Mbunge Jafari Chege Wambura aendelea na ziara Jimboni Rorya

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945
"Naomba Mbunge utusaidie kujenga nyumba za Walimu, Walimu wako tunakaa kwenye nyumba ambazo zimejengwa mwaka 1979, nyumba zetu hazina siri, tunashindwa kuwa na faragha na familia zetu, naomba Mheshimiwa Mbunge ulione hilo" - Mwalimu, Kata ya Mirare Jimbo la Rorya

"Lakini pia upande wa wanafunzi wangu madarasa wanayosomea siyo rafiki" - Mwalimu, Kata ya Mirare, Jimbo la Rorya akitoa maoni yake mbele ya Mbunge wa Rorya, Jafari Chege Wambura alipofanya ziara katika Kata ya Mirare

"Malalamiko yangu yanaenda kwenye madarasa, ni mabovu, mbu mchana kutwa, mbu wanaishi Madarasani. Nyumba za Walimu mabati yameharibika na Vyoo vya Walimu na wanafunzi vimeharibika" - Mwanafunzi, Kata ya Mirare Jimbo la Rorya

"Toka tarehe 13 Aprili, 2023 Shule ya Msingi Kilango iliezuliwa na upepo na watoto wanarundikwa kwenye darasa moja tu. Shule ya Sekondari Mirare hakuna Mwalimu wa kike watoto wanapofika kwenye siku zao wanapata shida" - Mwananchi, Kata ya Mirare Jimbo la Rorya

"Shule ya Sekondari Mirare hakuna choo, kuna choo yenye matundu matano tu na watoto katika shule hiyo ni 725" - Maoni ya Mwananchi wakati wa ziara ya Mbunge wa Jimbo la Rorya, Mhe. Jafari Chege Wambura

Mhe. Jafari Chege Wambura amesema amezichukua changamoto zote na kuzifanyia kazi huku akiahidi fedha za Mfuko wa Jimbo zitatumika kufanya marekebisho ya shule zote zilizotajwa na kumuomba Mkuu wa Wilaya Rorya kushughulikia suala la shule ambayo haina Mwalimu wa kike.

"Hatuoni sababu kwanini watu wa Mirare mnalalamika, mnalia na changamoto ya Maji pamoja na bomba kupita hapa. Baada ya Mkutano huu tumekubaliana Baada ya ziara yangu kutembelea maeneo yote tutakaa na watu wa RUWASA, tutahakikisha tunamuelekeza afanye utafiti ili wananchi wa eneo hili muweze kupata Maji" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya.


 
Back
Top Bottom