Mchepuko anachanganya mapenzi na pesa, nilichomfanyia nadhani kapata funzo

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
40,495
99,292
Habari wakuu,
Kuna siku Moja usiku nikiwa kwa mamaJ akanambia mchana wa Jana Yake, binti yake anayeuza dukani kwake kaibiwa Simu yake (Samsung smart phone) kwenye mazingira ya kutatanisha sana.

Anasema Hakukuwa na wateja alienda msalani chap nyuma ya fremu zao akaacha Simu chaji, aliporudi hakuikuta na kawauliza majirani wanasema hawakuona mtu akiingia ndani. Na Simu ilivyopigwa ikawa haipatikani.

Basi nikamshauri Kama Simu imepotea Ni Vema akatoe taarifa polisi, Unaweza kuzembea Simu yako imeibiwa kisha ikatumika kwenye uhalifu halafu ukaunganishwa kwny tukio la uhalifu. Akasema sawa, ataomba kesho nimpitie yeye na binti yake nnavyoenda kazini ili niwasindikize wakatoe taarifa ya kupokelewa simu polisi. Nikasema sawa.

Kweli kesho Yake asubuhi nmewapitia yeye, pamoja na binti wa dukani kwake dukani wote tumeongoza tumeelekea kituo cha polisi.

Baada ya kufika polisi, nikabaki kwenye gar na kumwambia yeye na binti wake waingie wakatoe taarifa watanikuta kwny gar nje nawasubiri tuondoke. Wakasema sawa. Sasa Baada ya kuona wamekaa ndan mda mrefu Sana hawatokei na mamaJ simu zangu hapokei, Ikabidi kumfata uko uko ndani ili afanye haraka ananipotezea Muda wangu nna Ratiba zangu nyingine. Nikamkuta ndo Yuko anatoa maelezo kwa afande.

Kuangalia Kumbe afande mwnyw tunafahamiana, kuna mahali flan tuliwahi kutana. Basi salamu za hapa na pale na afande Kisha Afande akanambia niketi amalizie kuandika maelezo Yao ili kuifungua kesi ya kuibiwa wa Simu, ili Kama uwezekano upo, simu yao ianze kufuatiliwa.

Basi nikaona ni wazo zuri. Afande akasisitiza kwamba mwizi wa Simu Hata akipatikana, Kama hakukuwahi kuwepo kesi polisi kwenye maandishi Ni ngumu Sana kumuwajibisha au kurudishiwa Simu yetu iliyoibiwa.
Nikasema sawa.

Na kingine, akasema Kama mwizi kaenda kuiflash ile kikawaida na imei number hajafanikiwa kufutika.
basi uwezekano wa kuitrack na kuikamata Ni mkubwa sana kupitia kitengo Chao cha ICT makao makuu.

Ila nao uko ICT wanataka Kwanza kesi iwepo kituoni kwny maandishi ndo waifanye kazi. Nikasema Basi wazo zuri Sana, fungueni kesi na Kama inawezekana ifuatilieni afu utanipa majibu afande tujue tunafanyaje.

Afande kasema POA, tukabadilishana mawasiliano na kumuacha afande pale kituoni. Binti karudishwa dukan kwa mamaJ , mamaJ nae kapelekwa kazini kwake, nami nikaenda kwenye shughuli zangu Kama kawaida. Siku ikaisha hivyo kwa utulivu.

Jioni yake nimeenda kwa mamaJ baada ya kufanya ya kufanya, nmeacha posho na nmeaga naondoka, mamaJ akaniomba nimsaidie nimtaftie binti yake Simu ndogo ya kutumia kwa MUDA, huku Simu ile iloibiwa ikiendelea kufuatiliwa na polisi maana bila mawasiliano dukani kwake kule Ni Changamoto Sana.

Nikamuuliza kwan ile Simu iloibiwa ilkuwa ya binti mwenyewe, Ni ya kwako au ni ya duka lako. Akasema ilikuwa ya binti mwenyewe binafsi. Nikamwambia basi ili siku nyingine awe makini, lazima umkazie na umwambie unamnunulia Simu ndogo ya kutumia itakuwa ya kwake manyw, ila mwisho wa mwezi ajue utamkata kwny mshahara wake ili awe makini next-time. Usipende kuendelea uzembe kazini, vitu vinapotea boss unalipa lipa TU kienyeji bila Kuchukua hatua, mfanyakazi wako atazoea na utapoteza vingn vingi zaid.

MamaJ Akasema sawa kanielewa, atamwambia binti. Nikamwambia kwakua Ni mambo ya dukan kwako, Simu ndogo ntanunua ila ntakukopesha, na pesa yangu mwisho wa mwezi ukipata mshahara unirudishie. Akasema haina shida nnachotaka Ni Simu tu kwanza, pesa italipwa.

Basi kesho yake kweli nmenunua Simu ndogo mpya ya Nokia 105 kwa elfu 40 na kumpeleka mamaJ, nikampa na risiti kuwa ntamdai elfu 40 yeye mwenyewe, hiyo simu akampatie binti yake wa dukani kwake aendelee na kazi. Akashukuru.
 
BAADA YA WIKI 1
Yule afande kanipigia kua suala la ile Simu kafanikiwa kule ict na inaonekana iliflashiwa ila imei number hawakufanikiwa kuzifuta na kuna namba mpya imeshajulikana inayotumika kwny ile Simu iloibiwa.

Kwahyo kinachohitajika wale jamaa wa ICT wanaomba Ela ya maji Elfu 50 ili watoe ile namba ya simu na location mnara inakosoma, ili yeye na timu yake wakaifatilie na kuikamata simu na mwizi husika.

Nikamwambia afande basi Ngoja Kwanza nimfahamishe boss wa yule binti aloibiwa Simu ili afanye mchakato haraka sana wa hiyo elfu 50 itumwe. Afande akasema POA.

Basi nikampigia mamaJ na kumpa taarifa zile, akasema elfu 50 Hana kwa Sasa, nimsaidie mimi kumlipia.
Nikamwambia nakulipiaje elfu 50 kwa Simu ya ofsin kwako na juz nmetoka kukununulia Simu ndogo ya kutumia kwa Muda. Inavoonekana wee hauko serious na kuipata Simu yako. Haiingii akilini kila kitu unalia lia nikusaidie Mimi. Hiyo ofisi yako unaiendeshaje haina hata akiba ya kucover changamoto ndogo ndogo Kama hizi.

Nnachokuelekeza Sasa,Toa pesa za dukan kwako haraka ukalipie hiyo elfu 50 kwa afande ili Simu irudi, acha mambo ya kijingajinga.ukishaikomboa simu yako utamkata binti mwnyw kwny mshahara wake kufidia pesa yako.

Akasema dukan hamna hela. Nikamwambia Basi tafuta sehemu ukakope, utarejesha mkishauza.
Akasema Hana sehemu ya kukopa.
Nikamwambia Basi nmegundua hauko serious na hili suala.

Nikamuuliza hivi kwahyo uko radhi Simu ya laki 6+ ipotee kwa kushindwa kulipa elfu 50 afande akaikamate Simu yenu? Akasema "Sasa Kama Sina Ela nifanyeje, wee mpenz wangu Kama huwez nilipia elfu 50 Basi acha hiyo Simu ipotee. Nihesabu hasara"

Nikamwambia,
"shaur zako, Kama mwnyw huna uchungu na Simu ya binti yako, Mimi Ni Nani niwe na uchungu nayo. Sasa Namrudishia jibu afande kua umesema huna Ela ya kukomboa hiyo simu. Tusije kulaumiana"

Mamaj Akasema "sawa Kama umeamua hivyo". Basi nikampigia afande na kumweleza aliyonijibu mamaJ. Afande akatushangaa Sana.

Afande akasema tatzo baadhi ya Watu wanadhan labda na sisi maafande tukiomba ela ya maji kwny ishu za hivi tunataka kuwatapeli, kwasasa mjini Hakuna mtu atakufanyia jambo lako bure bure. Sisi wenyewe maaskali wenyewe kwa wenyewe Ni binadamu, tuna familia na majukumu mengi. Na vyote vinahitaji saa pesa, kipato chetu halali hakitoshelezi, Watu wakiomba ya maji sio kwamba wanataka rushwa ,kutapeli mtu au vipi, Ni ktk kusaidiana TU maisha yaende.

Uyo mwanamke mwambie simlazimishi. Kama yeye kashindwa kutoa elfu 50, ntaitoa Mimi mwnyw maana kwa kazi iliyofanyika kurudi nyuma haiwezekani, ntaonekana mswahili nisipowalipa watu Ela yao ya maji, ila nikuahidi tu brother kua Hii simu ikipatikana naiuza mwnyw pesa ndefu na nisilaumiwe. Na ntakupa na ushahidi kabisa. Basi tukaagana na kukatisha mazungumzo yale. Kisha majibu Yale nikampa mamaJ, ila akaonesha kutojali uku lawama akizitupia kwangu kua namtelekeza kwny matatizo yake simsaidii.
Nikamwambia hata kusaidiwa nawe jivute vute kdg, sio kila kitu Mimi.
Kama hawez kukomboa hiyo Simu shaur zake. Afande akiikomboa ataiuza.

 
BAADA YA SIKU 5,
Ndo nafunga duka saa 11 jioni niondoke Afande yule kanipigia kua niende kituon Mara Moja anashida na Mimi.
Basi nikaenda. Kufika akanionyesha ile Simu na kuniuliza Kama Ni yenyewe. Nikamwambia sina uhakika sana labda nimuite mamaJ ndo anaifahamu vizur. Kweli mamaJ kapigiwa Simu,akasema ndo Yuko njian anaelekea nyumbn,Basi Ngoja ageuze na kuja kituoni. Tukamsubiri. Na kweli kafika.

Baada ya kuiona Simu na kuitambua akasema Ni yenyewe na kafurah Sana imepatikana. Basi mamaJ akaomba apatiwe Simu ile aondoke nayo. Akampa afande elfu 5.

Afande hiyo elfu 5 akaikataa akasema Hii Simu mpk pale imepatikana, imetumia zaid ya 150,000 maana alilipa elfu 50 kule ict, elfu 50 ya mafuta kufuatilia na elfu 50 ya posho za Watu alioambatana nao. Bado Muda waliopoteza kufuatilia Simu mtaa kwa mtaa. Jumla 150,000 cash.

Ila kwasababu tulijifanya wakaidi sana tulipoambiwa tutume pesa, basi ile Simu tuilipie 250,000 cash atupatie.
ili apate faida yake Cha juu laki 1 maana katumia gharama zake.
Mama J ghafla akahamaki. Nikamwambia jamaa Basi Ngoja tukazungumze mara moja pembeni na huyu mwanamke tujue tunafanyaje. Afande kasema sawa.Tukatoka nje na mamaJ.

Nikamkalisha na kumwambia tunafanyaje Sasa khs pesa ya jamaa, tulizembea kipind kile,Sasa Simu imepatikana, lete 250k ya afande tuikomboe Simu. MamaJ Akasema Hana ela,IPO elfu 5 tu. Nikamuuliza kwahyo tunafanyaje sasa. Akasema afande muongo usikute anataka kutupiga Cha juu,hajatumia gharama zote hizo.

Nikamwambia habar za gharama alizotumia hazihusiki Tena Hapa, tayar tushaingia Cha kike, tunafanyaje kuikomboa Simu na afande hawez kutupa bure bure au kwa hiyo elfu 5.
Mamaj Akasema huyu afande asilete ujuaji na uhuni, tukamripoti takukuru ili Hii Simu tukaichukue bure, Takukuru hatutoi hata Mia. Na atatulipa na fidia.
Nikamwambia achana na mawazo ya kipumbavu, mtu anataka kukusaidia afu unataka ukamchome? Una akili timamu kweli. Hizi Ni roho za kichawi.

Mamaj Akasema, hata Kama kutusaidia ila kwa 250,000 katupiga parefu sana, hajatumia gharama zote hizo zote. Nikamuuliza Kwan hiyo Simu ya binti yako inathaman kias gan ukilinganisha na hiyo 250,000. Akasema binti Simu alinunua 630,000 ndo risiti yake aliyowasilisha polisi imeandikwa.

Nikamwambia kwa ilivo tumika haijachakaa kabisa, kwa street value kwa 500,000 hiyo Simu afande akiamua kuiuza bado inauzika haraka sana.Toa pesa tumalizane hili jambo.
MamaJ akasisitiza pesa nitoe Mimi kwa kumkopesha Kisha atanirudishia akishauza dukan kwake.

Nikamwambia hauko serious,
Kisimu kdg nmetoka kukukopesha, Hii Simu kubwa nayo unataka nikukopeshe. Hii hapana. Hi Nicole pesa ndefu afu Nikukumbushe TU

"Tatizo lako Ni Moja TU, unashindwaga kutofautisha mapenz na pesa. zaman kdg niliwahi kukukopesha pesa ndefu, nilipodai pesa yangu MDA mrefu umepita hunilipi, ukanijibu wazi huilipi Hata nifanyeje Maana mimi Ni mpenz wako, nakulala siruhusiwi kukudai. Nilikwapua mkoba wako,nikachukua pesa za ofsn kwako kwa makusudi na nikajilipa Deni langu kwa lazima. Ukanuna balaa mpk ukatishia Kama vipi tuachane. Nikasema poa. Kisha rukarudiana. Na Hili sii Mara Moja Mara mbili kila akikopesha pesa,hata hizi pesa ndogo hurudishi kabisa. Hata hi ya kisimu kdg Ni hati hati kunirudishia"

Basi mamaJ akaanza kulalamika namsimanga, nikamwambia sikusimangi, nakwambia ukweli ili ubadilike. Hatuwez kuishi Mimi Na Wewe,Tena mpenz wako afu naogopa kukukopesha pesa, haya sio mapenz. Ujue hata Watu wanatushangaa tunaishi maisha ya kuviziana kwny pesa. Tabia yako imenifanya hata ukiwa na shida nisijitoe Sana kwako Maana una tatizo la ukikopeshwa hurudishi, Kisingizio sisi Ni wapenzi.

Basi mamaj akakasirika na kusema Kama siwez kumlipia hiyo Simu yeye anaondoka zake, ataenda kumnunulia binti yake simu mpya. Tuone mimi na afande tutafaidi Nini. Kwa jazba kaondoka.

Mimi nikarud ndan kwa afande na kumfahamisha alichonijibu mamaJ.
Afande akasema haina shida anapatia dalali wake akaiuze 300,000 haraka.
Ikabd nimuombe niinunue mm, tuachane na habar za yule mwanamke au dalali. Afande akasema nimpe hiyo 250,000. Nikaomba heri tukashuka mpk 180,000 nikalipia na Kuchukua ile Simu.

 
BAADA YA HAPO
Afande akasema anaichukua hiyo 180,000 TU kwasababu aliekamatwa nayo tayar keshawalipa 1,000,000 ya usumbufu maafande waliohusika kumkamata. Kwny hiyo mgao wa mil 1 yy aliambulia 200,000 tu, Kwaiyo sio mbaya itajifidia humo humo maana walimchimba mkwara kua aliyeibiwa Simu alivamiwa na kuuwawa, wanaimalizaje kesi. Ndo jamaa akawapoza hiyo mil. 1 chap.
Ikaisha tukaagana na kuondoka na ile Simu.

Basi nikaelekea kwa mamaJ,
Kufika nmeingia tumeketi kitandan
Nikamwambia kua simu ya binti tayar nmeshaikomboa, rudisha pesa yangu 180,000 cash Kama huna hiyo 250,000 ili nikafanye mambo mengine maana tayar nishavuruga hesabu zangu kuilipa hiyo 180k pale polisi.

Mama j akajua masihara, akaanza kusema kua tayar huo ukurasa wa simu keshaufunga, Simu itaenda kununuliwa mpya. Afande abaki nayo hiyo Samsung tuone Kama atafaidi.

Basi Ikabd kuitoa mfukoni na kumuonyesha live, mamaJ kashangaa na kuanza kunieletea mahaba mengi ya ghafla akinishika shika kidevu akinichum na kunisifia Mimi Ni mwanaume jembe, anajivuniankua na Mimi, hakuamini Kama ningeikomboa au ingepatikana tena.

Anaomba nimpatie hiyo Simu. Nikamwambia asilete mahaba kwenye maswala ya pesa. Leo Niko kikazi zaidi, lete 180k mezani upewe Simu yako. Akasema Hana hyo hela.

Nikamwambia,
Kama Huna hiyo hela Basi lete 150,000 pamoja na kile kitochi nilichokukopesha nikupatie Hii Simu. Akasema Hana Ela yoyote ndani.

Basi nikamwambia Hii simu naenda kuihifadhi, ikipita siku 2 ujaleta pesa naenda kuiuza na tusilaumiane.
Akasema Kama nikiamua kuiuza ili kumkomoa, niuze ila sawa TU.

Nikamwambia siiuzi ili kukukomoa,naiuza ili kurudisha pesa zangu nilotumia kuikomboa, Ela nilolipa polisi nmetoa kwny mzunguko wangu, kwahyo siwez kuyumba na nna Simu yenu ndani. Ntaiuza straght.
Basi nikamuachia posho yake, nikaaga na kwenda nyumbani kwangu.

 
BAADA YA SIKU 2 ZA DEADLINE KUPITA
Ikaongezeka siku ya 3 bado kimya, ikabd nitafte watu wangu wa karibu wanaoweza kuipush ile Simu haraka haraka nipate pesa nifanya mbo mengine.

Miongoni mwa wale Watu nikampata na bodaboda wa mamaJ na kumwambia nna Simu yangu samsung imetulia naipush kwa 350,000, nnachotaka nipate tu 250,000 nitaftie mteja wa haraka haraka jamaa. Akasema POA. Kisha nikamtuma picha zake WhatsApp Kwny Simu ya rafki yake.

Hatukukawia Sana,
Siku 3 mbele kanambia kuna sista mmoja mteja wake sana anaitaka, anayo 250,000 ila kamwambia anauza 350,000 mimi nikomae mwisho 300,000 ili apate ya maji.
MDA si mrefu atampa Simu mbele yake ili niongee nae tukubaliane bei. Nikasema sawa. Mpelekee Simu.

Kwny Simu, dada akasema Simu kaipenda ila 350,000 Hana. Nikamuuliza IPO Bei gan sasa.
dada akasema ipo 250,000 tu.

Nikamwambia hiyo Simu, sista kwa 250,000 haiendi maana bado mpya Kama unavoiona imetumika mwezi tu na Dukani Ni 650,00. Hiyo simu bei yake mwisho 300,000. Naiuza TU kwasababu nmenunua Simu nyngn Kali Zaid ya hiyo.

Basi Sista akaomba kuja kuikagua, nikamwambia boda uyo uyo akulete uikague. Basi boda akamleta yule dada dukan kuikagua Simu, kaipenda kaomba apunguziwe na Tukakubaliana mwisho 280,000. Sista kalipia 280,000. Kisha wakaondoka na boda.

Baadae boda kanipigia nampozaje maji yetu Yale, nikamwambia aje dukan, kaja na nikampatia elfu 30 yake Kama Cha juu maana tulishakubaliana tangu mwanzo kua mimi nahitaji top top 250,000 TU. Itakayozid ya kwake. Nikampatia akaondoka na Maisha yakaendelea.

Sasa Juz mamaJ kanipigia analalamika kwamba Mimi mwanaume sifai hata kidg, inavoonekana nafurahia matatzo yake. Haiwezekani Simu ilioibiwa dukan kwake nmeikomboa na nmekwenda kuiuza kwa boda wake kwa 280,000.

Akalalamika kua anawasiwasi Mimi huenda ndo nmetuma Watu waibe ile Simu ili niiuze nipate faida, mwanaume gani Sina utu nnaangalia fedha TU, sijali anapitia kipind gan, nayatumia matatizo yake kujinufaisha kiuchumi maana polisi anajua niliikomboa kwa 180,000 afu anashangaa anamkuta nayo boda na kumwambia alinunua kwangu kwa 280,000. Nnapenda Sana Ela na hazitonifikisha popote.

Ikabd kumfahamisha kua tusileteane mapenz na masihara kwny maswala ya pesa. When am talking abt business, namaanisha kweli am in business. Nilikupa deadline na ukashindwa kuitekeleza. Kwahyo sikua na namna Zaid ya kuiuza na kurudisha pesa zangu.

Na namshkuru mungu na faida kdg ya mafuta na usumbufu zile nenda Rudi nmepata. Kwahyo wee lalamika tu mpk uchoke,ila jua tayar Simu yenywe ishauzwa na haiwez kurudi tena.
Kanunue Simu nyngn mpya Kama ulivyoahidi. Basi nikamkatia Simu.

Ikabd Sasa kumpigia boda imekuje Simu ile kakutwa nayo na mamaJ na iliuzwa kwa yule sista, akasema alikua amempakia kwny pikpik aliposhuka kwake kupokea simu ya mteja mwngn akaiona na kumwambia Simu nzur Katoka kwny kitochi lini, aliipenda Sana ,kainunua wapi,ndo akasema nmeinunua kwangu. Kisha ikaisha hivyo.

Boda Akakiri kua alinidanganya TU, ile Simu aliipenda sana na alikua ananunua yeye na sio yule sista.
Nikamuuliza ilikuaje Sasa, akasema alimtuma TU yule mdada pisi Kali akiamini atapunguziwa Bei zaidi. Kuliko akiinunua yeye mwnyw km mwanaume.

Nikamuuliza Sasa Mbona Bei niliuza ile ile 250,000 Nilokwambia mwanzo, si ungenunua ww mwnyw Moja kwa Moja kwangu kuepuka usumbufu.
Akasema alitegemea kwasababu Ni pisi kali labda ile 250,000 nayo ingeshuka zaidi ya hapo.

Akaongezea kua,
Alivoona sijatetereka sn kwny kuiuza kwasababu ya yule pisi kali ikabd ampe tip dada kua inunuliwe hivyo hivyo waondoke kunasehem anawahi na yule dada alikwenda kumpoza kwa elfu 5 uko mbele ya safari. Basi nikasema haina shida. Fresh. Tukaagana nikakata Simu.

Sasa Jana usku nmeenda kwake,
Kaninyima hadi penzi,kanuna balaa kisa suala Lile la Simu niliyouza. Nilichomwambia yeye anune awezavyo mpk apasuke, Tisiingize mahaba kwenye masuala ya pesa na biashara.

Pesa za biashara hazitakiwi kuchanywa na pesa za mapenzi.
Ili tufike mbali lazima Tuheshimu makubaliano.

HIVI VITU VIWILI HAVIWEZI KUCHANGANYIKA HATA SIKU MOJA.

Basi Baada ya kumwambia hivyo,
Nikavaa nikamuachia posho Yake na kuondoka zangu kuelekea nyumban kwangu.

########mwisho#####

NAWASILISHA WAKUU
 
Siku nyingi sana sijasoma post zako mkuu. Safi sana kwa kusimamia msimamo wako.Wanawake wengi wakikopeshwa pesa na wapenzi wao huwa hawalipi kwa kigezo cha kutoa mbunye zao. Next time atakuheshimu linapokuja suala la pesa.

Ila nakulaumu mkuu kwa kushindwa kuikomboa simu kwa elfu 50 ,ungelipa pale mama J alipogoma kutoa pesa then ungekuja kuiuza kwa pesa ndefu zaidi.

Funzo nje ya story, tuwe makini sana kununua simu za mikononi, simu ya laki moja unaweza ukaja kuinunua kwa milioni moja na laki moja.
 
Siku nyingi sana sijasoma post zako mkuu. Safi sana kwa kusimamia msimamo wako.Wanawake wengi wakikopeshwa pesa na wapenzi wao huwa hawalipi kwa kigezo cha kutoa mbunye zao. Next time atakuheshimu linapokuja suala la pesa.

Ila nakulaumu mkuu kwa kushindwa kuikomboa simu kwa elfu 50 ,ungelipa pale mama J alipogoma kutoa pesa then ungekuja kuiuza kwa pesa ndefu zaidi.

Funzo nje ya story, tuwe makini sana kununua simu za mikononi, simu ya laki moja unaweza ukaja kuinunua kwa milioni moja na laki moja.
Isome story mpk mwisho,
Kuna sehemu ujasoma,simu niliuza kwa faida
 
BAADA YA WIKI 1
Yule afande kanipigia kua suala la ile Simu kafanikiwa kule ict na inaonekana iliflashiwa ila imei number hawakufanikiwa kuzifuta na kuna namba mpya imeshajulikana inayotumika kwny ile Simu iloibiwa.

Kwahyo kinachohitajika wale jamaa wa ICT wanaomba Ela ya maji Elfu 50 ili watoe ile namba ya simu na location mnara inakosoma, ili yeye na timu yake wakaifatilie na kuikamata simu na mwizi husika.

Nikamwambia afande basi Ngoja Kwanza nimfahamishe boss wa yule binti aloibiwa Simu ili afanye mchakato haraka sana wa hiyo elfu 50 itumwe. Afande akasema POA.

Basi nikampigia mamaJ na kumpa taarifa zile, akasema elfu 50 Hana kwa Sasa, nimsaidie mimi kumlipia.
Nikamwambia nakulipiaje elfu 50 kwa Simu ya ofsin kwako na juz nmetoka kukununulia Simu ndogo ya kutumia kwa Muda. Inavoonekana wee hauko serious na kuipata Simu yako. Haiingii akilini kila kitu unalia lia nikusaidie Mimi. Hiyo ofisi yako unaiendeshaje haina hata akiba ya kucover changamoto ndogo ndogo Kama hizi.

Nnachokuelekeza Sasa,Toa pesa za dukan kwako haraka ukalipie hiyo elfu 50 kwa afande ili Simu irudi, acha mambo ya kijingajinga.ukishaikomboa simu yako utamkata binti mwnyw kwny mshahara wake kufidia pesa yako.

Akasema dukan hamna hela. Nikamwambia Basi tafuta sehemu ukakope, utarejesha mkishauza.
Akasema Hana sehemu ya kukopa.
Nikamwambia Basi nmegundua hauko serious na hili suala.

Nikamuuliza hivi kwahyo uko radhi Simu ya laki 6+ ipotee kwa kushindwa kulipa elfu 50 afande akaikamate Simu yenu? Akasema "Sasa Kama Sina Ela nifanyeje, wee mpenz wangu Kama huwez nilipia elfu 50 Basi acha hiyo Simu ipotee. Nihesabu hasara"

Nikamwambia,
"shaur zako, Kama mwnyw huna uchungu na Simu ya binti yako, Mimi Ni Nani niwe na uchungu nayo. Sasa Namrudishia jibu afande kua umesema huna Ela ya kukomboa hiyo simu. Tusije kulaumiana"

Mamaj Akasema "sawa Kama umeamua hivyo". Basi nikampigia afande na kumweleza aliyonijibu mamaJ. Afande akatushangaa Sana.

Afande akasema tatzo baadhi ya Watu wanadhan labda na sisi maafande tukiomba ela ya maji kwny ishu za hivi tunataka kuwatapeli, kwasasa mjini Hakuna mtu atakufanyia jambo lako bure bure. Sisi wenyewe maaskali wenyewe kwa wenyewe Ni binadamu, tuna familia na majukumu mengi. Na vyote vinahitaji saa pesa, kipato chetu halali hakitoshelezi, Watu wakiomba ya maji sio kwamba wanataka rushwa ,kutapeli mtu au vipi, Ni ktk kusaidiana TU maisha yaende.

Uyo mwanamke mwambie mlazimishi. Kama yeye kashindwa kutoa elfu 50, ntaitoa Mimi mwnyw maana kwa kazi iliyofanyika kurudi nyuma haiwezekani, ntaonekana mswahili nisipowalipa watu Ela yao ya maji, ila nikuahidi tu brother kua Hii simu ikipatikana naiuza mwnyw pesa ndefu na nisilaumiwe. Na ntakupa na ushahidi kabisa. Basi tukaagana na kukatisha mazungumzo yale. Kisha majibu Yale nikampa mamaJ, ila akaonesha kutojali uku lawama akizitupia kwangu kua namtelekeza kwny matatizo yake simsaidii.
Nikamwambia hata kusaidiwa nawe jivute vute kdg, sio kila kitu Mimi.
Kama hawez kukomboa hiyo Simu shaur zake. Afande akiikomboa ataiuza.

Mama j chenga
 
Back
Top Bottom