Nimeona kwenye mitandao jinsi mchungaji kenan mwasomola alivyokuwa amewa kwa hisia kali na hasiri akikosoa uimbaji wa siku hizi makanisani kwamba sio wa roho mtakatifu. Amekosoa jinsi makanisa kutumia mitindo ya nyimbo na muziki wa kidunia kama vile Rap/R&B, Jazz, Reggae, Singeli nk na kuimba kwa kufokafoka. Yaani vyombo vinapigwa kwa fujo kama baa.
Binafsi nimemuelewa sana maana hata mimi kanisa langu la lutheran ni shida, yaani ni miziki na kinachoitwa pambio full mkoko utafikiri watu wapo disco. Kwenye makanisa ya kilokole hali ndio mbaya zaidi. Halafu kwasababu imeandikwa kuwa watu wamuimbie bwana kwa vinanda na vinubi basi ndio hoja wanayosimama nayo lakini kimsingi makanisa mengi siku hizi ni vurugu tu. Kanisa pekee lililobaki ni kanisa katoliki tu ndilo linalomuabudu mungu na kumsifu kwa heshima na ustaarabu.
Yaani makanisa yetu sasahivi nikushindana kununua vyombo vya muziki mkubwa.
Pia kunazidi kuongezeka wahubiri wakujitegemea wengi mitaani na barabarani ambapo mtu ukinunua spika yako moja na micphone basi tayari ni kanisa. Sasa hivi makanisa ya barabarani na stendi za daladala ni balaah cha msingi spika yako kubwa, mic na chombo cha kukusanyia maokoto.
Uhuru wa shughuli za dini umekuwa holela sana na watawala wanaogopa kuweka utaratibu kwa hofu ya kukosolewa.
Askofu Malasusa hebu turejeshee Lutheran yetu ya miaka ya 80 na 90 iliyokuwa lutheran iliyojengeka katika imani ya kweli, ustaarabu ndani ya ibada/kanisa na mafundisho/mahubiri ya injili ya kweli na kuishi maisha yenye kumpendeza Mungu. Siku hizi 80% ya mahubiri ni yale ya kidunia, kupata kazi, kuolewa, kufanikiwa kimaisha na msisitizo wa matoleo na michango halafu mziki mkubwa watu waimbe kama na kucheza kwa kujimwaga.
Lutheran imekuwa haina tofauti na makanisa ya kilokole.