Mbunge wa Mwibara aanza kupoteza sifa ya Ubunge

Jimbo la mwibara mbona linawatu makini sana! Namkumbuka mh.Bahati Mtamwega Mgaywa! Huyu jamaa alikuwa mnyenyekevu sana, na alikuwa karibu na wananchi wake wala hakupora maeneo kama kangi! Nimefuatilia nimebaini huu mgogoro upo kwa chini chini na mbunge ni sehemu ya tatizo wala hakuna mambo ya kisiasa hapo.

Namshauri kijana wa uvccm apeleke pingamizi mahakamani ili mbunge aitwe na haki itendeke.
 
Ccm ni janga la taifa wabunge wote wa ccm hawatakiwi kabisa
 
Ccm ni janga la taifa wabunge wote wa ccm hawatakiwi kabisa

Umenena mkuu! Yani wanalaana! Wamekaa kifisadifisadi tu; hata Lugola walewale; amejificha kwenye serikali 3 ili apate upepo wa kisiasa kumba janja janja ni gamba tu hana jipya!
 
Jimbo la mwibara mbona linawatu makini sana! Namkumbuka mh.Bahati Mtamwega Mgaywa! Huyu jamaa alikuwa mnyenyekevu sana, na alikuwa karibu na wananchi wake wala hakupora maeneo kama kangi! Nimefuatilia nimebaini huu mgogoro upo kwa chini chini na mbunge ni sehemu ya tatizo wala hakuna mambo ya kisiasa hapo.

Namshauri kijana wa uvccm apeleke pingamizi mahakamani ili mbunge aitwe na haki itendeke.

Umenikumbusha mkuu! Mtamwega nilisoma vitabu vyake vya uraia.( civics) yani nilivipenda sana sielewi kama vijana bado wanavitumia.
 
Kuna inzi wangu kanitonya kuwa, baada ya baba yake na kijana wa uvccm kufariki ndipo Kangi na mafisadi wake wakaanza kuvamia eneo la marehemu, mjane mke wa marehemu akawakurupusha wakatulia!

Naomba nimsaidie uvccm kuna kitu kinaitwa, adverse possesion, hii inampa mtu right to the land ikiwa amekaa kwenye ardhi zaidi ya miaka 12.

Lakini pia ukumbuke ardhi yote ya Tanzania ni mali ya umma na kwa manufaa ya umma watu wanaweza ambiwa wapishe na kulipwa fidia, yaani stahiki zao na kwa wakati!
 
Hii imetulia! Ila kwa mbunge kama Kangi namshauri awe sehemu ya kutatua migogoro!
 
Jimbo litalobaki ccm mkoa wa mara ni la kangi lugola tu,kwasababu yeye huwa hatekelezi sera za kifisadi za ccm
 
Mhh!! Wabunge wetu nao ni shidaaaa!!!! Wanaangalia matumbo yao tu! Sasa anaingiaje kwenye eneo la wetu wengine? Huu si ndiyo uonezi kwa watu wasio jua sheria! Kama kuna uwezekano mpelekeni mahakamani ili mpate haki yenu. Watu wakipata pesa wanaanza kuumiza watu wa kawaida ndo kama hivyo! Mbunge unashindwa kujali hata mali za watu wengine! Ccm imeoza yote tuwekeeni upinzani wananchi wanateseka sana. Mwibara maendeleo hakuna ni migogoro nenda rudi. Tumechoka!
 
Jimbo litalobaki ccm mkoa wa mara ni la kangi lugola tu,kwasababu yeye huwa hatekelezi sera za kifisadi za ccm

Gamba ni gamba tu! Linatumia mbinu za kimkakati kuunusuru ubunge, lakini hakuna cha kangi eende huko na li chama lake tumemchoka! Hawezi kutisha wananchi wake kwa tamaa ya ardhi akasalimika pesa kitu gani banaa!!
 
heshima kwenu wana ukumbi!

Leo nimekutana na wapiga kura wa mh.Kangi Ndege Lugola mbunge wa mwibara wakimlaumu mh.Mbunge kwa kitendo chake cha kiovu alichomfanyia mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Kibara tar.02.09.2014!

Wanachama wa ccm walishangazwa kuona mbunge wa jimbo lao; akitoa shinikizo kwa mkuu wa kituo cha polisi kata ya Kibara kuondoka na maaskari wanne wakiwa na bunduki mbili aina ya SMG na kumkamata kiongozi wa chama(jina limehifadhiwa) kwa madai kwamba yeye ni jambazi amevamia veta yake na kukata miti ovyo katika eneo lake. Mwenyekiti aliwekwa maabusu kuanzia saa 11 jioni mpaka kesho yake saa 3 asubuhi ndipo akapata dhamana.

Taarifa za ndani zilionekana mbunge alitoa shinikizo kwa askari polisi kumlazimisha huyo kiongozi wa chama, kuweka maandishi ya kukubali tangu leo; asifanye shughuli yoyote ya maendeleo ndani ya eneo hilo, kitu ambacho hakikuwezekana kabisa na mtuhumiwa alikataa na kudai familia inamiliki hilo eneo tangu Uhuru 1961.

Baada ya kufuatilia kwa wanakijiji; ilithibitika kuwa kiongozi huyo wa chama alikuwa kwenye shamba lao akiliandaa kwa ajili ya msimu wa kilimo, kama desturi yao ya kila mwaka. Shamba hilo lina upana wa mita 70 na urefu wa mita 104 sawa na mita za mraba 7280.

Baada ya kumtafuta kiongozi wa serikali ya kijiji cha Namibu(jina linahifadhiwa) aliyekuwepo wakati anapewa sehemu ya eneo hilo, alithibitisha hilo eneo ni mali ya familia anayotoka mwenyekiti wa UVCCM; na mbunge alipewa sehemu ya juu aliko jenga veta yake. Sehemu ya chini ni eneo halali la familia hiyo.

Kangi analazimisha apole eneo kwa njia za kifisadi; kitu ambacho mimi sikukubaliana nae, na niko tayari kwenda mahakamani kutoa ushahidi.

Wananchi walijaa hofu na kushaangaa silaha nzito za kuwindia majangiri zikipita mtaani; eti kuna majambazi yamevamia veta ya kangi! kumbe uongo mtupu! Kuja kuambiwa jambazi anaye tafutwa kumbe ni mwenyekiti wa UVCCM kijana mpole na mnyenyekevu! wananchi walimtupia lawama mkuu wa kituo cha polisi! na mbunge kwa kitendo cha kihuni alichokifanya.

Taarifa za ndani kutoka kwa katibu wa mbunge Mtesigwa Chikulugu! Zinasema kuwa; yeye ndiye aliyemshauri mbunge kumuachia kiongozi wa uvccm vinginevyo angemfunga amkomeshe alidai mmoja wa kiongozi wa karibu na Kangi.

Chanzo chetu cha habari kinadai huyu mwenyekiti wa UVCCM yuko kambi ya aliyewahi kuwa mbunge wa mwibara mh.Charles Mguta Kajege hivyo kumfanya Kangi kumalizia hasira zake kwa kijana huyo. Hizi ni habari za uhakika na popote alipo mbunge wa mwibara kama anabisha aje akanushe!

Tunaviomba vyombo vyote vya habari hasa ITV na redio one! kumulika huu mgogoro wa ardhi mpakani mwa taasisi ya hospitali ya Kibara.

Chanzo:
Wanakijiji Kibara na Namibu!

Huu uzi umekaa kichokonozi sana! ---- kuna na mengine mtujuze wana wa mwibara. Sauti ya umma ndiyo sauti ya Mungu! Tumieni vikao myamalize.
 
Mi mh.kangi namuelewa sana...hayo maneno yako ya urongo urongo sitaki

Unamuelewa kwa lipi! Ebu fafanua maana sijakusoma unachotaka kumaanisha! Urongo urongo hutaki ebu niweke sawa urongo wa shamba linalolalamikiwa au urongo upi?
 
Huu uzi umekaa kichokonozi sana! ---- kuna na mengine mtujuze wana wa mwibara. Sauti ya umma ndiyo sauti ya Mungu! Tumieni vikao myamalize.

Huu uzi hauchokonozi mtu! Unaweka fact kwa umma ili wajue ya kwamba, hawa wabunge wenye tamaa kama kangi! ni wakuogopa kama ukoma!

Anatisha watu na kuwaagiza polisi kufanya vitendo vya kiovu kwa raia ili waogope na kuachia haki yao ili haya majangiri ya ccm yaendelee kutawala kwa njia haramu!

Hii nchi ni yetu sote! kama Kangi anaamini ardhi ni mali ya Umma, atii sheria na asishawishi viongozi wa mtaa wenye njaa kali; kuuza utu wao na kusababisha migogoro kama hii isiyo na tija kwa wana wa Mwibara.
 
Mhh!! Wabunge wetu nao ni shidaaaa!!!! Wanaangalia matumbo yao tu! Sasa anaingiaje kwenye eneo la wetu wengine? Huu si ndiyo uonezi kwa watu wasio jua sheria! Kama kuna uwezekano mpelekeni mahakamani ili mpate haki yenu. Watu wakipata pesa wanaanza kuumiza watu wa kawaida ndo kama hivyo! Mbunge unashindwa kujali hata mali za watu wengine! Ccm imeoza yote tuwekeeni upinzani wananchi wanateseka sana. Mwibara maendeleo hakuna ni migogoro nenda rudi. Tumechoka!

Naam naam!! Wananchi kuweni macho sana na hawa wezi wa ardhi wanao jifanya eti wawekezaji; kumbe waporaji wa ardhi na wezi wakubwa!
 
Naam naam!! Wananchi kuweni macho sana na hawa wezi wa ardhi wanao jifanya eti wawekezaji; kumbe waporaji wa ardhi na wezi wakubwa!

Mimi natoka jimbo la Mwibara, naumia sana kuona wachumia tumbo wakitumia vibaya nafasi zao na kuanza kukwapua ardhi za watu walio kufa! Nimejilidhisha huu mgogoro hauna mausiano na chuki za kisiasa ndani ya makundi kama bandiko lilivyoeleza.

Kilichopo ni kwamba kuna shamba ndilo linalo leta shida! Ni vizuri Kangi akaueleza umma na wanakijiji kupitia mikutano ya wananchi juu ya uhalali wake wa kulinunua hilo eneo kutoka serikali ya kijiji cha Namibu! Mwenye kufahamu zaidi atujuze ili tupime wapi kuna shida.
 
Ndugu Yangu ni shida! Wananchi wa mwibara wameamka! Nawataarifu viongozi kuwa makini sana juu ya maswala ya ardhi. Hawa jamaa wamekomaa nadhani kangi hatoboi!
 
Kumekucha tena na makucha yake! Yawezekana wanaodaiwa kutaka kupora shamba sasa kuburuzwa mahakamani! Hizi ni taarifa za ndani nimedokezwa na mwanasheria ambaye ni mtetezi wa wanyonge karumbeta amedokezwa!
 
Haki inapatikana mahakamani na siyo kwenye majukwaa ya mitandao! Mwanasheria nakutakia kila la kheri!
 
Back
Top Bottom