Mbunge Lema akamatwa na Polisi!

HIVI Mulongo ana akili ndogo namna hiyo? Mbona kumkomoa mtu kwa kumweka rumande ni mambo ya kizamani na ushamba? Lema atatoka na hapo amempandisha chati na tunajua hiyo kesi ni nyepesi atashinda kwa sababu aliyeleta vurugu ni Mkuu wa mkoa na Mungu atashughulika naye.
 
Taarifa za sasa kutoka Arusha ni kwamba Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi Arusha na kuhojiwa kwa tuhuma za uchochezi wa vurugu za Wanafunzi wa chuo cha Uhasibu dhidi ya Mkuu wa Mkoa Arusha juzi.

Taarifa za uhakika kutoka kwa mke wa Mh. Lema sasa hivi ni kwamba Polisi wamekataa kutoa dhamana yake na kusema mpaka jumatatu ndio itajulikana.

Namkariri Mke wa Lema akiongea na TheTZA millardayo.com akisema “jana usiku saa sita kasoro watu walikuja kugonga nyumbani kwetu tukamtuma kijana aende kutazama ni kina nani, aliporudi akasema ni Polisi.. sisi hatukuamini na tulikataa kwa sababu hatukujua kama ni Polisi kweli au ni watu wanataka kuitumia hiyo nafasi kufanya uhalifu, mimi nimeshinda Polisi kutwa nikifatilia gari mbona chochote hakikutokea?”

“Baada ya muda kusogea ikabidi Lema aanze kuwapigia marafiki, jamaa na baadhi ya viongozi wa Chadema, kabla ya hapo pia tuliamua kupiga kengele ya kampuni ya security ambao muda mfupi baadae walikuja na gari yao huku Polisi wakiendelea na vitisho kwamba watapiga mabomu na kuvunja ukuta la sivyo Lema ajisalimishe, Viongozi wa Chadema na marafiki walipowasili wakamshauri Lema ndio akajitokeza wakati huo ni saa tisa usiku” – Mama Lema


“Alipojitokeza Polisi walimchukua na mimi nikaondoka nao, tulipofika kituoni walimtaka Lema kutoa maelezo lakini alikataa na kusema mpaka mwanasheria wake aje hivyo akapelekwa rumande, asubuhi tulipoamka na kuanza kufatilia.. R.C.O alisema yuko kwenye kikao na haongei na yeyote isipokua Mwanasheria wa Lema, walipomaliza kikao saa nane maelezo yakaanza kutolewa huku Mwanasheria akiwepo na kazi ikamalizika jioni saa 11 ambapo Polisi wamekataa kutoa dhamana mpaka Jumatatu” – Mama Lema

“shitaka kubwa lililo mbele yake ni uchochezi na kauli ambayo anadaiwa Lema kuitoa mbele ya Wanachuo cha Uhasibu kwamba dhambi kubwa kuliko zote ni uoga, na hata leo kwenye maelezo Lema amewaambia watu wa Arusha mjini hivyohivyo, kwamba dhambi kubwa kuliko zote ni uoga” – Mama Lema

Kwa kumalizia, Mke wa Mbunge Lema amesema “gari letu lililokua linashikiliwa na Polisi tumerudishiwa baada ya kutakiwa kulipia elfu 50 ya wale waliolivuta, gari liko zima kabisa………… toka nimeolewa na Lema nimeshuhudia akienda polisi zaidi ya mara 20, mara yake ya kwanza kushuhudia anapelekwa polisi ni wakati wa kampeni za Ubung
Hapo mama lema kweli huna mume. Nakushauri usijiingize kwenye huo mchezo wa mumeo maana kule jela hakufai. Kuna wanaume wana miaka kibao hawajui wake.
 
HIVI Mulongo ana akili ndogo namna hiyo? Mbona kumkomoa mtu kwa kumweka rumande ni mambo ya kizamani na ushamba? Lema atatoka na hapo amempandisha chati na tunajua hiyo kesi ni nyepesi atashinda kwa sababu aliyeleta vurugu ni Mkuu wa mkoa na Mungu atashughulika naye.
Umeambiwa kuwa kilichompeleka lema lumande ni maneno yake ya uchochezi. Hapo mulongo anainiaje?
 
ndugu AKA2030
umejiunga juzi tu Join Date : 5th January 2013
Posts : 233
Rep Power : 432
Likes Received36
Likes Given0
mleta mada ni wa tangu 2007 maribu miaka kumi
kama huna cha kuchangia bora ukae kimya au kwa vile umeahidiwa unapojibu post
ndivo utakavolipwa Lumumba? ok kachukue mshiko wao
sheria za JF soma vizuri usiwe na mdomo refu kama mbayuwayu.
Mtoa mada asante kwa taarifa

Huyu jamaa anakela sanaa, yani kuna huyu na Bungeni kuna umuhimu sana ya kuwaanika hawa ili heshima ya JF iendele milele kwani wanafananisha humu na FB.....
 
Hamna kesi hapo!

Hiyo kauli inatafsiriwa vipi?

Mbona haina cha ajabu na cha kutisha bali inafundisha ujasiri wa kudai haki!

Mahakamini wataishia kuumbuka!

Lakini lengo inawezekana ni kumkomoa tu.

Hawana nia na kesi bali wana lengo la kutisha na kukatisha tamaa wapinzani!

Wanafungua kesi kutimiza mashariti ya kisheria tu!
 
WEWE, BUNGENI, MAUDODO, AKA2030 na wengineo
njaaa zenu zitawaumbua.acheni unafiki humu
ulichoandika ni sawa na kuwatukana wapiga kura wake
tuwe wastaarabu humu mmejiunga juzi bado wageni mnaandika upuuzi humu.
anzisheni forum yenu Facebook
hili jukwaa linasomwa na watu wenye heshima zao
UOTE=Atongwele;6225144]Domo la lema linanuka maneno machafu[/QUOTE]
 
inasikitisha sana, tz tuna watawala madikteta
Ndio ila udikteta wa kishamba sana. Kwani polisi walipeleleza wakagundua ana makosa gani? Au ni kiasi tu cha mkuu wa mkoa kuamua kamata fulani weka ndani? Mtu mmoja anawatishia nyau watu milioni?
 
kuna mzee mmoja mwanajeshi mstaafu alikuwa studio za chanel ten asubuhi nilimpenda sana kwani anaijua dunia hii vibaya na alisema ukiona serikali inatumia mabavu ujue mwisho umefika.

haya ya lema kama ni siku ni saa kumi alfajiri.

Mkuu ni kweli haswa JK anapoteua vilaza kama mulongo kuwa wawakilishi akifikiri anarudisha hadhi ya Chama. Hapa Ar mulongo amelikoroga na amiharibia CCM kabisa.
 
Hamna kesi hapo!

Hiyo kauli inatafsiriwa vipi?

Mbona haina cha ajabu na cha kutisha bali inafundisha ujasiri wa kudai haki!

Mahakamini wataishia kuumbuka!

Lakini lengo inawezekana ni kumkomoa tu.

Hawana nia na kesi bali wana lengo la kutisha na kukatisha tamaa wapinzani!

Wanafungua kesi kutimiza mashariti ya kisheria tu!

hawawezi kukubali arudi bungeni kwani kule atamwaibisha babake ma riz ile issue ya udini.na wanaweza hata kumpa sumu..
 
Hapo mama lema kweli huna mume. Nakushauri usijiingize kwenye huo mchezo wa mumeo maana kule jela hakufai. Kuna wanaume wana miaka kibao hawajui wake.

Wewe nawe ulishakwenda wakakuondolea uwanaume au? Maana unaongea kwa uhakika kana kwamba na wewe ni muathirika. Kama ulikwenda kule wakakutenda ni tamaa zako za kupenda vya kupewa ila kwa watu ngangari kama Kamanda Lema sio mtu wa kujilegeza mpaka atendwe kama wewe. Mama Lema should be proud of her valiant husband
 
Hamna kesi hapo!

Hiyo kauli inatafsiriwa vipi?

Mbona haina cha ajabu na cha kutisha bali inafundisha ujasiri wa kudai haki!

Mahakamini wataishia kuumbuka!

Lakini lengo inawezekana ni kumkomoa tu.

Hawana nia na kesi bali wana lengo la kutisha na kukatisha tamaa wapinzani!

Wanafungua kesi kutimiza mashariti ya kisheria tu!

hawawezi kukubali arudi bungeni kwani kule atamwaibisha babake ma riz ile issue ya udini.na wanaweza hata kumpa sumu..
 
Umeambiwa kuwa kilichompeleka lema lumande ni maneno yake ya uchochezi. Hapo mulongo anainiaje?
Mimi niko hapa na ninaelewa bifu yake na Mulongo na ukitaka kujua amembambikizia kesi ili amwaibishe soma kesi inayompeleka mahakamani. Wewe elewa Mulongo alishangilia Lema alipovuliwa ubunge na ushahidi tunao. You're not informed tuulize sisi acha KUTUMIKA
 
kuna comment nimeisoma hapa,. ya "kibanga ampiga mkoloni"

lakini Ng. Kibanga (kama naweza kuku address namna hiyo)
Unaweza kulitazama hili kwa jicho negative nakuona ni Bw. Lema alie na "uhalifu" sana kiasi chakupelekwa polisi mara 20 kama ulivyo amua kufanya, au unaweza kuchagua kuwa critical thinker nakugundua kutoka kwenye historia kwamba yeyote anaye chagua kusimamia haki na hasa haki ya watu wasio na sauti, watu ambao vinginevyo wangekua wakudharuliwa, Alafu akaenda mbali zaidi nakuwafundisha watu hao kutokuogopa., akawaongoza watu akisimama mbele yao na si nyuma yao, akiwaambia follow me let's go! nasio what are you waiting for go! go! go! ungefahamu kuwa mtu huyo huwa adui wa utawala uliozoea kuogopwa, kutetemekewa, kutokukosolewa, utawala uliozoea wasomi wenye nidhamu za uwoga., watu waliojaa malalamiko kinyume cha utawala miyoyoni lakini sifa za utawala huo huo midomoni.., kwa vyovyote mtu huyo mwanamapinduzi atakuwa adui wa utawala huo.

haya ndiyo maisha ya mtu aliye amuakupigania situ haki yake na mke wake na familia yake, bali jamii yake na hata taifa lake kwa ujumla wake.
haya ndiyo maisha ya mwanamapinduzi.,

nitakuhakikishia kitu kimoja hapa. kwamba kamanda Lema hakutegemea itakua vinginevyo! alipoa amua kupigania haki, na kuzipigania rasilimali za taifa hili,. alifahamu na kuyategemeaa haya yote!

kwa mama Lema, naomba kuchukua fursa hii kukutia moyo mama., wewe ni kiongozi shupavu alongside our very own Kamanda Lema usikate tamaa., hawa ni wepeesi na weupe saana (kama anavypenda kusema mh. Lema)!

Mama Winfred Mandela Mke wa comrade Nelson Mandela aliwahi kusema alipo ulizwa na waandishi wa habari katika kipindi kilichokuwa kigumu sana kwake baada ya Nelson kuwa muhudhuriaji mzuri katika mahakama zakibaguzi za S.africa (kama ilivyo leo kwa Lema) na Nelson akapewa vifungo vingi hadi vingine ku overlap,.yani anatolewa gerezani nakupelekwa mahakamani tena asomewe mashtaka mengine mapya alafu anahukumiwa kifungo kingine kipya,. yaani kifungo juu ya kifungo. achilia mbali vitendo vya uvamizi vilivyo fanywa na polisi maranyingi nyumbani kwa Bw. Mandela na BANs alizokua akipewa sio yeyetu lakini hata mke wake na udhalilishaji wa familia yake mara nyingi.,

Lakini mama Mandela akasema "when i married Mandela, i knew i had married the Struggle and i have never regretted this"

Stoic Up mama Lema.

Mzani wahaki umeegeme Upande wetu,. (the balance of Justice has tilted in our favor)
haya yote hayata kuwa bure.

comrades,.
 
Back
Top Bottom