Membe: Msiponichagua mimi mchagueni Pinda

Wa kusoma

JF-Expert Member
Jul 30, 2011
3,454
2,975
Membe ameyasema hayo akiwa Mpanda mkoani Katavi, kwamba mpaka sasa roho yake inadunda mapigo mawili Pinda/membe ana uhakika akishinda yeye ameshinda Pinda akishinda Pinda ameshinda yeye

===================================

Mjini Sumbawanga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe amesema kwamba katika kinyang'anyiro cha urais ndani ya CCM mtu anayemnyima usingizi ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda. Membe alisema kuwa iwapo Pinda asingechukua fomu ya urais, angekuwa anafurahia ushindi tu.

Akizungumza kwenye ukumbi wa CCM Sabasaba, Membe alisema kuwa Waziri Pinda ni mtu mchapakazi, asiye mbinafsi, mwadilifu, mvumilivu sana mwenye hekima na busara ya hali juu, mwanasheria aliyebobea na ndiye mwalimu wake ambaye alimfundisha kazi.

"Wengine wote hawanitishi nitawagonga, nitawagonga, lakini nikifika kwa Pinda itabidi nipumue kwanza. Kwa hiyo mimi na Pinda ni pacha nikishindwa mimi nitamuunga mkono," alisema Membe ambaye pia aliwahi kusema atamuunga mkono Profesa Mark Mwandosya.

Awali, katibu uenezi wa chama hicho mkoani hapa, Clement Bakali alisema Membe amepata wadhamini 855.

Chanzo: Mwananchi
 
Ahhh wananungana baada ya kuona nguvu manywele ahhh ahh ukijiandaa kushindwa una shindwa ukijiandaa kushinda utashinda
 
Mikauli yake hii Inaonyesha Hasivyo Makini; Hana confidence, Anajua Hawazi Kuwa rais Wa Tanzania; Mara akikatwa atamuunga mkono Prof Mwandosya mara ni yeye au Pinda. Kiongozi Mwenye Determination hawezi Kukata Tamaa na Kuanza Kukosa Matumaini Kama Huyu Mweshiimiwa.

Safari Hii Nadhani Ndani ya CCM Kuna Sintofahamu ya Kutisha na si Lolote wala Chochote, Mambo yote UKAWA Kwa Kwenda Mbele.
 
Membe ameyasema hayo akiwa Mpanda mkoani Katavi, kwamba mpaka sasa roho yake inadunda mapigo mawili Pinda/membe ana uhakika akishinda yeye ameshinda Pinda akishinda Pinda ameshinda yeye
Akienda arusha atasema ka si yeye wchague Lwasa, akienda singida kama si yeye wamchague mwigulu!! Huyu kweli hajitambui na alisema kama si yeye basi wamchague Mwandosya!
 
huyu Membe si amewahi sema kama si yeye atamuunga mkono MWANDOSYA,kweli membe hafai hana msimamo akiwa rais atatuuza km njugu.
 
Nimemsikia kupitia ITV nikabaki namshangaa wakati aliwa kujinadi kuwa yeye ndio bora kuliko watia nia wengine.
 
Washapangana na anajua anakatwa na hivyo akaona ajiunge kwa pinda labda atapewa ubalozi
 
Huyu ni wa ajabu. Alipokuwa Mbeya alitoa kauli kama hii kwa Prof Mwandosya, akaenda Mara akatoa kauli kama hii kwa Makongoro! I think he is not serious
 
Mkuu anawapenda watu wa aina hiyo kufanya kazi chini yake maana hawana msimamo wanakubali tuu. Kwahiyo hata akiondoka atakuwa anaendelea kutawala nchi nyuma ya pazia. Watanzania tuwe macho sana, hki siyo kipindi cha pata potea, hiyo wabaki nayo wenyewe.
 
Back
Top Bottom