Mbeya: Watu watatu washikiliwa kwa kuingiza Vipodozi vyenye viambata sumu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Kamanda.JPG

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa watatu (majina yanahifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi) wakazi wa Tunduma kwa tuhuma za kuingiza nchini vipodozi vya aina mbalimbali vilivyopigwa marufuku vyenye viambata sumu pamoja na bidhaa za magendo kupitia njia za panya.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Benjamin Kuzaga amesema watuhumiwa wamekamatwa Machi 03, 2023 majira ya saa 12:30 asubuhi katika misako iliyofanyika maeneo ya Izumbwe, Wilaya ya Mbeya Vijijini na kufanikiwa kuwakuta wakiwa na vipodozi vya aina mbalimbali vyenye viambata sumu vilivyopigwa marufuku nchini ambavyo ni:-

  • CARORITE BOX 20
  • CREAM AINA YA NAOMI CATON 10
  • NEPROSONE GEL BOX 45
  • CREAM PEAU CREIRE CATON 8.
  • DIANA CATON LOTION 8,
  • CREIRE FOR MEN CATON 12.
  • DERMO GEL DAZAN 26,
  • COCOPUP BOX 26
  • MAFUTA AINA COCOPAP BOX 04.
  • EPIDERM ZIPO CATON 9.
  • VAROLIGHT BOX 2.
  • BETASOL BOX 2.
  • DERMO GEL 26
Ameongeza kuwa katika upekuzi, watuhumiwa walikutwa na mali Vitenge jola 26 vilivyoingizwa nchini bila kulipiwa ushuru wa forodha kupitia njia zisizo rasmi vikiwa ndani ya Gari namba T.165 BQT aina ya Cresta GX 100.

Watuhumiwa walikuwa wakisafirisha vipodozi hivyo vyenye viambata sumu na Vitenge hivyo kwa kutumia gari yenye namba za usajili T.165 BQT CRESTA GX 100 kutoka nchini Zambia kupitia njia isiyo rasmi ya Ilembo Umalila.

Kamanda Kuzaga amesema watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
 
View attachment 2536743

Wamekosa hela ya kuwapa askari.
 
Wanaacha kumkamata mwigulu wamuulize anapataga wapi nguvu yakutukana watanzania wanadili na waangaikaji
 
Wanawake kwenye vipodozi sijui wamerogwa?Unamwambia kabisa hii ni cream ya Fangasi usitumie kama mafuta,anakwambia nikiacha chunusi zinarudi,hizo cream huyo jamaa angepenya wateja anao tayari wala hatafuti soko,maana zinafanya mtu awe mweupe sababu ya hizo kemikali sumu.

Ndio maana Kansa na magojwa ya Figo sikuhizi yameshamiri,kumbe wameshajijaza ma Hydroquinon na mercury mwilini,kupitia vipodozi na dawa za kuoshea nywele.

Miaka kama kumi iliyopita,niliwahi kununua hio Carolite nilikuwa sijui kama inashida,nilipojipaka usoni tu nikasikia kichwa kama kinazunguka hivi,ikabidi nikanawe,tulikuwa na mama Mmoja anatupikia nikamuuliza huwa unatumia hii?akasema ndio,nikampa alifurahi sana nikamwambia Mimi nimeshindwa harufu,baadae ndio nikajua pia kumbe ina viambata vya sumu.

Sasahivi tunaambiwa pia zile mashine za kukaushia kucha zinasababisha kansa.
 
Back
Top Bottom