Mechi kali

mpigilie

JF-Expert Member
Sep 14, 2011
310
136
Haya ndugu watazamaji wa kituo chetu bora cha habari,ile mechi kali kati ya serikali na madaktari karibia kipindi cha pili kinaanza. HALF TIME ndo inaisha leo,timu zote zinajitaarisha kutoka kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.
Naona REFA(wananchi) anakagua kiwanja,kwenye goli la serikali refa anakuta kuna vitu vimefukiwa(manesi,wauguzi,vitisho,fitna, dharau.......)
Hii ni aibu kwa timu kubwa kama serikali kutumia mbinu chafu za kushinda mechi dhidi ya timu iliyopanda daraja msimu huu,ikichukua nafasi ya timu ya WALIMU iliyoonyesha kiwango kibovu msimu uliopita na kusababisha ishike daraja.

Mechi hii lazima mshindi apatikane safari hii,hata kwa ushindi wa penati..
 
kuna tetesi kwamba yule waziri mkubwa kuliko wote,ambaye takwimu zinaonyesha kuwa anaongoza kulia kuliko mawaziri wote,jana aliwaita timu pinzani ili wapange matokeo ya mechi,lakini wapinzani wakagoma kupanga matokeo
 
Mfungaj mahiri wa serikali atafanya nn kipindi cha pili?kipindi cha 1 alijiangusha wakapewa penalt wakafunga....
 
Anachukua dokta wa meno anampasia dokta wa ulimi, ulimi,ulimi!!! Aaaah ulimi anapoteza pale kwel ulimi uliponza kichwa. Serikali kabaki na goli anapiga pale..... Goooooo! Anapoteza pale mpira umepaa juu. Mech imehairishwa mpaka usiku wa manane.
 
anapiga pale mshambuliaji hatari sana huyu kwa jina la ulimboka! Nini nini pale, goli kiki
 
dk 90 zmeisha ngoma ni droo hvyo zimeongezwa dakika 30 hvyo ngoja 2one 120 nani mshindi,kuna kila dalili madktar kushinda naona timu ya serikali pumzi imekata wanakunywa maji ovyo...
 
hii mechi kweli kali,dakika 90 bado mshindi hajajulikana.wameongezewa dakika 30,ila kwa mbali naona hawa wenye siri kali kama wameanza kuishiwa pumzi. ili tusubili mpaka mwisho wa mchezo manake ni ngumu kutabili mshindi.madaktari wanapiga pasi nzuri sana,ila serikali wanacheza rafu kupita kiasi na refa anaonekana kufumbia macho rafu za serikali
 
Inaelekea timu ya serikali inategemea huruma ya mashabiki ili kuibuka na ushindi
 
Haya ndugu watazamaji wa kituo chetu bora cha habari,ile mechi kali kati ya serikali na madaktari karibia kipindi cha pili kinaanza. HALF TIME ndo inaisha leo,timu zote zinajitaarisha kutoka kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.
Naona REFA(wananchi) anakagua kiwanja,kwenye goli la serikali refa anakuta kuna vitu vimefukiwa(manesi,wauguzi,vitisho,fitna, dharau.......)
Hii ni aibu kwa timu kubwa kama serikali kutumia mbinu chafu za kushinda mechi dhidi ya timu iliyopanda daraja msimu huu,ikichukua nafasi ya timu ya WALIMU iliyoonyesha kiwango kibovu msimu uliopita na kusababisha ishike daraja.

Mechi hii lazima mshindi apatikane safari hii,hata kwa ushindi wa penati..

Baada ya serikali kufungwa 1-0 Abromovich ameamua kumfukuza kocha na kumweka kocha msaidizi
 
ila kocha wa timu ya serikali amesafiri yupo msaidizi lakini anatumia nguvu kucheza badala ya akili
 
Naona bench la ufundi la timu ya serikali wanaanzsha zogo hapa,wanasema kuna wachezaji wa tim ya madaktar ni mamruki hawajasajiliwa wanasadikika kutoka CDM hvyo wanaomba mechi kuhairishwa.
 
Back
Top Bottom