Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,331
- 33,141
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii wa Tanzania, Chikambi Rumisha
amesema meno hayo yapatayo 81 yana uzito wa kilo 303.
Kwa mujibu wa maafisa wa Wizara meno hayo ya tembo ni mapya ikiwa na maana yametokana na tembo 41
waliouawa ndani ya mwezi mmoja uliopita.
Naibu Waziri wa Maliasiali na Utalii wa Tanzania Lazaro Nyalandu amesema mauaji ya tembo yameongezeka
nchini humo baada ya operesheni ya kupambana na majangili iliyopewa jina la "Operesheni Tokomeza"
kusimamishwa kutokana na baadhi ya watendaji kukiuka haki za binadamu.
Mapema wiki hii Naibu Waziri huyo amesema tembo wapatao 60 wameuawa kati ya mwezi Novemba na
Decemba ikilingalishwa na tembo wawili waliouawa mwezi Octoba. Chanzo: bbcswahili
TANZANIA BILA UJANGILI HAIWEZI KWENDA KABISA KAZI KWELI KWELI IPO HAPO.