Mchakato wa uteuzi wagombea ubunge wa EAC kupitia CHADEMA

Tumaini Makene

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
2,642
6,071


TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTEUZI WA WAGOMBEA WA UCHAGUZI WA WAJUMBE WATAKAOIWAKILISHA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI (EALA) KUPITIA CHADEMA

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinatoa taarifa kwa umma kwamba uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kugombea ujumbe wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) kupitia CHADEMA umekamilika tarehe 6 Aprili 2012 saa 10 Jioni.

Uteuzi wa mwisho wa wagombea utafanyika tarehe 9 Aprili 2012 siku ya jumatatu kuanzia saa 3 asubuhi ambapo wagombea wote waliorudisha fomu wametaarifiwa kufika kwenye mkutano husika.

Wagombea waliorudisha fomu mpaka sasa ni pamoja na Godfrey Mnubi, Edgar William Chibura, John Simon Malanilo, Patrick Lubango Nkandi, Anna E. Maghwira, Deogratias George Assey, Pasquina Ferdinand Lucas, Deusdedit Jovin Kahangwa, Antony Calist Komu na Mwantum Khamis Mgonja.

Ikumbukwe kuwa tarehe 12 Machi 2012 Katibu wa Bunge alitoa Taarifa kwa Umma kwamba,Uchaguzi wa wajumbe tisa (9) watakaoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki utafanywa na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, wakati wa Mkutano wake wa Saba utakaofanyika Dodoma, kuanzia tarehe 10 hadi 20 Aprili, 2012.

Uchaguzi huo wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki unafanyika kwa kuzingatia kuwa maisha ya Bunge hilo lililoingia madarakani mwaka 2006 yatafikia ukomo wake 04 Juni, 2012.


Taarifa imetolewa kwa vyombo vya habari na:
John Mnyika
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
07/04/2012
 
Asante kwa taarifa, naomba mtoe watu makini.

Nategemea wa kutusemea EAC kutoka huku wale wengine wamelamba makarasa tu.
 
fomu mlianza kutoa lini? mbona mambio kimya kimy aau mimi ndip nilikuwa sina taarifa
 
Last paragraph, tarehe ya ukomo wa Bunge ni sahihi kweli?. I guess something is not right!
 
Bunge linalozungumziwa hapo si lile la JMT bali la EAC. Ni sahihi.
@Bubona
 
Ninachokiamina akilini na nafsini mwangu ni kwamba CHADEMA ni chama makini huwamnafanya maamuzi yasiyo na majuto kwenu na kwa raia pia nawapongeza kwa hilo sasa ni imani yangu mtachagua wabunge wenye nafasi ya kuijua EAC atleast kwa karibu kama sio kwa undani sana "Put the right man at the right place".
 
Duh Mabere Nyaucho Marando hajajitokeza? Naona Komu naye ndani ya nyumba!
 
wakuu nielewesheni kitu hapa, uchaguzi huu unakuwaje palebungeni, wagombea wote wa CCM&Upinzani hupigiwa kura pamoja?na kivipihakuna biasness kwa CCM dhidi ya candidates wa upinzani, nombeni msaada wakanuni
 
fomu mlianza kutoa lini? mbona mambio kimya kimy aau mimi ndip nilikuwa sina taarifa

Tangu mwanzo mchakato ulikuwa ukiwekwa public kupitia vyombo vya habari. Ndiyo maana wagombea wengine walijitokeza mara baada ya kusoma katika vyombo vya habari.
 
Asante kwa taarifa, naomba mtoe watu makini.

Nategemea wa kutusemea EAC kutoka huku wale wengine wamelamba makarasa tu.

Ungejua usemacho wala usingeandika hivi. Wanaochagua wabunge wa EAC ni bunge zima, sasa jiulize wengi ni wapi ndani ya bunge? Wanao amua hapa nani awe mbunge ni CCM
 
Mambo ya ajabu kabisa Chadema wanafanya uteuzi halafu CCM ndio wanawachagulia mbunge.
 
Back
Top Bottom