Mbunge wa Morogoro na naibu Meya wataka kuzichapa.

Akili Unazo!

JF-Expert Member
Feb 18, 2009
3,930
4,893
Wakuu nimesoma hii habari nikaona kuwa naibu meya alikuwa na haki ya majibu aliyompa mbunge huyo wa morogoro Dr.Mzeru.

Tukio hilo lilitokea walipotembelea miundo mbinu ya mamlaka ya maji ya manispaa ya Morogoro(Morowasa) ili kuona shughuli mbalimbali za mamlaka hiyo.
Sakata hilo lilianza mara baada ya mkurugenzi wa mtendaji wa Moruwasa kutoa maelezo jinsi mamlaka yake inavyottoa huduma ya maji ktk manispaa hiyo,lakini maelezo hayo hayakumridhisha mbunge huyo na kukanusha taarifa za mamlaka kwamba ina uwezo wa kutoa huduma hiyo kwa 95 percent ya maji kwa wakazi wa manispaa hiyo.

Baada ya kukanusha naibu meya wa manispaa ya morogoro akalazimika kuto ufafanuzi kwamba kukosekana kwa maji katika baadhi ya mitaa ya manispaa hiyo ni hali halisi ya uwezo wa mamlaka ya manispaa hiyo na kumtaka mbunge huyo apeleke malalamiko hayo bungeni ili katika bunge la bajeti linaloendelea liweze kumpatia fedha.

''Mheshimiwa mbunge leo(jana) bunge linajadili wizara ya maji na umwagiliaji ingekuwa vyema kama ungekuwa kule badalaya ya kulalamika hapa''

haya yote yalifanyika mbele ya Mkuu wa mkoa.

Wakuu bunge linaendelea na mjadala wa wizara husika halafu mbunge anakuja jimboni kwake kumkolomea naibu meya kuwa hawatowi huduma hiyo kwa kiwango kilichoelezwa.

Hivi Huyu Dr. Mzeru anajua majukumu yake kama mbunge au ndo yaleyale tuliyazoea kusikia kuwa ni kihiyo?

Source.Mwanachi.
 
Hiyo ni jazba na katika kujipanga kuelekea uchaguzi wa 2010.

Dr mzeru namfahamu ni mbunge wa morogoro mjini
 
Nimesoma habari sijaona mahala "walipotaka kuzichapa"
Wangeendelea na majibishano ni wazi wangeishia kuzichapa!
We unacheza na "KULA" za 2010 na jinsi zilivyo karibu!
 
Last edited:
mwe tutasikia mengi ,,mi nangoja pale pinda atakapo taka kuzichapa na mkuu wa kaya .teh teeeeh
 
Back
Top Bottom