Mbunge Martha Mlata azuiwa JKNIA kusafiri, hakuwa na kibali cha Ikulu

Nafikiri mbunge analipwa kutokana na bajeti ya serikali, sasa sijui huyu martha alikuwa anaenda kuomba ela kwa wafadhili au shopping ?
 
Kama hujui kitu bora kuuliza.aliyekwambia mbunge si mtumishi wa umma nani? Kwa hiyo anamtumikia nani sasa?
Sasa ni dhahiri hujui Utumishi wa Umma. Kwa hiyo kumbe serikali ikisema imeongeza ajira kwa watumishi wa umma, huwa unahesabu na wabunge pia?
 
Huyu mbunge alikuwa anaenda kwa hawara yake huko nje kwa kodi zetu?
Kodi ilikuwa yetu kabla hajafanya kazi, akishafanya kazi akalipwa mshahara, sio kodi yetu tena bali ni hela yake halali.
 
Huu ni uonevu, umbumbumbu wa sheiria na ujuha tuu!, mbunge sio mtumishi wa serikali, ni mtumishi wa watu!.

Pasco
Labda swali ni hili Huyu unaemuita mtumishi wa watu analipwa pesa zipi??? Kwa nijuavyo ni kuwa Bunge linatengewa pesa na Serikali... So kama wabunge wanalipwa na Serikali then wana fall in the same category... Hakuna Kusafiri mpaka Kibali kitoke IKULU.... Kwani hivyo Vibali havitoki??? SAFI SAAANA JPM
 
Mi nadhani hapa tatizo sio mbunge ni mtumishi au la! Nadhani tatizo ni hela za kuendeshea bunge na safari za bunge ni za nani? Kama ni za serikali basi hapo Inawezekana Rais akazuia safari za wabunge ili kupunguza gharama za serikali. Lakini kama mtu ana safari zake binafsi sidhani kama hii marufuku ya Magufuli itakuwa inamuhusu.
 
..kila mhimili udhibiti watu wake.

..safari za wabunge ziidhinishwe na katibu wa bunge.

..mawaziri wapate kibali cha waziri mkuu.

..safari za watumishi wa serikali ziidhinishwe na katibu mkuu kiongozi.

..pia haiwezekani mtumishi wa serikali asafiri bila katibu mkuu wa wizara kufahamu. kwasababu masuala ya ununuzi wa ticket, posho, etc yote gharama zake huidhinishwa na makatibu wakuu.

..hata huyo Mbunge Mlata kama alikuwa anasafiri kwa shughuli za kibunge, basi Katibu wa bunge lazima atakuwa anafahamu, na ameidhinisha gharama za safari hiyo. Vinginevyo labda Mama Mlata ameamua kufanya "kazi ya kanisa."

cc Pasco, Richard
wabunge shughuli zao ni kwenye majimbo sio nje ya nchi
 
hilo agizo haliwahusu wabunge wanaosafir kwa shughuli zao binafsi labda kama safar yake inalipiwa na serikali.

Mbunge si mtumishi wa umma
Vijana wa siku hizi kwa kuchanganya mambo! mbunge ni mtumishi wa umma ila siyo civil servant
 
vyovyote iwavyo bunge ni mhimili mwingine.ruhusa inatokaje himili mwingine(rais)?mngesema ruhusa ya ndugai ningeelewa.Tusije kushangaa hawa watu badae wakiiburuza serikali bungeni au hata mahakamani kwa maaumuzi yake kukurupuka!!
 
Wabunge na maofisa wa serikali. NJIA MBADALA

Pitieni Uwanja wa kimataifa wa Zanzibar kwa kusafiria hamtaulizwa kibali. Chukua boti fika Zanzibar chukua tiketi yako utakwenda kokote. Usikibali kuwa mfungwa, kuwa huru
 
wabunge shughuli zao ni kwenye majimbo sio nje ya nchi

..hilo halina mjadala.

..hoja yangu ni kwamba masuala ya wabunge yashughulikiwe na Spika na Katibu wa Bunge.

..nadhani ni makosa kuwalazimisha wabunge wapate vibali vya safari toka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.

..pia masuala ya watumishi wa serikali yashughulikiwe na Raisi, Waziri Mkuu, na Katibu Mkuu Kiongozi.
 
Wabunge na maofisa wa serikali. NJIA MBADALA

Pitieni Uwanja wa kimataifa wa Zanzibar kwa kusafiria hamtaulizwa kibali. Chukua boti fika Zanzibar chukua tiketi yako utakwenda kokote. Usikibali kuwa mfungwa, kuwa huru
Ok, unaweza pitia znz kwenda abroad, lakini Pombe akigundua huwa haundi tume, ni action papo kwa papo.
 
..hilo halina mjadala.

..hoja yangu ni kwamba masuala ya wabunge yashughulikiwe na Spika na Katibu wa Bunge.

..nadhani ni makosa kuwalazimisha wabunge wapate vibali vya safari toka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.

..pia masuala ya watumishi wa serikali yashughulikiwe na Raisi, Waziri Mkuu, na Katibu Mkuu Kiongozi.
hizo sio sera za CCM!
 
Duh!
Hii LOCKDOWN ni hatari sasa! Hadi wabunge?Mi nilidhani ni kwa waajiriwa wa serikalini tu! Kubenea alikuwa na mpango wa kusafiri lini? Nitaenda JKNIA nikaone anavyopigwa stop!
 
Back
Top Bottom