Mbunge Edward Lekaita Aisisitiza Kampuni ya Lake Group Kuzingatia Utunzaji wa Mazingira Katika Kata ya Makame

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942
Mbunge wa Jimbo la Kiteto Mkoa wa Manyara, Mhe. Edward Ole Lekaita ameshiriki hafla ya utiaji saini Mkataba wa Mwekezaji mpya wa Kampuni ya Untamed Horizons kutoka Lake Group na WMA Makame ambapo amewataka Wawekezaji kushirikiana na wananchi wa Makame katika kutunza na kuhifadhi Mazingira.

Kampuni ya Untamed Horizons kutoka Lake Group imesaini Mkataba na WMA Makame kufanya Uwindaji wa Kitalii na Utunzaji wa Mazingira ambapo WMA Makame itapata zaidi ya Shilingi Bilioni 9 ndani ya Miaka 10 kupitia Mwekezaji.

Aidha, Kampuni ya Untamed Horizons kutoka Lake Group imekabidhi Pikipiki 2 zenye thamani ya Shilingi Milioni 5 na Gari Moja lenye thamani ya Shilingi Milioni 150 kwa WMA Makame ikiwa ni baadhi ya vitu Mwekezaji huyo aliahidi kutimiza katika Mkataba.

Vilevile, Mbunge Lekaita ametembelea Zahanati ya Kijiji cha Makame kuona hali ya Huduma pamoja na ujenzi wa jengo jipya.


WhatsApp Image 2023-11-22 at 06.30.33.jpeg
WhatsApp Image 2023-11-22 at 06.30.35.jpeg
WhatsApp Image 2023-11-22 at 06.30.38.jpeg
WhatsApp Image 2023-11-22 at 06.30.38(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-11-22 at 06.30.39.jpeg
 
Back
Top Bottom