Mbwa ana akili kuzidi punda au punda wa Tanzania ana huruma kuzidi mbwa?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
5,036
6,837
Punda wa Tanzania bado hajampata mtetezi. Ukikutana na punda wa Kanda ya Ziwa, ni kawaida kuona michubuko migongoni na shingoni. Michubuko hiyo imetokana na ama vipigo, au kubebeshwa mizigo mizito iumizayo au vyote kwa pamoja.

Asipokuwa na hizo alama, ujue huyo punda anamilikiwa na msomi aliyeelimika, hivyo anajali mpaka wanyama punda akiwemo, au ni mcha Mungu hivyo hana tabia ya kuwatesa wanyama kwa vipigo kwa sababu anajua ni viumbe vya mwenyenzi Mungu, na ana jukumu la kuvitunza na kuvihudumia kwa upendo.

Nimeshangazwa na jambo moja! Pamoja na vipigo vyote wanavyopata, punda wameendelea kuwa wavumilivu na watiifu kwa wamiliki wao. Mbwa asingefanya hivyo. Labda kuhakikishwe kuwa hapati upenyo wa kutoroka.

Tokea tukiwa wadogo, tulijifunza kutokumpiga mbwa wa watu bila kosa. Kama akiwa kwenu au njiani na ukamtendea ndivyo sivyo, tuliamini kuwa siku na wewe ukiingia kwenye kumi na nane zake (ukiendaa kwao) , atalipiza kisasi. Kwa kiasi kikubwa, tulikuwa sahihi, kulingana na mbwa wa enzi hizo kule kijijini kwetu.

Hata kwa miaka ya hivi karibuni, nilishuhudia jinsi watu fulani walivyomfukuza mbwa wao ambaye walikuwa hawamtaki tena, japo walishakaa naye kwa muda mrefu.

Kwanza, walianza kumpiga bila sababu na kumnyima chakula. Huo ukatili ulimfanya huyo mbwa awaogope, na akawa anakuja mara moja moja kwa kujiibia. Baada ya siku chache, alitoweka na hakuonekana tena.

Bila shaka, alijiridhisha kuwa hatakiwi tena na hivyo akaamua kutafuta "ustaarabu" mwingine.

Mbwa alijiongeza baada ya kuona matendo anayotendewa si sahihi! Punda anashindwaje kujiongeza kama wafanywavyo mbwa?

Kwa jinsi baadhi ya wafugaji wanavyowatesa punda zao, natamani hao Pinda wajiongeze na kutoroka na kisha kujipeleka mahali wakakokubalika na kuthaminiwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom