Mbunge CCM Hamisi Kingwangalla atishia kujiuzuru

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

• ADAI AMECHOSHWA NA KUNYANYASWA WAPIGA KURA WAKE

na Mustapha Kapalata, Nzega

MBUNGE wa jimbo la Nzega Dk. Hamis Andrea Kigwangalla (CCM), ametishia kujiuzulu ubunge endapo serikali ya chama chake itashindwa kutenda haki kwa wananchi wake.

Mbunge huyo alitoa tishio hilo juzi mara baada ya kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya ya Nzega, akikabiliwa na tuhuma za makosa sita, likiwemo la kuvamia Kituo cha Polisi cha wilaya ya Nzega.

Kigwangalla, akiwa na watuhumiwa wenzake watatu, alisema kama suala lake halitafanyiwa uchunguzi na kupata suluhu pamoja na kuangalia haki kwa pande mbili za walalamikaji, atafanya maamuzi mazito.

Alisema hawezi kuendelea kuwa mbunge huku akishuhudia wananchi wake wakinyanyaswa na kunyimwa haki zao na serikali iliyo madarakani kwani mgogoro huo unajulikana hadi ngazi ya juu.

"Kama serikali isipoingilia na kutenda haki kwa wananchi wa Isunga, Ngwanda, Mwabangu na kwa mbunge wao na watu wengine ambao wameshtakiwa bila utaratibu, mimi naweza kuchukua hatua kali zaidi na hata kujivua ubunge kwa sababu siamini katika dhana ya kufanya kazi ya kuwawakilisha wananchi ya kufanya kazi katika mazingira ya dhuruma, unyanyasaji na ukandamizaji usio na maana.

"Bahati nzuri mimi ni mbunge wa CCM na kama Serikali ya CCM ni sikivu, basi leo isikie kilio changu na ifanye maamuzi. Yaliyonikuta na yaliyonitokea ni mazito na siwezi kuvumilia. Mimi kama mimi, nitaamua kujitoa ubunge na pengine kutokugombea nafasi yoyote ile ya uongozi ndani ya chama," alisema Dk. Kigwangalla.

Mbali ya kutishia kujivua ubunge, mbunge huyo pia alifikia hatua ya kusema kwamba yuko tayari kufa kutetea haki ya wananchi wake dhidi ya manyanyaso ya serikali ya CCM.

Wengine wanaoshtakiwa na mbunge huyo ni Mrisho Hamis, Mathew Dotto na Mwanja Mwandu ambao wote kwa pamoja wanadaiwa kuhamasisha wanakijiji wa Mwabangu kuvamia kituo cha polisi kupinga manyanyaso dhidi ya wachimbaji wadogo wa madini.

Mungu anamakusudi sana chadema wakifanya hayo wanaonekana wahuni sasa yameanza kuwarudi mpaka 2014 ccm itakuwa tabani..
 
Kama ulivyosema anatishia , lakini hawezi kujiuzulu, nakwambia hawezi, Huyu Kingwalangwala hawezi, hasilani hawezi kama unabisha akijiuzulu nitamuomba Mod anipe Ban ya mwezi mmoja ...! kingwalangwala hawezi asilani kuachia madaraka
 
kama yeye si mnafiki basi hili la kupigwa na polsi linatosha kuachia ubunge. Sasa anasubiri nini zaidi ya hapo?
 
Huyu mtu kuna mgao wa kifisadi anataka apewe na yeye. Mwenye nia thabiti hawezi kutishia kujiuzulu. Inatakiwa ajiuzulu, wapoteze jimbo watie akili ili waanze kuwatendea haki wananchi.
 
Mungu anamakusudi sana chadema wakifanya hayo wanaonekana wahuni sasa yameanza kuwarudi mpaka 2014 ccm itakuwa tabani..

Mkuu hiyo inathibitisha kwamba ccm ndio wahuni, ila wamekuwa wakiipakazia chadema lakini sasa wameumbuka.
 
kama yeye si mnafiki basi hili la kupigwa na polsi linatosha kuachia ubunge. Sasa anasubiri nini zaidi ya hapo?
Posho na marupurupu ya ubunge ni manono ukilinganisha na kamshahara kake ka udaktari. Kamwe hawezi kuthubutu kuuacha ubunge
 
Naomba nirejeshe nyuma maneno yangu ya awali: niliwahi kumsema Kigwangalla aache unafiki alipotaka kuandaa maandamano ya kupinga mgodi huu unaomtesa hadi sasa. Sasa naomba niseme kuwa naona dalili za kupevuka kijana huyu tuliyemuokoa kufukuzwa chuo pale Muhimbili miaka kadhaa ilopita. kama ni kweli naamini anamaanisha asemalo. Tumpe ushirikiano na ushauri muafaka, anaweza kuwa chachu ingine ya mabadiriko.... Kila la kheri Khamis. Naamini ****** ya sufuria hayaogopi moto!
 
• ADAI AMECHOSHWA NA KUNYANYASWA WAPIGA KURA WAKE

na Mustapha Kapalata, Nzega

MBUNGE wa jimbo la Nzega Dk. Hamis Andrea Kigwangalla (CCM), ametishia kujiuzulu ubunge endapo serikali ya chama chake itashindwa kutenda haki kwa wananchi wake.

Mbunge huyo alitoa tishio hilo juzi mara baada ya kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya ya Nzega, akikabiliwa na tuhuma za makosa sita, likiwemo la kuvamia Kituo cha Polisi cha wilaya ya Nzega.

Kigwangalla, akiwa na watuhumiwa wenzake watatu, alisema kama suala lake halitafanyiwa uchunguzi na kupata suluhu pamoja na kuangalia haki kwa pande mbili za walalamikaji, atafanya maamuzi mazito.

Alisema hawezi kuendelea kuwa mbunge huku akishuhudia wananchi wake wakinyanyaswa na kunyimwa haki zao na serikali iliyo madarakani kwani mgogoro huo unajulikana hadi ngazi ya juu.

"Kama serikali isipoingilia na kutenda haki kwa wananchi wa Isunga, Ngwanda, Mwabangu na kwa mbunge wao na watu wengine ambao wameshtakiwa bila utaratibu, mimi naweza kuchukua hatua kali zaidi na hata kujivua ubunge kwa sababu siamini katika dhana ya kufanya kazi ya kuwawakilisha wananchi ya kufanya kazi katika mazingira ya dhuruma, unyanyasaji na ukandamizaji usio na maana.

"Bahati nzuri mimi ni mbunge wa CCM na kama Serikali ya CCM ni sikivu, basi leo isikie kilio changu na ifanye maamuzi. Yaliyonikuta na yaliyonitokea ni mazito na siwezi kuvumilia. Mimi kama mimi, nitaamua kujitoa ubunge na pengine kutokugombea nafasi yoyote ile ya uongozi ndani ya chama," alisema Dk. Kigwangalla.

Mbali ya kutishia kujivua ubunge, mbunge huyo pia alifikia hatua ya kusema kwamba yuko tayari kufa kutetea haki ya wananchi wake dhidi ya manyanyaso ya serikali ya CCM.

Wengine wanaoshtakiwa na mbunge huyo ni Mrisho Hamis, Mathew Dotto na Mwanja Mwandu ambao wote kwa pamoja wanadaiwa kuhamasisha wanakijiji wa Mwabangu kuvamia kituo cha polisi kupinga manyanyaso dhidi ya wachimbaji wadogo wa madini.

source pls
 
kama ulivyosema anatishia , lakini hawezi kujiuzulu, nakwambia hawezi, huyu kingwalangwala hawezi, hasilani hawezi kama unabisha akijiuzulu nitamuomba mod anipe ban ya mwezi mmoja ...! Kingwalangwala hawezi asilani kuachia madaraka

si yeye tu wana magamba wote kujiuzulu?! Hakuna kit kama hicho.si unamuona raisi wa munduli.yeye ni kama bado yupo tu serikalini alilazimishwa kila siku yupo kwny media lol
 
Kama anatetea watu wake tumtie moyo, viongozi wengi wamesahau kupigania raia maskini wanaowaongoza. Pigana Kigwan Gala hata kama wewe si tajiri kama Aziz lakini pia kujiuzuru ni vema
 
Back
Top Bottom