Mbeya: Viongozi wa SACCOS Rungwe washtakiwa kwa Ubadhirifu

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,618
Oktoba 20, 2023 katika Mahakama ya Wilaya Rungwe, mbele ya Mhe. Mwinyijuma Bwaga, imefunguliwa kesi ya uhujumu uchumi na 3/2023, Jamuhuri dhidi ya Vumilia Simoni ambaye ni Makamu Mwenyekiti na Mauyeni Kilumbe, Mjumbe wa SACCOS ya CHAMIWARU iliyopo Halmashauri ya Wilaya Rungwe mkoani Mbeya.

Washtakiwa hao wameshtakiwa kwa kosa la ubadhilifu na ufujaji wa kiasi cha Sh. 1,000,000 mali ya SACCOS ya CHAMIWARU. Ilidaiwa walizichukua fedha hizo benki na baadaye kutengeneza nyaraka wakionesha kuwa wametumua fedha hizo kiasi cha 1,000,000 kumkopesha mwanachama mmoja wa SACCOS ili hali wakijua kuwa ni uongo kwani kiasi hicho cha fedha waligawana kwa matumizi yao binafsi.

Kosa hili ni kinyume na kifungu cha 28 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11/2007.

Washtakiwa baada ya kusomewa mshitaka yao wameachiwa kwa dhamana na shauri limepangwa kuendelea kwa hatua ya kuanza kusikiliza maelezo ya awali (PH) Novemba 14, 2023.

Chanzo: TAKUKURU
 
Back
Top Bottom