Kingmairo
JF-Expert Member
- Apr 7, 2012
- 4,936
- 3,533
Sababu haswa ya kubomolewa .hiyo nyumba ni ipi kati ya hizi?
1. Alisema nyumba hizo, zimevunjwa kwa kuwa zimejengwa bila kibali cha ujenzi kutoka Manispaa ya Kinondoni.
2. Mama Lwakatare hana hati ya kumiliki eneo hili wala kibali cha kujenga nyumba kutoka Manispaa ya Kinondoni.
Awali ofisi ya Ardhi ilipokea malalamiko kutoka kwa mmiliki halali wa eneo hilo, Janeth Kiwia, kwamba eneo lake limevamiwa na kujengwa bila kibali Desemba 24.
Zote hizi ni sababu mkuu. Kwa mujibu wa sheria hata kama una umiliki halali wa eneo ni lazima upate BUILDING PERMIT toka mamlaka husika. Ukijenga bila kibali hata kama una hati ya kiwanja chako wakiamua kukubomolea wapo ndani ya matakwa ya sheria, kwasababu umekiuka sheria. Hivyo hata kama aliuziwa na kulikuwa na mgogoro wa umiliki, kisheria hakupaswa kujenga permanent structure yoyote mpaka michoro yake ya ramani ipitishwe na wahandisi wa manispaa na apewe kibali cha kuanza ujenzi.