Mbona yalikuwa makubwa!

Ujumbe.
1. Ni muhimu kuwa na vitambulisho wakati wote uwapo nje ya nyumbani kwako.
2. Si wote wenye makosa wanahusika. Wengine wanasingiziwa kwa makusudi au kwa bahati mbaya.
3. Si vizuri kumhusisha mtu na jambo kubwa bila ya kuwa na uhakika.
4. Matatizo hayakupigii simu.


Pole sana mkuu. Kwahiyo safari ya kwenda kiwandani ikaishia hapo hapo.
 
duh pole,mie nisingeshuka hivi hivi...ningemkwida huyo dada mpaka angenikoma.
 
Pole sana.Bila vitambulisho ulikuwa umepiga tiktak ukiwa umevaa msuli tu na bila kuwa na nguo ya ndani!
 
Duh! Sio mchezo! Dingi umenikumbusha kisa cha mtu aliombwa lift saa moja usiku hivi kndoni makaburini na wadada 2. Kufika kituo along morocco-mandela rd wakasema wanaomba kushushwa kituoni. Dada mmoja asianze kusema nipe hela yangu! Akilalamika yeye ni changu na walipatana kiasi fulani. Kafungua mlango anaongea kwa sauti ya juu,mwenzie anasema ni kweli! Ilibidi jamaa atoe b4 umati haujaongezeka. Mjini kuna mikasa sana!
 
Mkuu pole sana
Yaani usingekuwa na hivyo vitambulisho ingekuwa balaa. Ungeswekwa ndani bila maelezo mpaka waje kuproove kuwa sio wewe ni issue
 
Nakumbuka ilikuwa ni mwaka 2005, nilikuwa naelekea Mbagala kwenye kiwanda cha kutengeneza kanga na vitenge cha KTM. Nilikuwa ndio kwanza nimefungua biashara ya kuuza kanga na vitenge na nilikuwa nachukulia mzigo wangu kiwandani moja kwa moja.

Siku hiyo nilikuwa naenda kuweka order kwa ajili ya wiki inayofuata, na safari yangu ilianzia pale Kariakoo ambapo nilipanda basi aina ya DCM na kupata kiti. Naijua adha ya usafiri wa Mbagala, lakini siku hiyo usafiri haukuwa na tabu sana, labda kwa sababu ilikuwa ni mchana. Nikiwa nimekaa kwenye kiti , alikuja abiria mwingine na kukaa kwenye kiti hicho na mara basi likaanza kuondoka baada ya kupata abiria wa kutosha. Alikuwa ni msichana tu, ambaye alionekana kama mgeni kidogo hapa Dar, na hiyo ilitokana na mavazi yake na hata ongea yake, hasa pale alipomsalimia mama mmoja aliyekaa kiti cha jirani. Sikujishughulisha naye kwani nilikuwa nimejiinamia nikisoma gazeti.

Huyu binti alikuwa akinitizama sana, na alikuwa akinichunguza kwa udadisi, wakati wote alikuwa akinitizama kama ananitilia mashaka, ilibidi nimgeukie na kumuuliza kama anashida gani, maana nilianza kumuona kama kero. Alinitazama kwa taharuki na kuniambia, ‘eh, ulijua mwenyewe sitakushika hivyo, ulijua una akili kama maraika. Sasa leo nimekushika au sikukushika?’ kwanza, nilifikiri ni mzaha, ingawa sikuwa nimemwelewa ana maana gani. ‘Unasema na mimi?’ Nilimuuliza. Alisonya na kusema, ‘kumbe ivo nasema na nani mwingine?’ alikuwa na lafudhi ya Kiiringa kabisa. ‘Umejitia mjanja, ati unajifanya kunibaka, ukajua sikushiki.’ Alisema na nilianza kupata wasiwasi.

‘Wee binti wacha wendwazimu wako, yaani mimi nimekubaka wewe?’ nilisema na sauti yangu ilikuwa na kitetemeshi kwa sababu ya hasira na hofu. ‘Hee, yaani unataka nikupigie kelele wakupeleke polisi. Nataka uniambie kwa nini siku ile ulipokuja kulala kwa dada ulininyatia usiku ukanigeuzaga mkeo?’ Hapo nilizidi kuchanganyikiwa, kwa sababu pia abiria wengi walikuwa wamevunja shingo kutaka kujua kulikoni. ‘Sikiliza binti, nadhani umechanganya mambo. Mimi naitwa nani?’ Yule binti alisema, ‘bwana wee usitake kunichanganya. Wee si binamu yake dada, hakujui nani wewe. Wewe si Julius. Mii nikionaga mtu siku moja tu, simsahaugi tena….. Ndio maana tangu siku ile hujaja tena kwa dada.’ Aliunganisha madai.

Sasa nusu ya basi walikuwa wanasikia kinachoendelea. ‘Naomba tushuke twende kituo cha polisi ili tukajue mwenye haki.’ Nilisema, nikiwa sina hakika kama natoa pendekezo sahihi. ‘Twende kwani mie naogopa, twende ukafungwe miaka 30 ukome kubaka watoto wa wenzio. Jitu kubwa linanyatia wanawake ………’ Baadhi ya abiria walicheka na wengine waionyesha dalili zote za kutaka kujichukulia sheria mikononi, maana hata miaka 30 jela nilishahukumiwa mle mle ndani ya basi.

‘Dereva ingiza basi kituoni, kuna mtuhumiwa wa ubakaji humu ndani ya basi amenaswa.’ Abiria mmoja pandikizi la mtu alisema huku akiwa amenikazia macho, nilianza kuwa mdogo kama sisimizi…….. Lakini abiria mwingine alidakia, ‘kwani wewe binti unamjua huyu kaka kwa jina? ‘Namjua, anaitwa Julius anafanya kazi kwenye kutengeneza semeti ni dereva. Yule abiria alisema, ‘braza, unaweza kutupa kitambulisho chako tuone?’ Nikajua mambo yamekuwa mambo. Nilitoa kitambulisho changu cha kupigia kura na kadi ya benki. Havikuwa na jina la Julius. Yule abiria alivisoma kwa sauti na kusema, ‘binti inawezekana umechanganya mambo, na ujue kumsingizia mtu jambo kama hilo ni kosa la jinai’

‘Je kama kabadilisha jina mii nitajuaje. Basi, kama ni hivyo mimi namwachia Mungu.’ Ilibidi nikatishe safari na kushuka njiani ili nirudi nyumbani, kwani uso wote ulikuwa umesawajika kwa fedheha………Kumbe mtu anaweza kukufanya ukauawa hivihivi…………………….! Sikuwa namjua yule binti, na wala katika maisha yangu sijawahi hata siku moja kufikiria kumnyatia hata house girl wangu, au hata kutongoza hovyo.

Matusi ya nguoni hayo, kaka. Tena kutoka kwa mtu usiyemfahamu. Ungemgeuzia kibao hapo hapo.
 
Back
Top Bottom