Mechi kati ya timu ya mkoa wa Mbeya na Mkoa wa Kagera...!!

Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,983
12,702
Fikiria wewe ni mtangazaji wa mpira. Mechi inayochezwa ni kati ya timu ya mkoa wa Mbeya na timu ya mkoa wa Kagera....hivi ndivyo utakavyoutangaza mpira....

Anakwenda pale Andendenisye Mwakisomola...anapiga kwake Nsajigwa Malafyale...naye kwake Asangalwisye Mwasabwite....anapiga pasi kwake Anongisye Mwakatebela...anatokea pale Salvatory Rugemalira ananyang'anya mpira...anatoa pasi kwa Bagambilaine Ntuyabaliwe....anacheza vizuri kabisa kwake Kokushobura Rugaimukamu...naye anampa pale Rwekaza Rweyemamu...anacheza vizuri...asalalee namna gani pale ananyang'anywa na Anyosisye Mwakifwamba...anagonga mbili tatu pale anapiga pasi ndeeefu kabisa inakuwa njiwa....

Mpira ni wa kurushwa sasa kuelekea lango la timu ya mkoa wa Mbeya...anakwenda kurusha nani pale...jezi nambari saba pale...haya sasa Rweyongeza Rutashubanyuma anarusha mpira kwake Lutatinisibwa Mutahyabarwa...ancheza daglizi pale...kwake nani sasa...kwake Nyamuhanga Lutabasibwa...anatokea pale Alinanuswe Mwakatapanya anachukua mpira...anatokea Kamugoza Rwegoshora anapigwa tobo pale na Mwakatapanya...anacheza vizuri pale kwake Andendekisye Mwamasangula...anaruka kichwa..hatari pale...gooooooooooooo......bao safi kabisa lile....golikipa Christosom Rwehumbiza alikwenda kushoto....Andendekisye Mwamasangula akapiga kichwa maridadi kabisa kulia...beki wa kati Mutakyawa Mukyanuzi akabaki kushangaa...

Mbeya moja na Kagera hawajapata kitu......

Mpira ukiisha lazima uwe na lundo la diclofenac walahi vile!
 
Hahahahahaha mtangazaji akitoka hapo moja kwa moja kwenye chumba cha upasuaji.
 
E bwanaeee,katavi una kipaji,nina mpango wa kuanzia Fm radio,sitakusahau mkuu.
 
mghoooooonileeeeeeeeee,hobwike fijo ni story jha katavi....kumyetu kununu fijo une nguganile.
 
Ta kamugisha is very fantastic natela three postion for one time! actually he is very ..,.fantastic
 
il iyo mech itangazwe lazima kuwe na watangazaj wawil mnyakyusa na mhaya.kila m2 atangaze upande wa timu yake.
 
Back
Top Bottom