MovingForward
JF-Expert Member
- Nov 10, 2009
- 489
- 49
Sipendi na ninapinga mawazo ya wabunge kujimirikisha majimbo utadhani wameyazaa wao.
Mbunge anaposema kuna watu wanazunguka zunguka katika jimbo langu, ni upuuzi!. Anatakiwa aseme kuna watu wanazunguka katika jimbo la wananchi wa MFULUKUTO!. Wanaposema jimbo langu, wanawapiga vita ya kisaikolojia watu wengine wanaotaka kugombea ubunge wawe na uoga kna kwamba wao ndiyo wanakubalika na wananchi!.
Unasema jimbo lako; umelizaa? Mke wako alibeba mimba ya miezi tisa kulizaa jimbo la wananchi!. Acheni lugha za kuwanyanyasa wananchi. Hii ni dharau! Hivi jimbo unaloliwakilisha kama Mbunge unaweza kusema ni la kwako!!. Mbunge ni mwakilishi wa wananchi, kwa lugha nyingine ni kama mshenga au agent, ambaye amepewa dhamana ya kufanya uwakilishi wa jimbo la wananchi, akiwepo na yeye mwenyewe. Ndiyo, si ni mwananchi naye wa eneo analoliwakilisha?.
Sasa, tunapompatia dhamana ya uwakilishi, kisha anatugeuka anaanza kusema hili ni jimbo lake, anataka kutuambia ametuzaa na kuwazaa wananchi? Ndiyo, ni lugha iliyozoeleka kusema Mh Mbunge wa MFULUKUTO, yaani mwakilishi wa jimbo hlo, lakini si kusema jimbo langu. Ni afadhali wangekuwa wanasema jimbo letu la MFULUKUTO!. Wanaanza ubinafsi hata katika namna ya kujitambulisha!. Wanapiga vita ya kisaikolojia. tangu lini Mkurugenzi wa Kampuni akajimilikisha kampuni badala ya wanahisa?
Mh Spika (Sitta), naamini utakuwa unapitia pitia mtandao huu wa JF, ninakuomba hivi: KATIKA BUNGE LIJALO, NINAKUOMBA UTUMIE KALE KA MUDA AMBAKO HUWA UNAKATUMIA KUWACHEKESHA WAHESHIMIWA WABUNGE, K.M UNAPOSEMA POLENI WATANI WETU WA YANGA KWA KICHAPO CHA JANA, KUWAELIMISHA WAHESHIMIWA HAO NAMNA NZURI YA KUJIELEZA WANAPOTAKA KUJITAMBULISHA, WASIWE WANAPIGA VITA YA KISAIKOLOJIA, WANAPOCHANGIA MISWADA BUNGENI AU MAHALI PENGINE. NI KISWAHILI TU CHENYE MANTIKI, KUTOKUSEMA JIMBO LANGU!!!.
TUAMKE!.