Mbunge wa Musoma kuwasha moto kuhusu milki ya mgodi wa Buhemba

Waungwana huyo Mkono aliyesema atawasha moto Bungeni kuhusiana na umiliki wa mgodi wa Buhemba mbona hatujamsikia?

Bubu
Nasubiri kuona huu moto utakaowashwa huko bungeni,kwa kuwa mkono ameuona huo mgodi wa Meremeta ulioko Buhemba kwa siku nyingi ukinyanyasa wananchi hadi wawekezaji kupiga wananchi risasi za moto na kuhodhi mabwawa ya maji,eti leo anajitutumua bungeni?Tena wale wawekaji(wawekezaji) waliacha hata bila kufukia mashimo.

Serikali isije ikawa inamtumia kuziba ukweli fulani kwa kuwa ndo mbuge wa jimbo hilo kwa zaidi miaka 5.

Kumbuka huu mgodi nao ulikuwa ulaji wa mafisadi
 
hamu yangu apeleke tu hiyo hoja binafsi bungeni.....yalobakia yatamalizwa na wengine.
mwaka huu haufichwi ukweli wowote, mafisadi wanajaribu kujisafisha kwa kuwa wamezila bila hesabu. mwisho unakaribia
 
Mkono kama mwanasheria wa wawekezaji kwenye sekta ya madini tayari ni suspect wa conflict of interest.Kwanza ilitakiwa chochote atakachokisema aki preface na disclosure ya jinsi alivyojimix humo, isije kuwa anatumiwa na wateja wake kuja ku launch crusade na kupata privileged information for his personal gain as well as his clients'.

This is why that ethics bill is so cricial, it is also very important that the bill does not leave any loopholes for slick lawyers like Mkono and their likes.
 
yaleyale ya mtu fulani kwenda ""Msibani na kuanza kusema mie sio fisadi badala ya kutoa rambirambi""....mie sijui itakuaje?? Ila ninachomkubalia kuyu kikofia ni kwamba ""Anaiba kidogo anajengea shule na kusaidia watu kinachobaki mfukoni"" kuliko kina flani ni wabinafsi hata hela za wizi
 
Tatizo la Mkono ni kwamba maji yako shingoni, 2010 inakaribia na hajui kama ataweza kurudi Bungeni kwa hiyo anachofanya sasa hivi ni kujisafisha na kuwaonyesha wananchi wake wa Musoma Vijijini kwamba yeye yuko safi na hana ubia na mafisadi. Pia wakati wa uchaguzi wa CCM aliwasagia sana wagombea wa uongozi wa CCM wa Mkoa wa Mara na kujifanya yeye ni msafi na hatoi rushwa!

Wakati wa kuwadanganya wadanganyika umekwisha na hivyo inabidi atumie hata njia ambayo itamuumbua yeye mwenyewe au kuwaumbua maswahiba wake.

Wote tunajua jinsi Mkono alivyokuwa close na Ballali na Mkapa. Hela za Buhemba zililiwa na wajanja hao hao akina Mkapa na Ballali na wengineo waliokuwa close na hiyo Top Brass ya CCM. Leo hii atakapoomba tume ya kuchunguza Buhemba ni sawa na kutaka kuwaumbua akina Mkapa na wenzake, kitu ambacho kinaweza kuwa na gharama kubwa.

Hawezi kujitenga na ufisadi iwapo baadhi ya shareholders wa Bank M wanatuhumiwa kwa ufisadi. Si ajabu hiyo hela ya Meremeta, Mwanachi, na Buhemba imo kwenye mtaji wa kuanzisha Bank M.

Anachokifanya yeye kwa sasa ni kujiweka kwenye front pages kwa mazuri na kujifanya ni mtetezi wa walalahoi na serikali. Angalia siku akifanya ka-development kadogo kwenye cases ambazo anaiwakilisha serikali nje ya nchi, magazeti yote yanamuweka kwenye front pages.

Kwa hiyo hapo ninaona ni changa la macho na tusubiri njia atakayotumia kuwasha huo moto. Kama akisema iundwe tume teule ya Bunge kuchunguza madudu ya Buhemba nitampa credit, lakini hoja yake ni kulalamika tu hapo sioni la maana atakalokuwa amelifanya bali itakuwa ni kutafuta cheap popularity kwa wananchi wake wa Musoma Vijijini.
 
Mkono kama mwanasheria wa wawekezaji kwenye sekta ya madini tayari ni suspect wa conflict of interest.Kwanza ilitakiwa chochote atakachokisema aki preface na disclosure ya jinsi alivyojimix humo, isije kuwa anatumiwa na wateja wake kuja ku launch crusade na kupata privileged information for his personal gain as well as his clients'.

This is why that ethics bill is so cricial, it is also very important that the bill does not leave any loopholes for slick lawyers like Mkono and their likes.

Mkono anajua kwamba hakuna anaefuatilia au hata kujua misingi ya utawala bora kama hiyo. Huo utamaduni wa kutangaza kwanza mahusiano yako na mtu unaetaka kumuongelea Bongo hakuna.

Ni vigumu sana kwa binadamu wengi kudhibiti tabia zao kwa hiari kama hakuna kichochezi cha nje. Ndio maana hata Papa aliwahi kuwa chipukizi wa Hitler wakati utamaduni wa Ujerumani uliona ni sawa kufungia watu kwenye vyumba vya gesi. Ndio maana watu wengi wanatenda mema kwa sababu tu hawataki kwenda jehanamu.

(Nimechukulia kama ni kweli Mkono anawakilisha hizo kampuni. Najua ni wakili mkubwa, na sio ajabu akawa anawakilisha kila mtu hapa mjini. Lakini ukinipa ka-link kanako onyesha wachimba migodi ni wateja wake nitashukuru.)
 
Back
Top Bottom