TANZIA Mchungaji Mang'welela wa kanisa la Sabato Kahama afariki dunia

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,872
35,875
Inafahamishwa kutokea Kahama kuwa, mchungaji John Mang'welela wa kanisa la Sabato huko amefariki dunia leo.

IMG_20210129_150704_893.jpg


Taarifa zaidi ni hii hapa kama ilivyotolewa:

----------
"Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Nyanza Gold Belt Field Mch. Enoch Sando.

Tunasikitika kutangaza kifo cha mchungaji mstaafu Pr. John Mang'welela kilichotokea leo katika hospitali ya wilaya hapa Kahama. Ninaomba washiriki tuiombee sana familia hii katika kipindi hiki kigumu na taratibu zingine tutawajulisha.

Pr Joshua Mbwambo
Katibu wa Wachungaji.
Nyanza Gold Belt Field"
-----------

Poleni wafiwa na wote mlioguswa na msiba huu.

Bwana alitoa na bwana ametwaa.

Jina lake lihimidiwe.
 
"Wapo walioenda huko nje kuchanjwa wametuletea corona za ajabu-ajabu". Jpm

Vipi wale watalii waliokuwa wanakuja wakijinasibu kuwa Tanzania ndiko ambako ni pekee wanakokwenda na hawasumbuliwi kwa lolote na mambo ya hii ngwengwe? Eti kuwa huku ndiko iliko "tourists destination" na hivyo tutavuna sana mapene, nasi tukachekelea?

Kwa nini wasiwe wao ndiyo walio tuletea hii corona ya ajabu ajabu mheshimiwa jpm?

Kweli tamaa mbele mauti nyuma.
 
Me naona wazike tu kimya kimya.. sasa mtu anakufa tu bila historia ya ugonjwa?
Na historia yake wala haisemwi yani kama ville tunaish kijiji kimoja

Kuna mwamba hapendezwi na hizo historia. Hata hapa wewe nakunong'oneza tu.

Hata akipiga marufuku matangazo ya vifo wala haitakuwa ajabu.
 
Huyu muda wake wakutumikia wanadamu umeisha na hapo ana 80 yrs kuendelea.
Apumzike kwa amani.

Inafikirisha. Palikuwa na uzi humu:


Wazee hawa waliihitaji sana chanjo hii.

Wewe uko kundi gani jombi? Au ni lile kabila letu pendwa la kanda maalum ambako hata wazazi wao wenyewe huwaona ni mzigo wanapozeeka, wakawa brand kuwa ni wachawi ili kuhalalisha kuwafuta kabisa kutoka kwenye uso wa dunia?

Disgusting.
 
Kwa nini hawasemi chanzo?R.I.P Ndemi.

Mkuu hata wakisema watasikia? Tukiwa hai tuliwaandikia haya:


Sembuse katika kifo?

Wana jambo lao kule nanihii. Chanjo si kipaumbele.
 
Me naona wazike tu kimya kimya.. sasa mtu anakufa tu bila historia ya ugonjwa?
Na historia yake wala haisemwi yani kama ville tunaishi kijiji kimoja

Ni kweli kuwa pana watu wangependa sana wafu wazikwe kimya kimya.

Kwanza wanaleta taharuki.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Vipi wale watalii waliokuwa wanakuja wakijinasibu kuwa Tanzania ndiko ambako ni pekee wanakokwenda na hawasumbuliwi kwa lolote na mambo ya hii ngwengwe? Eti kuwa huku ndiko iliko "tourists destination" na hivyo tutavuna sana mapema, nasi tukachekelea?

Kwa nini wasiwe wao ndiyo walio tuletea hii corona ya ajabu ajabu mheshimiwa jpm?

Kweli tamaa mbele mauti nyuma.
Mitano tena, Ni Yeye...
 
Back
Top Bottom