Media kuikosoa Serikali: Je, Tanzania tuna Strong Media au Strong Journalists wenye Uwezo huo?

Sasa wandishi wenyewe kama wewe hapo Paskale ulikuwa unashinda humu unamsafisha bwana Bashite kwa masilahi yako ndo uweze kuikosea serikali?
 
Mkuu Mkaruka, hii ni kweli kwenye private media lakini kuna public media paid by taxpayers money, inatakiwa to save the public and not the government.
Kwenye sheria yetu ya habari, sheria imetambua makundi mawili tuu, public media na private media. Kwenye Public Media, wameweka Government Media only wakimaanisha hata TBC ni chombo cha habari cha serikali!. Kiukweli TBC ni chombo cha habari cha umma, public media, kinawajibika kwa umma wa Watanzania na sio kwa serikali, vyombo vya serikali ni Habari Maelezo, Daily News na Government Gazette (GN).

TBC ndio inayotakiwa kuwa strong media kuihudumia jamii na kuikosoa serikali. Lakini kwa TBC yetu hii hili linawezekana? . Niliamini Dr.Ayoub Rioba amepelekwa pale kwa sababu alikuwa very critical lakini... labda tumpe muda zaidi.
Paskali.
Hicho unachokitaka ni Fantasy tu, hakuna popote duniani MEDIA ya SERIKALI ( Wewe unaita ya UMMA ) ikakosoa serikali.No NETRAL Media anywher
 
Nashukuru sana kwa kunipa heshima ya kunijibu. Kwanza nashukuru umetupa track yako ya u media, ambayo imenisaidia ku confirm kuwa ni kweli wewe si muandishi wa habari. Kuwa host wa kipindi kinacholeta magwiji sio kuwa muandishi wa habari. Ni sawasawa na kumuita Zembwela Muandishi wa habari, kama tulivyomuuliza makonda, tuletee track yako ya uandishi wa habari, investigative na public interest, Maxence hajawahi kujiita muandishi wa habari, pamoja na kuwa na kuwa na uwezo mkubwa sana wa kuwakutanisha watu kuzungumzia habari. Zile habari sio zake, ni sawa na wewe, kiti moto hakikuwa investigative work yako, wale madiwani wa ccm wanaotoka kibaha na wazalendo wengine walikua wanatulietea scops tu, sio wewe. Pili nashukuru pia kuwa miaka yako 27 ya kukaa studio, not even press room, haitoshi kukuita muandishi wa habari. Ni sawa na kutuambia kuwa kwa kuwa unakaa karibu na mahakama basi wewe ni mwanasheria. Ndio maana karani wa mahakama aliyekaa mahakamani miaka 30 haitwi mwanasheria. Swala la Makonda haliweze kuwa your piece of literature, ni swala linalohusu integrity ya Taifa la Tanzania na kitu kinachoitwa Good Governance, sio mambo ya opinion zako, ulitakiwa ujue hata hilo kabla hujaingiza ujikombi wako, kwenye mambo serious. Once again, usipende kujikwaza sana na kujifanya mjuaji, neno linasema, ajikwezaye atashushwa, kwanini kama huna point lazima tu uongee, jitambue kuwa wewe sio opinion leader kwenye sekta ya media, kwanza sidhani hata kama unazo qualification zaidi tu ya ujanja ujana fulani, kama we bingwa weka vyeti vyako hapa tuone kama walau diploma ya uandishi, sana sana pengine una certificate ya Royal bahati kama una ya TSJ. (over) nakusubiri!
Mkuu Nndondo asante, kwa vile lengo la hili bandiko sio majisifu ya Pasco Mayalla ni mwandishi au laa na aliwahi kufanya nini kwenye newsroom hadi kufikia kuhoji integrity yangu kama nina vyeti au laa. Kwa vile hii sio subject matter ya uzi huu, for the sake of uzi huu, naomba kukubalia kuwa na mimi ni mtangazaji kama Zembwela, si mwandishi na elimu yangu ni kama ya Bashite hivyo sina vyeti vyovyote vya kuwasilisha jf . Ya Makonda you've missed the point. Tuendelee na mada iliyopo mezani.

Paskali
 
Wanabodi,

Declaration of Interest: Mwanzisha Mada ni Mwandishi wa Habari Mstaafu ambaye amehudumu kwenye tasnia hii kwa miaka 27, hivi sasa ni mstaafu akiendelea kuhudumu kama Mwandishi/Mtangazaji was Kujitemea kupitia kampuni ya PPR.

Serikali zote duniani huendeshwa na mihimili 3 ambayo ni rasmi, Serikali, Bunge na Mahakama, ila kuna mihimili wa nne ambao ni mihimili usio rasmi, huu ni mhimili wa Media, The Fourth Protocol.

Waziri wa Habari Mhe. Nape Mnauye ametoa ruhusa kwa media kuikosoa Serikali. Ili hili liweze kufanyika kwa manufaa na kuleta tija, lazima kwanza tuwe na Independent Stong Media na tuwe na waandishi mahiri ambao ni ma Iconic figures akiandika "This is wrong", Serikali itasikiliza.

Swali ni jee Tanzania tunazo hizo strong media?, jee tunao hao strong journalists wenye uwezo wa kuikosoa Serikali na Serikali ikawasikiliza? .

Kama tunazo ni zipi? . Kama hatuna kwa nini hatuna strong media?. Na jee hao waandishi strong journalists tunao?, ni kina nani wakiandika au wakisema Serikali itasikia, itabadilika?.

Mifano ya Strong Media.
US wana strong media. Wana vyama viwili vikuu vya siasa The Democrats na The Republican. Wana magazeti makuu mawili, The New York Times na The Washington Post. Pia wana TV mbili kubwa CBS na ABC.

UK pia wana Strong Media. Wana vyama vikuu viwili vya siasa, Labour na Conservative. Wana gazeti moja kuu, The Daily Telegraph. Wana radio moja kuu na TV moja kuu, BBC.

Sisi na huu utitiri wa vyama, utitiri wa magazeti, utitiri wa TV stations na utitiri wa magazeti, jee tuna any strong media ndani ya utitiri huu?.

Paskali
Ukweli ni kwamba hatuna strong Media bali tuna some few strong personalities kwenye media mmojawapo ni ndugu fulani ambaye anamiliki magazeti lakini yeye anawaandika Marais vibaya au kuwakosoa pale tu anapoona amepuuzwa mfano aliandika sana tena kishabiki kumshambulia Ben simply kwa sababu alitegemea kuchaguliwa position fulani lakini hakupewa alafu akazushiwa kwamba sio raia wa Tz,. Alianza vizuri kumuandika Jk lakini baadae akaona kimya hakuchaguliwa basi JK alipomaliza vipindi vyake aliipata ya jiwe akaandikwa vibaya. JPM naye alianza kuandikwa vizuri na magazeti ya huyu ndugu lakini alipoona hateuliwi hata ubunge sasa ameanza kumsakama JPM vibaya.
 
Wanabodi,

Declaration of Interest: Mwanzisha Mada ni Mwandishi wa Habari Mstaafu ambaye amehudumu kwenye tasnia hii kwa miaka 27, hivi sasa ni mstaafu akiendelea kuhudumu kama Mwandishi/Mtangazaji was Kujitemea kupitia kampuni ya PPR.

Serikali zote duniani huendeshwa na mihimili 3 ambayo ni rasmi, Serikali, Bunge na Mahakama, ila kuna mihimili wa nne ambao ni mihimili usio rasmi, huu ni mhimili wa Media, The Fourth Protocol.

Waziri wa Habari Mhe. Nape Mnauye ametoa ruhusa kwa media kuikosoa Serikali. Ili hili liweze kufanyika kwa manufaa na kuleta tija, lazima kwanza tuwe na Independent Stong Media na tuwe na waandishi mahiri ambao ni ma Iconic figures akiandika "This is wrong", Serikali itasikiliza.

Swali ni jee Tanzania tunazo hizo strong media?, jee tunao hao strong journalists wenye uwezo wa kuikosoa Serikali na Serikali ikawasikiliza? .

Kama tunazo ni zipi? . Kama hatuna kwa nini hatuna strong media?. Na jee hao waandishi strong journalists tunao?, ni kina nani wakiandika au wakisema Serikali itasikia, itabadilika?.

Mifano ya Strong Media.
US wana strong media. Wana vyama viwili vikuu vya siasa The Democrats na The Republican. Wana magazeti makuu mawili, The New York Times na The Washington Post. Pia wana TV mbili kubwa CBS na ABC.

UK pia wana Strong Media. Wana vyama vikuu viwili vya siasa, Labour na Conservative. Wana gazeti moja kuu, The Daily Telegraph. Wana radio moja kuu na TV moja kuu, BBC.

Sisi na huu utitiri wa vyama, utitiri wa magazeti, utitiri wa TV stations na utitiri wa magazeti, jee tuna any strong media ndani ya utitiri huu?.

Paskali
Kama waandishi wenyewe ndio Nyinyi kutwaa kucha kumsifia na kumuimbia Mapambio ya Sifa na utukufu Daudi Bashite mtaweza kuhoji kitu kweli ?
 
Hicho unachokitaka ni Fantasy tu, hakuna popote duniani MEDIA ya SERIKALI ( Wewe unaita ya UMMA ) ikakosoa serikali.No NETRAL Media anywher
Mkuu Mkaruka TBC ni public media not government media ndio maana ina bodi yake independently hivyo inaweza kuikosoa serikali kama ilivyo BBC.

Sijazungumzia neutrality, nimesema public media inatanguliza mbele maslahi ya umma, kazi ya serikali ni kuutumikia umma, hivyo serikali ikikosea TBC ilipaswa kuwa na uwezo wa kuikosoa.
Paskali
 
Dictatorial govt kama Zimbabwe huwa HAZIKUBALI KUKOSOLEWA KAMWE...
•KUKOSOA HUWA NI JINAI KWA KWA MABAVU YA WATAWALA...
Naunga mkono hoja ila hizo serikali za kidomokrsia zina udikiteta wake. Kitu ambacho ni kweli kuhusu serikali zote za kidikiteta zina kiuka haki za binaadamu na ku suppress the media, hakuna freedom of expression. Tanzania bado hatujafika huko na hata Zimbabwe sio udikiteta bali ni African Democracy. Kama hoja ni ile ya Mugabe kung'ang'ania madaraka, tumependekeza Magufuli apewe muda zaidi
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?
Paskali
 
Hatuna. Hatuna vyote. Hatuna strong wala independent media houses wala journalists. Hakuna mwandishi ambaye unaweza ukamuamini 100% leo hii. Hakuna makala utasoma ikawa inajitosheleza bila kusoma "upande wa pili" kutoka katika "source" zao.
Waandishi wa leo wako biased na attached waziwazi kwa upande fulani. Imefikia hata waandishi wa michezo nao biased; aaaaggh.
 
Mkuu Nndondo asante, kwa vile lengo la hili bandiko sio majisifu ya Pasco Mayalla ni mwandishi au laa na aliwahi kufanya nini kwenye newsroom hadi kufikia kuhoji integrity yangu kama nina vyeti au laa. Kwa vile hii sio subject matter ya uzi huu, for the sake of uzi huu, naomba kukubalia kuwa na mimi ni mtangazaji kama Zembwela, si mwandishi na elimu yangu ni kama ya Bashite hivyo sina vyeti vyovyote vya kuwasilisha jf . Ya Makonda you've missed the point. Tuendelee na mada iliyopo mezani.

Paskali

Hahahaaa, huyu ndiye Pasco. Binafsi najifunza vingi kupitia wewe.
 
Pascal Mayalla hii changamoto iko kwako kwa kiasi kikubwa? Umesema umestaafu na sasa ni mwandishi huru sasa sijajua hii imekaaje?

Lakini nikuulize ushawahi kukaa na kujiuliza umetenda nini kwenye tasnia ya habari (uandishi au kuripoti) ambacho umefanya kitaweka historia na kuwa chachu kwa waandishi wengine wachanga?

Na kama hujafanya na sasa ni mwandishi huru ni nini unatarajia kufanya cha kuweka historia ambayo itakwenda kwenye vitabu vya kumbukumbu kama waandishi wengine wa habari kama Mohamed Ali au Komla Afeke Dumor.

Ulikuwepo pale na inawezekana kabisa ni kanuni, sheria na misingi ya kampuni husika zilikubana uliyvokuwa unafanya sasa kwanini wewe usijivike mzigo huo wa kuikosoa serikali pale inapokosea kwa kutumia weledi na mwanya huu uliokuwa nao sasa?

Don't wait for another man to bring change be the catalyst for change Paskali.
Don't be the follower Paskali, be the leader and make a mark in the history books.
Don't follow the path Paskali, creat the path that may leaves the mark for others to follow.
Don't just be JF's keyboard hero Paskali go out there and make the change and I know its not easy Paskali but its possible
You got the name and reputation be the Key Person of Influence (KPI) don't allow yourself to die and merely leave the name without a trail.
Time is now Paskali go and tell the Government and the world stories of Tanzania as it really is
 
Nape huyo huyo alikomalia sheria mbovu ya huduma za habari ipitishwe, halafu leo anaibukia jukwaani akisema tuikosoe serikali! Huu ni mtego.
Wanahabari walipaswa kupambana sheria ile isipite, maana ni hatari mno kuikosoa serikali kwa sheria ile, narudia tena, ni hatari sana.
Sheria ile sio mbaya kivile, japo is not the best, something is better than nothing. Tusilaumu tuu kila kitu, Sheria ya Habari imetanguliwa na jambo moja zuri sana ambalo halikuwahi kuwepo Tanzania tangu tupate uhuru, hii ni ile Sheria ya Haki ya kupata Habari. Tangu tumepata uhuru, kupata habari haikuwa haki bali just favours na watoa habari walitoa pale tuu walipojisikia kutoa habari, lakini sasa kwa mara ya kwanza, kupata habari ni haki yako na mtoa habari analazimishwa lazima atoe habari. Hili ni jambo zuri sana kwa tasnia ya habari.

Sheria hii mpya ya habari ni afadhali mara mia kuliko uliyokuwepo hivyo if you can't get what you want, just take what you get. Tushukuru kwa kidogo ili tuweze kupatiwa kikubwa. Wito kwa wanahabari: If you can't get what you want, just take what you get!
Paskali
 
Kama waandishi wenyewe ndio Nyinyi kutwaa kucha kumsifia na kumuimbia Mapambio ya Sifa na utukufu Daudi Bashite mtaweza kuhoji kitu kweli ?

Bramo acha kumtukana Paskali inahitaji utulie na akili ya ndani kujua huwa anaandika nini?

Sarcasm, Irony and Journalism

Kafanyie utafiti hayo maneno matatu ndiyo utamwelewa Paskali
 
Na katika wanaongoza kwa njaa huyu jamaa katia fora. Yuko all over the place kutafuta uDC kwa nguvu zote.

Pamoja na mapungufu mengine yaliyopo, njanjaa zenu ni tatizo kubwa sana.

Waandishi na wamiliki wa vyombo vya habari mmeshindwa kutambua kabisa watawala hawana urafiki wa kudumu na media bali wanachoangalia ni maslahi yao kupitia media namna gani yanalindwa.

Hata hivyo,kuna waandishi wachache wanaostahili pongezi kwa kusimamia maslahi ya Taifa.
 
masoudkipanya-20170311-0001.jpg
 
Pascal,

Ni uongo kwa Mwandishi wa Habari kama wewe kuandika hapa kuwa kuna magazeti mawili muhimu huko Uiingereza na Marekani.

Ukweli ni kuwa kuna magazeti zaidi ya mia Marekani peke yake na magazeti si chini ya 10 huko Uiingereza.

Mtu yoyote anaweza ku google " how many daily newspapers are there in America/ USA?" Na akapata majibu haraka sana kupinga kauli yako.

Mimi sihitaji ku google kwa sababu ninayasoma kama matatu kwa kila nchi kila siku.

Ninasoma The Independent, The Times na The Guardian, zote za Uiingereza.

Ninasoma The Washington Post, The New York Times na Los Angeles Times, zote za Marekani.

Sasa sijui umepata wapi hizo habari kwamba wana magazeti mawili muhimu tu wakati kila jimbo wanachapisha magazeti!

Pili, huhitaji ruhusa ya Waziri, kuuliza maswali magumu. Hii ni kazi ya Mwandishi wa Habari.

Kukosoa serikali ni wajibu na haki ya kila mwananchi katika nchi yao.

Hii haki inaheshimika katika Umoja wa Mataifa na inajulikana kama "Freedom of Speech".

Ni nchi za kidikteta peke yake ndizo zinazotaka waandishi wa habari waombe rukhsa na kupewa ruhusa na Waziri kukosoa serikali.

Mpaka sasa, siamini kuwa Tanzania tuna uhuru wa kuandika chochote kukosoa serikali. Huhitaji Ph.D kuona kuwa hatuna haki hiyo.

Na hamna kitu kama "fourth pillar" katika katiba yetu wala za nchi zilizo na demokrasia kamili.

Tofautisha "checks and balances" na uhuru wa kufikiri na kuandika.

Hivo ni vitu tofauti kabisa.

Don't mix oil and water, please!
 
Pascal Mayalla hii changamoto iko kwako kwa kiasi kikubwa? Umesema umestaafu na sasa ni mwandishi huru sasa sijajua hii imekaaje?

Lakini nikuulize ushawahi kukaa na kujiuliza umetenda nini kwenye tasnia ya habari (uandishi au kuripoti) ambacho umefanya kitaweka historia na kuwa chachu kwa waandishi wengine wachanga?

Na kama hujafanya na sasa ni mwandishi huru ni nini unatarajia kufanya cha kuweka historia ambayo itakwenda kwenye vitabu vya kumbukumbu kama waandishi wengine wa habari kama Mohamed Ali au Komla Afeke Dumor.

Ulikuwepo pale na inawezekana kabisa ni kanuni, sheria na misingi ya kampuni husika zilikubana uliyvokuwa unafanya sasa kwanini wewe usijivike mzigo huo wa kuikosoa serikali pale inapokosea kwa kutumia weledi na mwanya huu uliokuwa nao sasa?

Don't wait for another man to bring change be the catalyst for change Paskali.
Don't be the follower Paskali, be the leader and make a mark in the history books.
Don't follow the path Paskali, creat the path that may leaves the mark for others to follow.
Don't just be JF's keyboard hero Paskali go out there and make the change and I know its not easy Paskali but its possible
You got the name and reputation be the Key Person of Influence (KPI) don't allow yourself to die and merely leave the name without a trail.
Time is now Paskali go and tell the Government and the world stories of Tanzania as it really is
Mkuu Nimeguswa sana bandiko lako hili, this is very inspirational words. Mwanzo nilipanga to work out of media 2015 baada ya uchaguzi ikatokea mayai yangu yote nikayaweka kwenye kukapu kimoja, hivyo yakapasuka yote! .

Sasa nitawalk out 2020, hivyo in between najiandaa kuondoka kwa kuacha kitu. Kuna wakati nilijaribu kupitia JF, lakini nilipigwa sana madongo nika abandon.

Vipindi Maalum vya JF kwenye TV: Naomba Maoni Yako!

Kwa sasa nazifanyia kazi some of these 10 TV Programs ideas kabla sijaagana rasmi na media.

rams.
3.1 Prog. 1-KWA MASLAHI YA TAIFA- TV Political Hard Talk Show- 30min
3.2 Prog. 2-SIRI YA MAFANIKIO – Profile Program-30 min
3.3 Prog. 3- TANZANIA NA MAENDELEO- Descriptive Program 30 min
3.4 Prog. 4- KUELEKEA TANZANIA YA VIWANDA- Feature Program
3.5 Prog. 5- KIPINDI MAALUM- Documentary in any specific Topic-30 min
3.6 Prog. 6- PPR NEWS EXTRA- 5 Minutes News extra "Habari Zaidi ya Habari na PPR.
3.7 Prog.7- IJUE KATIBA, SHERIA NA HAKI ZAKO-30 Minutes kuhusu Katiba, sheria na haki.
3.8 Prog.8- ITS ALL ABOUT POWERS THAT MATTERS -30 Minutes TV Program about power be it Supernatural, Devine, Psychic, Meditation,Mind Over Matter etc.
3.9 Prog. 9- TULIPOTOKA, TULIPO NA TUNAPOKWENDWA -30 Minutes Program about Trends za issues za Kisiasa, Kiuchumi na Kijamii.
3.10 Prog.10- HIFADHI YA JAMII NI HAKI YAKO- 30 Minutes Program kuhusu hifadhi ya Jamii ni haki kwa wote sio privilege to some or favors.

Paskali
 
Umesema sahihi sana.Naomba nichangie kwenye ili la utitiri wa vyombo vya habari.

Ingawa uwepo wa vyombo vingi vya habari unatoa fursa za ajira kwa wananchi wenzetu.Lakini ni wakati wa kuangalia sheria ya uanzishwaji wa vyombo hivi.Sasa hivi imekua kama "fasheni" kila mkoa kuwa na either kituo cha radio/tv. Lakini hazina impact yoyote katika kukuza maendeleo/maadili na uchumi wa sehemu husika!!

Hii inatoka either na ubora na umahiri wa wanahabari hawa.
 
Back
Top Bottom