Mbunge wa CUF Magg Sakaya na wenzake warudishwa rumande Urambo!

Malafyale

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
13,813
11,126
Wajumbe wanne wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi (CUF), na maofisa wengine saba wa chama hicho akiwemo Mbunge wa Viti Maalum (Tabora), ambaye pia ni Katibu wa Wabunge wa CUF, Magdalena Sakaya, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Urambo mkoani Tabora kwa shtaka la kufanya mkutano bila kibali.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Liberatus Barlow, aliliambia NIPASHE jana kuwa walifikishwa mahakamani hapo jana asubuhi chini ya ulinzi mkali wa polisi na kusomewa mashtaka ya kumshambulia mpelelezi, kutojitambulisha kwa makusudi kwa askari polisi na kwenda kuchukua mifugo ambayo inashikiliwa na polisi.

Kamanda Barlow alisema walifikishwa mbele ya Hakimu Oscar Burugu wa mahakama hiyo, baada ya kusomewa mashtaka walinyimwa dhamana.

Alisema mahakama hiyo ilikataa dhamana yao kwa kuhofia kuvunjika kwa amani kwani wangeweza kwenda kuhamasisha wananchi kwenda kuchukua mifugo ambayo bado inashikiliwa na polisi.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro, alisema mahakama hiyo imewanyima dhamana ikidai kuwa iwapo wataachiwa amani inaweza kuvurugika.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 6, mwaka huu na washtakiwa wote walirudishwa rumande.

Wajumbe hao wa Baraza Kuu waliofikishwa mahakamani na kunyimwa dhamana pamoja na mbunge huyo, ni Doyo Hassan, Yassin Mrotwa, Zainabu Nyumba na Masoud Omar.

Wengine ni Ofisa Haki za Binadamu na Sheria Makao Makuu ya CUF, Hashim Bakari na aliyekuwa mgombea ubunge kupitia chama hicho Jimbo la Urambo Magharibi, Kirungi Kirungi.

MY NOTE:Niliwahi kumsikia Mwenyekiti wa CUF Prof Lipumba akisema kuwa CHADEMA kukamatwa kwao Arusha ilikuwa halali maana ni CHADEMA ni chama cha vurugu na kutotii sheria za nchi;sasa kwa kukamatwa kwa Mbunge wao na watendaji wa ngazi za juu wa CUF bado Lipumba atazidi kusema kuwa CHADEMA hawafuati sheria au sasa atajirudi na kugundua kuwa serikali ya CCM imeshindwa kutawala na sasa inadumu kwa nguvu za dola tu?
 
CUF na CCM lao moja hapa wanajaribi kuficha madhambi ya Tarime ili kuwavuruga watu wasichambue uozo wa Tarime.Lengo lao ni kutaka kuzimisha moto wa CDM.Maandamano nchi nzima ni mziki mdogo inahitaji kujituma haswa hawa CUF HAWANA MOLARI wa kufanya hivyo watachemsha kwani wanajua hawataungwa mkono
 
Wajumbe wanne wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi (CUF), na maofisa wengine saba wa chama hicho akiwemo Mbunge wa Viti Maalum (Tabora), ambaye pia ni Katibu wa Wabunge wa CUF, Magdalena Sakaya, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Urambo mkoani Tabora kwa shtaka la kufanya mkutano bila kibali.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Liberatus Barlow, aliliambia NIPASHE jana kuwa walifikishwa mahakamani hapo jana asubuhi chini ya ulinzi mkali wa polisi na kusomewa mashtaka ya kumshambulia mpelelezi, kutojitambulisha kwa makusudi kwa askari polisi na kwenda kuchukua mifugo ambayo inashikiliwa na polisi.

Kamanda Barlow alisema walifikishwa mbele ya Hakimu Oscar Burugu wa mahakama hiyo, baada ya kusomewa mashtaka walinyimwa dhamana.

Alisema mahakama hiyo ilikataa dhamana yao kwa kuhofia kuvunjika kwa amani kwani wangeweza kwenda kuhamasisha wananchi kwenda kuchukua mifugo ambayo bado inashikiliwa na polisi.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro, alisema mahakama hiyo imewanyima dhamana ikidai kuwa iwapo wataachiwa amani inaweza kuvurugika.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 6, mwaka huu na washtakiwa wote walirudishwa rumande.

Wajumbe hao wa Baraza Kuu waliofikishwa mahakamani na kunyimwa dhamana pamoja na mbunge huyo, ni Doyo Hassan, Yassin Mrotwa, Zainabu Nyumba na Masoud Omar.

Wengine ni Ofisa Haki za Binadamu na Sheria Makao Makuu ya CUF, Hashim Bakari na aliyekuwa mgombea ubunge kupitia chama hicho Jimbo la Urambo Magharibi, Kirungi Kirungi.

MY NOTE:Niliwahi kumsikia Mwenyekiti wa CUF Prof Lipumba akisema kuwa CHADEMA kukamatwa kwao Arusha ilikuwa halali maana ni CHADEMA ni chama cha vurugu na kutotii sheria za nchi;sasa kwa kukamatwa kwa Mbunge wao na watendaji wa ngazi za juu wa CUF bado Lipumba atazidi kusema kuwa CHADEMA hawafuati sheria au sasa atajirudi na kugundua kuwa serikali ya CCM imeshindwa kutawala na sasa inadumu kwa nguvu za dola tu?

Malafyale, naomba sina hii issue ya kunyimwa dhamana au mtu kupelekwa mahakamani isiwe CHADEMALISED. Tuichukulie seriously kwamba polisi hawasimamii usalama wa raia kama nembo yao inavyoonyesha bali ni usalama wa watawala.

Na mahakama kwa upande wake haisimamii misingi ya haki na matakwa ya sheria, bali matakwa ya upande wa utawala.

Tukemee na tupige kelele kwa nguvu zote hii kitu. Makosa ambayo dhamana inakatazwa yanajulikana wazi, ikifika mahali watu wananyimwa dhamana kwa ajili ya kukutana, uhuru wetu ambao ulitafutwa na waasisi wa nchii uko wapi?????
 
Hivi hiyo bange unayovuta mkuu imelimwa wapi vile ?
 
Kwenye katiba na vitabu vya sheria.

Kama unaona hiyo ni bange ( whatever it means) pole sana. Utaendelea kushangaa hadi itafika siku na wewe unyimwe dhamana ndo utashangaa na kulia mdomo juu ukikumbuka maandiko yangu.
 
Ni kitu cha kushangaza kuwa sijasikia viongozi wa ccm kukamatwa kwa kufanya mikutano bila vibali. Hivi hivyo vibali kwao ni automatic, au ndio wao wanajua kufuata sheria sana? I am just curious!
 
Huwa nashindwa kuelewa, maana mara kwa mara utasikia Chama fulani cha upinzani kimefanyiwa, hivi mara vile. Nadhani wapinzani na Serikali iliyo madarakani hawakujiandaa, kufahamu upinzani ni nini; na jinsi ya kuongoza katika zama za upinzani. Na hii imesababisha kuwepo na migongano ya hapa na pale maana Serikali ilikuwa na mazoea ya kuongoza wakti wa chama kimoja na wapinzani wanadhani upinzani ni kuhoji kila kitu.
 
Ni kitu cha kushangaza kuwa sijasikia viongozi wa ccm kukamatwa kwa kufanya mikutano bila vibali. Hivi hivyo vibali kwao ni automatic, au ndio wao wanajua kufuata sheria sana? I am just curious!

Kuna OCD alipigwa na mgombea wa CCm wakati wa uchaguzi kesi imefunikwa blanketi mpaka sasa imesahaulika.

Kuna mbunge alikamatwa na masanduku ya kuru nje ya kituo cha kuhesabia taarifa ikapelekwa polisi, wameiatamia mpaka leo hakuna vifaranga wala mayai visa.

Nchi inasikitisha sana hii,
 
Back
Top Bottom