Mechi inaendelea kati ya CCM na CDM

Gurtu

JF-Expert Member
May 15, 2010
1,247
342
Mpambano bado unaendelea kati ya Timu ya CCM na CDM. Mpaka sasa CCM wameshabadilisha wachezaji (CC) lakini bado wanazidiwa kimchezo.

Mechi ya kwanza CCM wamashapoteza baada ya kuleta Muswada wa Mapitio ya katiba wakati watu wanataka katiba mpya. Hata muswada huo pamoja na kwamba unazungumzia kitu kingine kabisa, tofauti na kile ambacho wanataka wananchi, ulikuwa na kasoro nyingi. Hapo CCm imerudi nyumbani ikiwa imepigwa bao moja kwa zero.

CCM wameamua kucheza kwa mtindo wa kujivua gamba. Kujivua gamba kunaweza kusisaidie CCM kwani mpaka sasa wanacheza mchezo wa kujilinda na siyo kushambulia. Jana wakati timu CCM inajilinda Dar wenzao CDM wanashambulia Tabora. Kwa ushauri wangu CCM waende wakalinde goli Tabora kwani mashambulizi ya CDM kule Tabora ni makali.

Tunaendelea kutazama mchezo unavyoenda. Tutaendelea kupeana matokeo.
 
Siku hizi wanaogopa hata kwenda Jangwani wanapwaya wanajibana bana kwenye vibaraza vya Bharesa manzese wataweza huko mikoani.
 
Huwa wanalinda goli kama unabeki. CCM wote ni washambuliaji sasa hivi si UVCCM, Secreatariat, n.k
 
hahaaaaa beki za ccm hazikabi..watakuwa vifua vimejaa moshi wa sigara wanashindwa kurudi wakipanda mbele..hahaaaa
 
hawawezi kukimbia na mpira manake matumbo yao ni makubwa sana yamejaa rushwa na ufisadi kwa vyovyote mechi hii watafungwa tu
 
Washambuliaji wote wa ccm wanajikanya wao kwa wao,na kocha wao anabaki kushangaa eti hajui lolote,sijui anawafundishaje wachezaji wake kama hajui,wachezaji vilaza kocha kilaza sijui inakuwaje hopo.
 
wachezaji hawafundishiki hawa
 
deadly striker dr. Peter slaa, huyu chance moja bao moja, mbowe midfield maestro, mnyika, aka jack wilshire, wonder kid, lema aka super mario baloteli, zitto...?
 
Back
Top Bottom