwake maana damu ni nzito kuliko maji. Kabla hajakujubu mwambie na wewe ni hivyohivyo.
Mwambie kama anataka maisha ya ndoa yaendelee basi aweke mbali imani za ndoto na kishirikina na amtangulize Mungu maana yeye ndie muweza. Mwambie hata wewe ulishaota sio chini ya mara 6 kuwa alishatoa sana mimba ndio maana mimba ya kwanza iliharibika, je na wewe utuhumu kama yeye anavyofanya.
Baada ya hapo funga mjadala na usiujadili tena.
Utamuacha na maswali yasiyo na majibu yakimtafuna na siku akipata nafasi ya kuomba msamaha ndio atatua mzigo wake.
Asante mkuu kwa ushauri wako murua
 
kwenye familia zetu haya yapo sana.mm ililishampekua mama yangu mzazi baada ya kudaiwa kamuua baba yangu. kua makini tayari familia yako inatatizo.jitaihidi kulimaliza taratibu usije ukaliongeza maana mama yako akijua anaitwa mchawi ni balaa. mama yako wala si mchawi uwe na amani .kua karibu na mkeo zaidi mwenyeshe upendo zaidi mawenge yataisha
 
Kuna ka uzi kauganga na bihashara isijekuwa umeua mtoto wa tumboni upate Mali nyingii ooooh ITAKUTOKEA PUANI na hapa jf hutokuja maana itakuwa ni aibu japo twatumia fake IDs!
 
Kuna ka uzi kauganga na bihashara isijekuwa umeua mtoto wa tumboni upate Mali nyingii ooooh ITAKUTOKEA PUANI na hapa jf hutokuja maana itakuwa ni aibu japo twatumia fake IDs!
Duh mbona huo uzi wa hiv karibuni na inshu ya mtoto ni miezi sita sasa,mbona uzi wangu mnauunganisha sana na uzi wa uganga jmn?
 
Mimi hata ikitokea mama yangu kuwa mchawi siwezi kumtetea Hata kidogo, sana sana nitamwambia akautupe baharini, au akapeleke kwa madhabahuni akajisalimishe ili kujiokoa yeye na uzao wa tumbo lake ingawa kukubali kufanya hivyo inahitaji Neema maalum ili akubali kuacha maana siyo rahisi ingawa inawezekana kabisa kuacha! Mchawi Hata akiwa mama yako mzazi usuje shangaa Siku ikifika zamu Yake ya kutoa nyama akamtoa mtoto wake wa mzaa akafa Kwa Mazingira ya kutatanisha! Kwa hiyo mleta mada nakushauri ufanye subra huku ukifanya uchunguzi wa Polepole utakuja kujua Kama ni Kweli Au la!
 
Fuatilia kujua tangu zamani Watu humnena kuwa ni Nani, Je alishawahi singiziwa kuwa ni mchawi? N.k uzoefu unaonesha baadhi ya wanaosingiziwa huwa ni Kweli kuwa ni wachawi !
 
Kwanza you need to know hiyo message haijakosewa kutumwa (crossposted) kama unavyodhani...ni intention kwamba upate ujumbe.
Pili, kaa fanya uchunguzi...ongea na mkeo
 
Back
Top Bottom