Mengi vs Manji: Ukweli ni upi?

Tanzanianjema,hatukatai kama nchi inaoza ama imeoza,lakini tuwe na hoja,tusiwe watu wa jazba,lete hoja lete ushahidi,sio unaleta hoja huna ushahidi nayo.sie sio watu wa jumbe ndio,we have to hoji why?how?sio mtu kaleta hoja basi unaivamia tu tanzanianjema.
 
mwanasiasa lazima ujue,nini ilikuwa kesi ya msingi,usi seme tu Manji firauni kawashika,nssf,ccm sijui ikulu,No kesi ya msingi ni kuwa Mengi anatumia vibaya vyombo vyake vya habari,kesi hii it has nothing to do with manji.Its between Mengi and malima thats it!!!Alipoulizwa Mh malima unao ushahidi juu ya hilo?akasema ndio ndipo alipowaleta akina Dr Dau,Sheikh Bassaleh,Jaji Warioba na wengine.hao wote wamekwenda katika kamati ya maadili KUTIBITISHA KAULI YA MH MALIMA JUU YA MENGI NA MATUMIZI YAKE MABAYA YA VYOMBO VYAKE VYA HABARI.Kwanza nakutaka ujue,sheria ya vyombo vya habari ulimwenguni,HAIMTAKI mwenye chombo cha ahabri kujionyesha yeye katika Prime time kama taarifa za habari,ndio maana huwezi kumuona mwenye SKY NEWS katika TV,lakini mengi kila kukicha juu katika taarifa za habari,leo kafungua choo,kesho katoa msaada katika Madrasa msasani.Sheria inamtaka mwenye kumiliki chombo cha habari hususan Tv kutojionyesha yeye mmiliki ktika prime akama akitaka hayo,basi aweke kipindi maalum,na ndio maana kama utakumbuka siku za nyuma amejoinyesha akitoa mdsaa katika kipindi maalum sio katika NWES TIME.Kwa kujionyesha yeye katika news time ITS CRIMINAL OFFENCE,haya kama huyajui mwanasiasa nakutaka uyajue kuanzia leo,waulize wanaosemosea mambo ya Media,au waulize TCRA pale ilipokuwepo SHIHATA zamani wale ndio wanaotoa lesseni.
 
Mzee wa london

sheria ya vyombo vya habari ulimwenguni,HAIMTAKI mwenye chombo cha ahabri kujionyesha yeye katika Prime time kama taarifa za habar

Kwa kujionyesha yeye katika news time ITS CRIMINAL OFFENCE,


Unaweza ku-prove maneno haya?
 
Lakini has been siding with CCM all these years , alifikia mahala pa ku potrya wapinzani kama Mamluki na kwamba watamwaga damu kama Burundina Rwanda and CCM has always been happy with that . Leo what went wrong ? Na mambo ukiangalia vyombo vyake ya habari ni pro CCM akiwemo Malima ambaye hana msimamo maana kahama vyama na kaamua kula karudi CCM. Mengi akiamua kutumia vyombo vyake vya habari vulivyo nasema kesho CCM inaanguka madarakani na wanamfunga ila kwa kuwa anakula nao basi tena . Hiyo sheria mimi binafsi sijawahi kuisikia naomba kueleweshwa tafadhali na baadaye watueleze ila kuandika habari upande mmoha ambayo Mengi anatumia kuwapa CCM mlo.

Malima na mashahidi wote ni wale ambao wamekuwa exposed kwa uozo na magazeti ya This Day na Kulikoni kupitia Mengi lakini yale si magazeti ya Mengi kila mmoja anaujua ukweli hapa . Ushahidi gani dau kaenda kutoa ambao haukuwa kwenye kuonekana LIVE hadi Malima akaropoka Bungeni ? Nina swali . Je kwa kuuliza na hata kusababisha walipa kodi kuliwa pesa zao 100m Malima kawasaidiaje watu wa Mkuranga ?

Mwisho nasema wale wameenda kutoa ushahidi wa kuwa wako na Manji wote .Nani hajui kwamba ni baada ya kusemwa na magazeti ya Kulikoni na This Day ndipo Union yao imeanza kulia na Mengi ?
 
Mzee wa London...I second you. Na hicho ndicho alichookuwa akiulizia Mh Malima.Kama kuna policy inayo-guide wamiliki wa media ku dominate...news etc issue ya Mengi aliitoa kama mfano. Sasa naona ile pint muhimu haijafafanuliwa na Wizara husika au TCRA...badala ya 100m zinatumika kuendeleza "ego" za watu . Nina wasiwasi kama tutaiendeleza nchi hii kwa stail hii ya " ku maintain ego za watu." Bunge nalo lina entertain ishu binafsi za watu kuendeleza visasi.
 
Mzee wa london




Unaweza ku-prove maneno haya?

Ole,
Hoja hizo hapo juu (zilivyotolewa na Mzee wa London) zimenigusa kwani nami nimekuwa nikizifuatilia tangu juzi.

Binafsi niliwahi kufahamishwa hivyo; kuwa ni makosa kwa mmiliki kutumia chombo chake cha habari ambacho ni kwa ajili ya umma kwa kujitangaza binafsi-kitu kama hicho. Nafikiri neno mojawapo lililotumika kwenye Kiingereza katika sheria/kanuni/itifaki hiyo ni "reasonable". Yaani kama mmiliki atalazimika kuonekana basi iwe ni "reasonable" au muda atakaotumia uwe ni "reasonable". Sasa najua kisheria wakati mwingine ni vigumu kukubaliana kuhusu nini ni "reasonable".

Tangu juzi nimekuwa nikitafuta uwezekano wa kupata hiyo rejea yenye kuelezea suala hili lakini sijafanikiwa.

Nadhani pia kuna sheria/kanuni/itifaki ambayo hairuhusu, kwa mfano, mtangazaji wa kituo kimoja cha TV kuonekana akiongea katika TV nyingine labda pale ambapo vituo hivyo vinarusha matangazo yao kwa wakati ule kwa pamoja; au labda awe anashiriki katika kipindi kingine maalum cha TV katika kituo hicho ambacho si chake, kama mchangiaji mada fulani. Inasemekana hii ni kwa ajili ya kuepusha kuwachanganya watazamaji wa vituo hivyo.
 
hamna kitu kama hicho. wewe sema hiyo sheria inaitwa au ilitoka mwaka gani, sisi tutapekua kwani tuna access na sheria zote kuanzia enzi ya Mwingereza.

jamani mzianze kuanzisha sheria za alinacha na nduguze hapa.

toa rejea ili ueleweke.
 
Nakushukuru mwanagenzi maelezo yako makini kabisa,hiyo sheria ipo ila siikumbuki,lakini all in all ngoja niitafute give me time.Aljazeera nikisha ipata hiyo sheria ndio utaamini kuwa Mengi anatumia vibaya vyombo vyake vya habari?
 
Kuhusu ITV kuwa ni TV ya taifa ama la ni hoja ambayo haina jibu la moja kwa moja. Kwanza Lowasa kabla ya kuzungumzia rushwa ana hoja ya kujibu kuhusu kesi husika na angeitwa na kamati kabla hata ya rushwa kuibuka kwani Malima alimtaja Lowasa na Kikwete (Rais JK) katika bunge kwamba wanapewa dakika moja na nusu (sijui kama kazithibitisha) kuliko Mengi anayepewa dakika kumi (hawezi kuthibitisha, taarifa ina dakika 20, hakuna mtu anayeweza kutumia dakika kumi).

Kwa kutajwa na Malima, Lowasa angeitwa kuulizwa kama alimtuma Malima kuuliza bungeni kwa kuwa haridhishwi na muda anaopewa na kama aliona Malima kamsingizia, akiwa Kiongozi wa Serikali Bungeni (JK huwa haingii bungeni) Lowasa angesimama na kusema kwamba, "Malima umesema uongo, mimi nilipewa dakika tatu na si moja na nusu na kwa kweli sihitaji dakika zaidi labda kama ni kipindi maalumu" na pale Spika angemtaka Malima afute kauli na leo tusingekuwa na yote haya. Lowasa hakusimama kukanusha kuwa hajapewa muda mdogo, Lowasa hajaitwa kuulizwa kama anaridhika na muda na kama haridhiki, alimtuma Malima? lakini kabla ya kuitwa, kunaibuka hoja kwamba Lowasa kagundua wabunge WAMEHONGWA na Manji! Amejuaje? Lakini pia ukiangalia MALIMA KUMTETEA KUWA ANAPEWA MUDA MDOGO na YEYE (EL) KUMSHAURI MENGI AJITOE KWANI WABUNGE WAMEHONGWA NA MAJI, ni hoja inayozidi kuibua utata na kumuunganisha moja kwa moja na hoja husika. PICHA SASA Inamuunganisha moja kwa moja na vikao ama MTANDAO wa kumshughukikia MENGI, kuanzia na kauli ya MALIMA bungeni na RUSHWA katika Kamati
 
sheria ya vyombo vya habari ulimwenguni,HAIMTAKI mwenye chombo cha ahabri kujionyesha yeye katika Prime time kama taarifa za habar

Kwa kujionyesha yeye katika news time ITS CRIMINAL OFFENCE,

Unaweza ku-prove maneno haya?

Hata mimi nasubiri kwa hamu sana uthibitisho huu!
 
Lakini has been siding with CCM all these years , alifikia mahala pa ku potrya wapinzani kama Mamluki na kwamba watamwaga damu kama Burundina Rwanda and CCM has always been happy with that . Leo what went wrong ? Na mambo ukiangalia vyombo vyake ya habari ni pro CCM akiwemo Malima ambaye hana msimamo maana kahama vyama na kaamua kula karudi CCM. Mengi akiamua kutumia vyombo vyake vya habari vulivyo nasema kesho CCM inaanguka madarakani na wanamfunga ila kwa kuwa anakula nao basi tena . Hiyo sheria mimi binafsi sijawahi kuisikia naomba kueleweshwa tafadhali na baadaye watueleze ila kuandika habari upande mmoha ambayo Mengi anatumia kuwapa CCM mlo.

Malima na mashahidi wote ni wale ambao wamekuwa exposed kwa uozo na magazeti ya This Day na Kulikoni kupitia Mengi lakini yale si magazeti ya Mengi kila mmoja anaujua ukweli hapa . Ushahidi gani dau kaenda kutoa ambao haukuwa kwenye kuonekana LIVE hadi Malima akaropoka Bungeni ? Nina swali . Je kwa kuuliza na hata kusababisha walipa kodi kuliwa pesa zao 100m Malima kawasaidiaje watu wa Mkuranga ?

Mwisho nasema wale wameenda kutoa ushahidi wa kuwa wako na Manji wote .Nani hajui kwamba ni baada ya kusemwa na magazeti ya Kulikoni na This Day ndipo Union yao imeanza kulia na Mengi ?


Mengi hana ugomvi na CCM na wala hana ubavu wa kuwa na ugomvi na CCM. Ana ugomvi na Manji na Malima, huu umoja umeundwa kwa makusudi ili kumlinda Malima lakini hasa ni kumuumbua Mengi ili kumfurahisha Manji. Malima aliropoka bila kujua anachosema na pengine wala hatugemea kama Mengi angelalamika kwenye kamati ya bunge.

Ni kukundi kidogo sana ndani ya CCM ambacho kinautata na Mengi kwanza kikundi chenyewe wala sio Heavy Weights.
 
Yusuph Manji ni kijana kama angekuwa mswahili watu wangesema anatumia majini. Huyu bwana anogopwa na kuheshimiwa na kila mtu ambaye kwa namna moja au nyingine anafaidika anye. Utashangaa kuona hata wale mawakili wake wa Professional Center wanavyokwenda kasi akienda kuwatembelea ofisini kwao - wanatamanio hata wambebee karatasi alizoshika mkononi.

Mr. Mengi, pamoja na kuwa mara nyingine vyombo vyake vya habari huchukua muda mwingi kutangaza mabo yake, ambayo naona ni muda unaolingana na jinsi hivyo vyombo vinavyoifagilia serikali ya CCM NAKUMBUKA WAKATI FULANI MIAKA YA TISINI ALISHA WAHI KUULIZWA NA WAANDISHI WA HABARI NI NINI AZMA YAKE KATIKA SIASA.. ALIWAJIBU KWAMBA YEYE NI MFANYA BIASHARA, HIVYO HATOWEZA KUFANYA VIZURI ZAIDI KATI YA KIMOJA WAPO ENDAPO VYOTE ATAVICHUKUA KWA MARA MMOJA!!

Mzee wa London, unamjua Adam Malima kuwa ni mtoto wa marehemu Kighoma Malima? kakaa mno London, muulize alikuwa anishi huko kwa gharama ya nani???
 
Nakushukuru mwanagenzi maelezo yako makini kabisa,hiyo sheria ipo ila siikumbuki,lakini all in all ngoja niitafute give me time.Aljazeera nikisha ipata hiyo sheria ndio utaamini kuwa Mengi anatumia vibaya vyombo vyake vya habari?

Haya makubwa tena! Yaani mnaanza kwa kunukuu sheria halafu ndio mnaitafuta? Mwee hii kali. Kama alivyosema Al jazeera hakuna sheria akama hiyo. Sky News wasipomtajataja mmliki wake ni kwa sababu hicho anachofanya kwao siyo News. ITV na magazeti ya Mengi kwao anachofanya Mengi ni News. Ina maana TVT na RTD wanatakiwa wasitoe habari za serikali kwa sababu serikali ndiyo mmiliki wake? Acheni fiksi hizo jamani
 
Makubwa haya!

Hivi Mengi kama mfanya biashara anatakiwa kumtaja rais mara ngapi vile ili ikubalike?.. Je, serikali ina hisa ama hutoa kiwango fulani cha fedha kwa Mengi kuhakikisha wanatangzwa?...
Na sheria ya kupata kibali cha utangazaji habari -News huwa zina vipengele vipi hasa ambavyo vinamfunga Mengi ktk kukiuka sheria.

I mean haya maswala sielewi kabisa yanahusu kitu gani bunge letu kiasi kwamba badala ya serikali kuweka kikao maaalum cha Richmond, Rada ama IPTL wameshikilia kunyoosheana vidole utafikiri wapo uswahilini wakisukana nywele, samahani mh. ndugu Spika!

Who said/he said inahusu nini kweli kikao kizima kutafuta udaku wa kusutana ati nani kaanzisha?....
Hivi kweli waziri mkuu mzima awe na habari ya rushwa badala ya kuchukua hatua inapita udaku kwanza, kisha mkosa ni yule aliyepokea udaku!. I mean what's going on Bongo jamani hakuna maswala ya maana zaidi!
Ikiwa kuna wabunge wamepokea rushwa hili halina mjadala!..na wala sioni sababu kwa swala zima kuwa bungeni....period!
 
Wanabodi,
Hoja iliyo mbele yetu (Tuhuma za Rushwa kwa Kamati) ilitokana na hoja kuu nyingine (Malalamiko ya Bw Mengi dhidi ya Mhe Malima na kinyume chake). Maswali makuu mawili katika hoja hii ya "Malima na Mengi" ni je, Mwananchi anaweza kumsema (kumshambulia kwa maneno) Mbunge kwa hoja aliyoitoa bungeni? na je, Mbunge anaweza kumsema (kumshambulia kwa maneno) Mwananchi nje ya bunge?

Wakati tunachangia humu, kwa kujua, ama kutojua, tumekuwa pia tukichangia kuhusu hizo hoja mbili kama nilivyoainisha hapo juu.

Kwa ufupi niseme yafuatayo:

1. Hoja kuu ya Bw Mengi dhidi ya Malima (MB) ilikuwa ya msingi na yenye kuibua utata au tafsiri ya kisheria kuhusu mamlaka ya bunge ndani na nje ya bunge. Wengi wenu bila shaka mtakumbuka kuwa hata wakati wa Spika Msekwa, ilifika mahali watu wakaitwa wajieleze kwa nini "wamelisema" bunge nje ya bunge. Baadhi ya wananchi walilalamika kuwe Bunge "lao" limekuwa "si lao" na limekuwa "untouchable". Ndiyo maana nakubaliana na Mhe Sitta (Spika) kuwa ilikuwa vema pesa za walipa kodi zitumike ili kufikia mwisho mzuri wa tafsiri hizo za kisheria na mamlaka ya bunge nk. Si kuna msemo demokrasia ni ghali! Kwa maana hiyo hoja hii ni muhimu na ina maslahi kwa taifa na si kupoteza wakati kama baadhi yetu tunavyotaka kuchukulia. Huenda ni jazba tu kutokana na kukatishwa tamaa na ripoti mbalimbali huko nyuma ambazo hazikufanyiwa kazi kama wananchi walivyotarajia.

2. Tuhuma za rushwa ndani ya kamati zinapaswa kushughulikiwa. Kwangu mimi ingependeza kama wote waliohusika/waliotajwa kuhusika wafuatiliwe na TAKURU.

3. Pamoja na kwamba mtu/mwanachi ana uhuru wa kuanzisha, kuendesha na kumiliki chombo cha habari, lazima kuna taratibu zifuatwe. Hata kama chombo ni mali binafsi, lakini maadam ni kwa ajili ya umma, basi lazima kuangalia aslahi ya umma (public interest). Kwa bahati nzuri au mbaya, Tanzania ina Sera ya Habari ya mwaka 2003. Huenda sera hiyo haikubaliki kwa kila mtu, lakini hilo ni suala lingine. Pamoja na mambo mengine, sera hiyo kuna mahali inasema:
"Private-owned radio and television stations must participate fully in nation building and in national campaigns and disaster" (§ 2.7.3).

Pia kuna vitu vingine kama vile "content" iweje, "local programmes" ziwe nyingi kiasi gani (isiwe tu foreign programmes) na hata lugha ambapo sera inasema ni Kiswahili na Kiingereza tu! Hata hivyo inawezekana kwa kibali maalum wakaruhusiwa kutumia lugha tofauti. Nasikia kuna redio ilikuwa ikiwalenga Wamasai hivyo ikawa inatumia Kimasai; sijui kama bado hilo lipo au la. Pia kuna redio walitumia Kisukuma wakapigwa "top". Nadhani nao wameacha hilo, unless kama wana kibali maalum. Huku Ngara kuna Radio Kwizera, kwa vile ni kwa ajili ya wakimbizi (zaidi) wa Rwanda/Burundi basi wameruhusiwa kutumia Kinyarwanda/Kirundi.
 
Mwanagenzi,
kwanza navyofahamu mimi hiyo namba 3 inatangulia yote haya kwani ndilo chimbuko la namba 1 na 2.

Well, Ukitazama vipindi vya Tv ya Mengi sidhani kama kuna ukiukaji wowote wa sheria ulozitaja. To participate fully haina muda wa kusema kila baada ya dakika fulani lazima mabo haya yatajwe. Taarifa za habari zipo, Vipindi vya ujenzi wa nchi vipo na vipindi vya burudani vipo, lakini sijawahi kuona kupangiwa nini cha kuzungumza na wahusika wake..
Kifupi, mengi ni mfanya biashara ambaye atapenda sana kuitangaza nchi na TV yeke iwe inatazamwa sana na wananchi. Sidhani kama kweli kuweka sura yake ama sura ya JK ni biashara ama kuijenga nchi.. Maswala muhimu huzungumziwa iwe kwa negative ama positive maadam malengo yake ni kukosoa ama kuelekeza nini kifanyike. Ni ujinga mkubwa kutazama ama kuweka madai kuhusu sura ya nani inayotoa message hiyo ama hutokea zaidi.

Pili, swala zima la rushwa limekuja tokana na uzembe ulikuwepo toka mwanzo, na mfano wa spika Sapi kuita watu kujieleza ktk who said what hali maneno hayo hayajengi wala kubomoa uchumi wa taifa ni kupoteza muda. Ikiwa kweli Sitta anataka swala hili liwe wazi basi ifunguliwe kamati mpya ya kuchunguza RUSHWA bungeni kisha mashahidi wataitwa kulingana na shitaka lenyewe na sio shitaka moja kuchukua mkondo mwingine katikati kupoteza mwelekeo wa shitaka la kwanza.

Hapa inatakiwa kesi mbili tofauti na ndio maana hata ktk kesi za jinai huwezi kuunganisha na kesi za madai kuwa kesi moja hata kama zinahusiana.

Nafikiri labda babu ubishi hapa nianze kuchukua law maanake uzembe mkubwa sana unafanyika!
 
Kuna Mtu kamuweka Prof.Safari kuwa anaweza kuwa DPP. sijui kaweka kwa mantik Gani. inawezekana walewale walio na dhana zao..utamalizia mwenyewe. Infact prof.Safari ana kesi dhidi ya serikali ktk madai ya kuondolewa Pale Chuoni eti kwa kuwatetea Prof Lipumba.na wao wakidai yeye ni CUF. Fautilieni hilo mjue. na JK anahusika kwani ni yeye ndie aliekuwa bosi wa Foreign Affairs na ndiyo yenye mandate ya Chuo cha DIplomasia..Achane dhana mbaya kwa watu...
 
Chuma,
Nadhani wewe ndo uachane na dhana...
Hayo uliyoyasema tunayajua, na mengine pia...
Kwa mfano, unajua kuwa huyo mwanazuoni huko nyuma alikuwa akifanya kazi ofisi hiyo ya DPP na akawa amefikia ngazi ya juu tu?
Unajua kuwa pia ashawahi kutumiwa na PCB kuwaendeshea mashtaka katika kesi zao wakati huo ambapo baadhi ya watu walimwona na kumhisi kuwa anawasaidia CUF?
Huwezi kudhani kuwa akipewa hiyo nafasi na kesi yake dhidi ya chuo hicho inaweza ikafikia mwisho wake??
 
Ni kwa nini R.Mengi anaogopewa kuliko JK?
Hili ni swali jembamba sana lakini lina majibu mapana sana,
kama swali halijaeleweka ninaomba mliweke vizuri,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom