Mbunge wa Mwibara aanza kupoteza sifa ya Ubunge

karumbeta

JF-Expert Member
Sep 20, 2014
214
39
heshima kwenu wana ukumbi!

Leo nimekutana na wapiga kura wa mh.Kangi Ndege Lugola mbunge wa mwibara wakimlaumu mh.Mbunge kwa kitendo chake cha kiovu alichomfanyia mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Kibara tar.02.09.2014!

Wanachama wa ccm walishangazwa kuona mbunge wa jimbo lao; akitoa shinikizo kwa mkuu wa kituo cha polisi kata ya Kibara kuondoka na maaskari wanne wakiwa na bunduki mbili aina ya SMG na kumkamata kiongozi wa chama(jina limehifadhiwa) kwa madai kwamba yeye ni jambazi amevamia veta yake na kukata miti ovyo katika eneo lake. Mwenyekiti aliwekwa maabusu kuanzia saa 11 jioni mpaka kesho yake saa 3 asubuhi ndipo akapata dhamana.

Taarifa za ndani zilionekana mbunge alitoa shinikizo kwa askari polisi kumlazimisha huyo kiongozi wa chama, kuweka maandishi ya kukubali tangu leo; asifanye shughuli yoyote ya maendeleo ndani ya eneo hilo, kitu ambacho hakikuwezekana kabisa na mtuhumiwa alikataa na kudai familia inamiliki hilo eneo tangu Uhuru 1961.

Baada ya kufuatilia kwa wanakijiji; ilithibitika kuwa kiongozi huyo wa chama alikuwa kwenye shamba lao akiliandaa kwa ajili ya msimu wa kilimo, kama desturi yao ya kila mwaka. Shamba hilo lina upana wa mita 70 na urefu wa mita 104 sawa na mita za mraba 7280.

Baada ya kumtafuta kiongozi wa serikali ya kijiji cha Namibu(jina linahifadhiwa) aliyekuwepo wakati anapewa sehemu ya eneo hilo, alithibitisha hilo eneo ni mali ya familia anayotoka mwenyekiti wa UVCCM; na mbunge alipewa sehemu ya juu aliko jenga veta yake. Sehemu ya chini ni eneo halali la familia hiyo.

Kangi analazimisha apole eneo kwa njia za kifisadi; kitu ambacho mimi sikukubaliana nae, na niko tayari kwenda mahakamani kutoa ushahidi.

Wananchi walijaa hofu na kushaangaa silaha nzito za kuwindia majangiri zikipita mtaani; eti kuna majambazi yamevamia veta ya kangi! kumbe uongo mtupu! Kuja kuambiwa jambazi anaye tafutwa kumbe ni mwenyekiti wa UVCCM kijana mpole na mnyenyekevu! wananchi walimtupia lawama mkuu wa kituo cha polisi! na mbunge kwa kitendo cha kihuni alichokifanya.

Taarifa za ndani kutoka kwa katibu wa mbunge Mtesigwa Chikulugu! Zinasema kuwa; yeye ndiye aliyemshauri mbunge kumuachia kiongozi wa uvccm vinginevyo angemfunga amkomeshe alidai mmoja wa kiongozi wa karibu na Kangi.

Chanzo chetu cha habari kinadai huyu mwenyekiti wa UVCCM yuko kambi ya aliyewahi kuwa mbunge wa mwibara mh.Charles Mguta Kajege hivyo kumfanya Kangi kumalizia hasira zake kwa kijana huyo. Hizi ni habari za uhakika na popote alipo mbunge wa mwibara kama anabisha aje akanushe!

Tunaviomba vyombo vyote vya habari hasa ITV na redio one! kumulika huu mgogoro wa ardhi mpakani mwa taasisi ya hospitali ya Kibara.

Chanzo:
Wanakijiji Kibara na Namibu!
 
Mkoa wa mara ccm imeshakufa,jimbo ambalo ccm watabaki nalo ni jimbo la kangi lugola na hii ni kutokana na misimamo yake na si kwa kukipenda chama
 
Mmhh!! Ardhi itatoa watu roho! Mbunge jipange vizuri na wananchi wako hii haijatulia kabisa!
 
Mkoa wa mara ccm imeshakufa,jimbo ambalo ccm watabaki nalo ni jimbo la kangi lugola na hii ni kutokana na misimamo yake na si kwa kukipenda chama

Misimamo yake haina madhara kwa chama chake! Pia anajificha kwenye misimamo ili kunusuru ubunge lakini hafai kabisa!
 
Huyo kijana wa UVCCM bado anangoja nini kuendelea kujumuika na majambaka hayo ya CCM !!!? Wakati ni huu aachane na Chuma Chakavu Marufuku[CCM]•
 
Ccm wamekwisha jimbo la mwibara wanataka mabadiriko wasipo yapata ndani ya ccm watayatafuta nje ya ccm. Ushauri kwa Kangi kuhusu mgogoro wa ardhi akajipange vizuri kwa wananchi wake vinginevyo itakuwa baraaaaaa!!!
 
OK nitafatilia kwa watu walioko huko bt uchaguzi n mwakani nahisi kama hujuma zimeanza za kisiasa

Hapana mkuu nenda Kibara utajionea mwenyewe wala hakuna mausiano ya uchaguzi.ngoja nikuoneshe chanzo cha mgogoro kwa picha. 1411411670680.jpg
 
Ni mwibara maeneo gani

Kibara hospitali karibu kabisa na majengo ya mbunge (Veta) ambayo nimekutumia picha yake. Eneo lenye utata ni kuanzia kwenye kichuguu kushuka chini. Wapambe wa mbunge walikata mipaka ya katani lakini alama zipo.
 
Kibara hospitali karibu kabisa na majengo ya mbunge (Veta) ambayo nimekutumia picha yake. Eneo lenye utata ni kuanzia kwenye kichuguu kushuka chini. Wapambe wa mbunge walikata mipaka ya katani lakini alama zipo.

OK asante kwa kutujuza mkuu
 
Huyo kijana wa UVCCM bado anangoja nini kuendelea kujumuika na majambaka hayo ya CCM !!!? Wakati ni huu aachane na Chuma Chakavu Marufuku[CCM]•

Huyu uvccm anaonekana ni mtiifu sana kwa magamba! Hoja yake ni kunyanyaswa na mh.Mbunge kwa kudhani kwamba kuna mtu anayemtumia kwa kutumia hilo shamba lao kisiasa!

Jionee eneo lao na huyu uvccm Kata ya Kibara! ambalo mbunge analitamani hata kwa kumwaga damu!
 

Attachments

  • 1411414452066.jpg
    1411414452066.jpg
    74.2 KB · Views: 304
Back
Top Bottom