minyoo
JF-Expert Member
- May 25, 2013
- 21,647
- 20,382
Ulinipeleka wewe?
Vipi mgonjwa wako nyaulingo anaendeleaje kaanza kutembea sasa? Miguu imepona,?
Ulinipeleka wewe?
Vipi mgonjwa wako nyaulingo anaendeleaje kaanza kutembea sasa? Miguu imepona,?
Haahaa dunia kweli duara, aliyekuwa waziri Wa mambo ya nje Leo analalamika kama sie RAIA.hili Ni somo kwa waliopo madarakani Leo wasidhani watadumu mamlakani milele.Ila membe kwa misemo hatari, eti wabwekaji Wa taifa.
wasije wakawa wanatafuta kumuwowa kama amesifiwa hivyo... wanamume hawasifiwiEti Musiba ndio Good looking mwenye sura ya kuvutia handsome kulikowwanaume wote mkoa wote wa mara.
Mpelekeni mahakamani si kumchafua kila siku kwenye magazeti na mitandao ya kijamii. Majungu tu.
Wabwekaji wa Taifa..!! Mmh ngoja niingize kwenye hansard yangu.. Kwa hiyo hata mm ninaemtetea usiku na mchana Mh. Rais wangu Magu ni mbwekaji wa Taifa.?
Hivi huwa mnamtetea rais dhidi ya nani na kwa nini?Je kumtetea na kumkinga ili asikabiliane na waajiri wake mnamaanisha kwamba hatoshi kwa nafasi aliyoiomba mwenyewe,au ni ujinga wenu tu?Wabwekaji wa Taifa..!! Mmh ngoja niingize kwenye hansard yangu.. Kwa hiyo hata mm ninaemtetea usiku na mchana Mh. Rais wangu Magu ni mbwekaji wa Taifa.?
Wabwekaji wa Taifa na matumbo yao, jitu zima likishakuwa livivu la.kufanya kazi likajipatia kipato, linaishia kuwa liilmba kwaya za kuwafurahisha maditete na kujiaibishaAnaandika Bernard Membe.
Rondo- Lindi.
Watanzania Wenzangu! Nawasalimia! Kwa siku tatu mfululizo magazeti ya makuhani wa fitina na unafiki Musiba na Mchange na wenzao wamekuwa wakinishambulia kwa uchochezi wa sintofahamu iliyotokea kuanzia Alhamisi tarehe 17 Octoba siku ambayo Mhe Rais ameondoka Lindi kuelekea Dar hadi Jumapili ya tarehe 20. Mimi nipo Kijijini kwangu Rondo kwa mwezi mmoja sasa.
Ni nini hicho nilichokisema au kukiandika kwenye mitandao ya kijamii? Kwa kuwa mawasiliano yangu yote nayafanya kwa simu yangu ambayo inasikilizwa na kudukuliwa, naviomba vyombo vinavyohusika vitoe hadharani mazungumzo na maandishi yangu ili watu wasikie, wasome na wanihukumu. Napenda niuhakikishie umma kuwa Mimi sikuwa mjinga! Nilijua kuwa nikisema au kuandika vibaya, wabaya wangu wataninyooshea vidole.
Sikuingia kwenye mitego yao hiyo. Mimi kama Watanzania wote wenye akili za kawaida nilishangazwa sana na ukimya wa Serikali huku damage na rumours zikiwa zimetanda kote nchini bila kuzitolea maelezo kwa siku 3 mfululizo! Mhe. Rais ni kiongozi wa Umma. Inapotokea sintofahamu au upotoshaji wowote ule, ulikuwa ni wajibu wa Msemaji wa Ikulu au wa Serikali kukanusha na kuweka mambo sawa kama wanavyofanya siku zote.
Vinginevyo wale wenye akili za mbilikimo na makuhani wa unafiki wanachukua mwanya huo kutunga ya kwao ili kumfurahisha Mhe. Rais. Good governance requires quick response to rumours. Rumours left unattended damages governance! Narudia! Naviomba vyombo husika vitoe hadharani nilichokisema au kupost kwenye mitandao ili nihukumiwe na Wananchi wenyewe na sio na Wabwekaji wa Taifa.
Ben Membe.
Rondo- Lindi.View attachment 1241102View attachment 1241103
wasije wakawa wanatafuta kumuwowa kama amesifiwa hivyo... wanamume hawasifiwi
Ulikuwa wapi wr mnafiki mbona ulipotea baada ta kufufka na wewe umeibuka kama mzuka. hahhaaaa wanafiki nyie.Sikubaliani na Membe.
Ilichokifanya serikali nadhani ndicho kilikuwa sahihi.
Kwamba, tetesi za kijuha na kipumbavu, ni vyema kuzipuuza kwa maneno lakini pia kuzijibu kwa vitendo ndani ya muda mzuri.
Rais kujitokeza na kuendelea kufanya kazi zake, lilikuwa ni jibu murua kabisa kwa majuha wote walioshiriki kutunga na kueneza uzushi wao.
Hivyo ndivyo inavyotakiwa.
Msemaji wa serikali akianza kujibu kila aina ya uzushi, kufanya hivyo ni kuubariki na kuuhalalisha uzushi huo. Serikali itafanya hivyo kwa mangapi? Maana uzushi na uongo ni sehemu kubwa sana ya hii mitandao ya kueneza na kujazana ujinga.
Safi sana serikali. Safari hii mmetenda vyema.
hatuwezi kumuunga mkono DiktetaMembe arudishe tu mabilion ya Watanzania aliyopora kutoka libya
Jamhuri ikiamua kumshitaki atafilisika
Pia sio vizuri kuwatumia vijana kubweka mtandaoni kuisema serkali
Tuendelee kumuunga mkono mh Rais Kwa uchapa kazi
#NIGUSE NINUKE#Wabwekaji wa taifa?!!!.......... Huu ni msamiati mpya!
Wabwekaji wa taifa?!!!.......... Huu ni msamiati mpya!
Yaani uko dunia gani Musibaaaaaaaaa njoo huku kuna huyu tenaWaziri alimkanya Musiba, lakini Musiba ameendelea kuisemea serikali na hachukuliwi hatua, maaskofu waliiuliza serikali ikiwa haimzuii Musiba na wengi wanaamini serikali inamtuma, kwanini serikali isijitenge naye na asiruhusiwe kuisemea serikali, na imchukulie hatua.
Waziri alimuonya hadharani na alisema akirudia vyombo vya dola vita mshughulikia.
Tunaona tena kafanya yale yale, sasa tusemeje?! Uhakika upi ungekufaa wewe?!