Mbeya : Viongozi 58 wa Vyama Vya Ushirika Watiwa Mbaroni Kwa Kutapeli Wakulima wa Kakao Shilingi Milioni 800.

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,109
49,812
Hawa Mabwana Kwa Kushirikiana na matajiri wanunuzi wa zao la Kakao waliuza mazao ya mkulima yaliyohofadhiwa kwenye maghala ya Serikali Kwa bei ya sh.8,000 Kwa kilo ila wakawalipa Wakulima sh.1,600 za Juu wakapiga takribani Shilingi Milioni 800.

--
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Comrade Juma Homera ameagiza kukamtwa na kuchunguzwa kwa Viongozi wa vyama vya Ushirika na Watunza Ghala wa zao la Kakao Wilayani KYELA kwa Kosa la kuhujumu mfumo wa Stakabadhi Gharani uliosababisha kupotea kwa kiasi Cha Fedha Milioni mia Nane za Wakulima.

Baada ya kuunda Tume ya Uchunguzi na kuwahoji Wakulima kwa ushahidi wa Rist imebainika ni kweli hawajalipwa kiasi hicho Cha Fedha jambo ambalo limemfanya RC Homera kulitaka Jeshi la Polisi kwa kishirikiana na TAKUKURU kuondoka na washutumiwa mara baada ya kufunga Kikao hicho jambo ambalo limetekelezwa haraka iwezekanavyo.

Kaimu Mkurugenzi wa Mfumo wa Stakabadhi Ghalani Wilayani Kyela Asangye Bangu amemwambia RC Homera kuwa Uchunguzi uwao libaini Wahusika walikuwa wakizitumia Fedha hizo kula Raha katika fukwe za ziwa Nyasa.

View: https://www.instagram.com/reel/CyNA_R6NaSZ/?igshid=MTc4MmM1YmI2Ng==

Baada ya uchunguzi umebainisha Jamaa walikuwa wanatumbua na kula Raha Kwa pesa wakulima walizogawana kwenye beaches za Matema huko Ziwa Nyasa.

Aidha Serikali inawasaka matajiri 8 walioshirikoana na Viongozi wa Vyama vya Ushirika kufanya hujuma Kwa wakulima.

My Take
Serikali leteni sheria ya kumfilisi Mwizi ndio hukumu zingine ziendelee maana watu wanahukumiwa fine wanalipa na pesa za Umma zinakuwa zimeenda.Hii Nchi Ina tatizo kubwa sana la Maadili.

View: https://www.instagram.com/reel/CyeUuT8tST6/?igshid=MTc4MmM1YmI2Ng==
 
Wamechukua zaidi ya nusu! Inasikitisha!!!
 
Back
Top Bottom