Mbunge mstaafu, Abdul Mteketa alia mtandaoni akiomba msaada wa matibabu kutoka kwa Rais Magufuli

Mutu imepingwa risasi inaombwa saidia rais anakatala, lakini huyu papa maarufu ya kutuza watu kushoo za live bendi anahudumiwa na kodi za maraiaa, ina maanisha mbunge mustafu hana kubima ya afya, au bima yake iko na sawa na hizi zetu za wakulima
 
Sumaye alilazwa akapona pale, mama Janet magufuli, heche,mama mtanzania na wengine wengi.
Unajuaje labda walikuwa na wageni wengi huko kwao?!
Kama hao walikuwa wanaumwa kweli nasikitika kwanini shilawadu hawakusema mapema wangepelekwa india kutibiwa.
 
Mutu imepingwa risasi inaombwa saidia rais anakatala, lakini huyu papa maarufu ya kutuza watu kushoo za live bendi anahudumiwa na kodi za maraiaa, ina maanisha mbunge mustafu hana kubima ya afya, au bima yake iko na sawa na hizi zetu za wakulima
Bima za matibabu za wabunge ni miaka mitano
 
Tena alimdhurumu dada yangu kabisa huyu pedeshee angekufa tu
Kabla ya JPM mtandao wao ulikuwa mkubwa, hata uende wapi hupati sheria, haina tofauti kama ya yule mama aliyepoteza title 2 kwa mmiliki wa "Galaxy", huyu kina Katunzi, Papa Msofe, Ndama, Masawe, marehemu Khamis faraji n.k. ilikuwa nchi yao, kweli aliye juu msubiri chini, wameliza magari na majumba ya watu kinoma noma, makatili sana hawa..
 
Awamu ya tatu ya mh. Mkapa alijaribu kuwapa nafasi za uwekezaji wale waliolitumikia taifa hili lakini hata hivyo awamu zilizofuata zikashindwa kujenga mazingira bora zaidi.
Chini ya CCM nchi hii haitakuja kupata mafanikio kwa kuwa wanachoangalia CCM na serikali yake ni kushinda uchaguzi tu.
Kinachofanyika ni kukomoana na kurudishana nyuma. Hii ni ili kuhakikisha kuwa kila anayeingia madarakani anatengeneza mfumo wake wa kiuchumi huku akijaua kiwa yeye hatashitakiwa kamwe.
Haiwezekana mbunge awe na maisha magumu hivyo. Ni sera mbovu kabisa za kutowajali wananchi.
CCM wenyewe kwa wenyewe na watanzania wengine wanaoneana wivu na kukomoana ili tu kumalizana kisiasa.

Bila CCM kufa kifo cha kisiasa na watu kukaa meza moja na kuweka dira ya nchi kwa pamoja nchi hii haiwezi kustawi.
Tujiulize inakuwa Zanzibar yenye watu wasiozidi mil.2 iwe nchi maekini chini ya CCM?
Jibu ni kwamba CCM ndio mhimili wa umaskini,maradhi na ujinga. Haya ndiyo mtaji wa CCM na ndio hirizi yake ya ushindi.

Fikiri CCM wanawaza kabisa kuwafilisi watu waliolitumikia taifa hili na chama cha mapinduzi kwa miaka zaidi ya 40 ili tu wapate furaha kuona wakiwa ombaomba kwa mh. Rais. Watu waliofikia mpaka level ya iwaziri mkuu. Leo unashangaa wakimiliki shamba hekari 200.

Tumuombe sana Mwenyezi Mungu atuinulie waonaji katika taifa hili.
 
Anamwomba rais pesa zetu. Hatuna pesa tulishaziweka kwenye budget tunatekeleza budget. Labda anamwomba pesa toka mshahara wake.
 
Leo kwenye pitapita zangu mtandaoni nimekutana na video ya mbunge mstaafu wa Kilombero mh Abdul Mtegeta akimuomba Mh president msaada wa matibabu, imekuwa jambo la kawaida sasa au fashion watu maarufu wenye vipato kulialia mtandaoni wakiomba msaada.

Hivi najiuliza kipindi wakiwa kwenye form walishindwa fanya serving au kuwekeza kijiutega uchumi hata banda la kuuza samaki?

Basi hata bima ya afya imewashinda kukataa 1.2m sijui per year hata mimi nisiye na ajira maalumu na mudu?

=====

MBUNGE mstaafu wa Kilombero (CCM), Abdul Mteketa, ambaye aliomba msaada wa matibabu ya upasuaji wa magoti kwa Rais John Magufuli kupitia mitandoa ya kijamii, amesafirishwa kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kutibiwa.

Jumamosi iliyopita, Mteketa alirekodi ujumbe wa video na kuuweka kwenye mitandao ya kijamii akimwomba Rais Magufuli amsaidie matibabu kwani hali yake kiuchumi ni mbaya.

Mteketa aliyetumikia jimbo la Kilombero kwa miaka mitano baada ya kushinda katika Uchaguzi Mkuu wa 2010, alishindwa kwenye mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM kwa ajili ya kutetea kiti hicho 2015.

Katika ujumbe wa video alioutuma Jumamosi, Mbunge huyo mstaafu alimweleza Rais Magufuli kuwa hali yake ya kiafya ni mbaya na kwamba amekuwa akibebwa kwenda maliwatoni na kuogeshwa.

"Mheshimiwa Rais John Magufuli, mimi ni Abdul Mteketa, Mbunge mstaafu wa Kilombero nipo hapa mbele yako kwa sababu nimejitahidi miaka yote kukufikia lakini nimeshindwa tangu uingie madarakani," alisema na kueleza zaidi:

"Hali yangu kiafya ni mbaya kama unavyoniona, nabebwa kwenda chooni, naogeshwa, kila kitu nategemea msaada wa mtu. Nimejitibu kwa mwaka mzima sasa lakini bila mafanikio.

"Nimeenda kwa madaktari wameniambia tatizo ni magoti, kwanza nimeumwa mguu huu madonda kila sehemu yamepona, magoti yangu yanatakiwa kufanyiwa upasuaji."

Siku iliyofuata, Mteketa aliweka tena ujumbe mwingine wakati akiwa kwenye gari la kubeba wagonjwa baada ya Rais Magufuli kumsaidia ambamo anamshukuru kiongozi huyo wa taifa.

Mteketa anasema katika ujumbe huo kuwa baada ya Rais Magufuli kuona ujumbe wake wa video aliyoituma kwenye mitandao ya kijamii Jumamosi, alichukua hatua ya kumsaidia.

"Jana (Jumamosi) nilituma ujumbe wa video ya hali yangu kuwa mbaya, niliyompelekea Rais, alipoiona leo (Jumapili) amechukua hatua; amenitumia gari la wagonjwa ambalo sasa hivi nipo ndani napelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili," anasema.

"Nakushukuru sana Rais, Chama cha Mapinduzi CCM na Watanzania waliopeleka ujumbe wa video yangu mpaka zimemfikia Rais. Naomba mniombee."
Tanzania ina mafukara wengi,wenye hari mbaya kuliko hata huyo mheshimiwa,
Kusaidiwa huyo mbunge,haimaniishi mafukara wa nchi hii wamepata nafuu!!,La hasha!!!
Serikali iweke mifumo,ambayo itasaidia wastaafu na wananchi kwa jumla kuishi maisha mazuri,pale wanapofikia umri mkubwa
 
SIPATI PICHA NENDENI HOSPITAL YA OCEAN NDO MTAJUA KUWA FEDHA ZINATAKIWA KUPELEKWA KULE..HIVI KIPI BORA KUOKOA MAISHA YA MTU MMOJA AU WATU WENGI?
 
Bibi yangu amestafu uwalimu mwaka 1990 ila mpaka leo pesa ya kula matibabu hategemei mtu ukitaka kumpa Ni kwa hisani yako yupo fit balaa..Sasa huyu kastafu mafao zaidi ya 300m juzi tu hapo analialia huu Ni upuzi wa kiwango Cha Masters
mbona viongozi wengi hulia tu hawana fedha ili hali walikuwa na mafao makubwa tu.Kuna mkuu mmoja wa wilaya ya kinondoni naye aliwahi kulia asaidiwe matibabu.Ni ajabu viongozi kama hawa kulialia wasaidiwe matibabu wakati inajulikana walikuwa watumishi Wa super scale salary
 
Hii inaweza kuwa fundisho kwetu sote. Ila kwa waliopo mjengoni ni nzuri kufikiria miswada inayopitishwa inatakiwa kuwa yenye masilahi mapana ya taifa.
 
Back
Top Bottom