Mbona kama Wabunge Wanalalamika na Kulia lia badala ya kuchukua Hatua Dhidi ya Wezi?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,076
49,785
Kwa Hali ilivyo ni ngumu sana ccm kujichukulia hatua maana wizi wote huo wao ni wanufaika wa Moja kwa Moja.

Ndio maana hakuna hata mbunge mmja wa kuja na hoja binafsi japo ya kutunga sheria wa kuwafilisi wezi achilia mbali kuwanyonga.

Pili Wabunge wa ccm wanakosa maarifa,yaani wanachangia kama wanaiomba Serikali wakati katika Hali ya kawaida Serikali inatakiwa kulazimishwa na Ili kulazimishwa lazima waje na maazimio ya nini Cha kufanya na Kwa timeline.

Pia kama haijafanyika hivyo wamshinikize Waziri Mkuu kuachia ngazi so kukiwa na shinikizo Serikali watafanya vinginevyo ni taarabu.

Hiki anachoongea Tabasamu kimenifikirisha na kunisikitisha sana lakini hii approach ya kuomba Serikali haifai.Just imagine taarifa za CAG miaka 3 Iliyopita hazijafanyiwa kazi unategemea nini?

Hawa wenyewe ni wezi wameiba uchaguzi 2020, pia walitoa rushwa 2020, Kila mtu ale tu ndo suluhu, wengine tutakwepa Kodi na kuwapiga wake zenu
 
Niko nasoma Katiba nione wanapaswa kuwa na Nguvu kiasi gani

Nakumbuka Bunge lilishindwa kumuwajibisha Jairo akiwa Katibu mkuu wa Nishati
Hawakushindwa wanaweza hata kukataa kufanya kazi nae,wanaweza ku table Azimio la kubadili sheria ambazo wanaona Zina shida na pia wanaweza kumkataa Waziri Mkuu ikiwa Serikali haitekelezi maazimio Yao hivyo Serikali kuanguka.

Na mwisho kuzuia Bajeti ya serikali na Bunge kuvunjwa ila Sasa wale vocal wanaweza wasirudi Bungeni Kwa sababu chama kinaweza kutowapitisha nk.

Kimsingi Katiba yetu haiwapi Nguvu za kutosha yaani wako kwenye kwapa la Serikali na chama.
 
Kwa Hali ilivyo ni ngumu sana ccm kujichukulia hatua maana wizi wote huo wao ni wanufaika wa Moja kwa Moja...
Dont mind them ni wamoja hao. Wanatuchezesha sisi mchezo wa kuigiza tuone wanafoka lkn hakuna hatua yeyote itakayochukuliwa believe me kila mwaka wimbo huwa ndo huo huo bunge litaisha na maisha yataendelea na wizi utaendelea
 
Tatizo bunge ni la chama kimoja na kuna party caucus, hivyo wanaogopana. Cha msingi katiba iruhusu mgombea binafsi na mbunge kuhama chama na kumaintain ubunge wake kuliko Sasa. Haya yakitokea wabunge watakuwa huru kuisimamia serikali.
 
Kwa Hali ilivyo ni ngumu sana ccm kujichukulia hatua maana wizi wote huo wao ni wanufaika wa Moja kwa Moja.

Ndio maana hakuna hata mbunge mmja wa kuja na hoja binafsi japo ya kutunga sheria wa kuwafilisi wezi achilia mbali kuwanyonga.

Pili Wabunge wa ccm wanakosa maarifa,yaani wanachangia kama wanaiomba Serikali wakati katika Hali ya kawaida Serikali inatakiwa kulazimishwa na Ili kulazimishwa lazima waje na maazimio ya nini Cha kufanya na Kwa timeline.

Pia kama haijafanyika hivyo wamshinikize Waziri Mkuu kuachia ngazi so kukiwa na shinikizo Serikali watafanya vinginevyo ni taarabu.

Hiki anachoongea Tabasamu kimenifikirisha na kunisikitisha sana lakini hii approach ya kuomba Serikali haifai.Just imagine taarifa za CAG miaka 3 Iliyopita hazijafanyiwa kazi unategemea nini?

View: https://www.instagram.com/reel/CzOGTbDiO0c/?igshid=MWlrdHNzZnFhaDdwNA==
 
Back
Top Bottom