BUSHU3
Member
- Apr 8, 2021
- 71
- 72
Jeshi la Polisi mkoani Mbeya, linawashikilia Askari watano wa Jeshi hilo kwa tuhuma za kujihusisha na usafirishaji wa wahamiaji haramu raia wa Ethiopia kuwapeleka nchini Malawi kupitia mpaka wa Kasumulu uliopo wilayani Kyela.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,Kamishna Msaidizi wa Polisi, Benjamin Kuzaga, amethibitisha kukamatwa kwa Askari hao.
Aidha Kuzaga ametoa wito kwa Askari kuacha kujihusisha na vitendo vya usafirishaji wa wahamiaji haramu.
Chanzo: EATV
=============
JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya, linawashikilia Askari Polisi watano kwa tuhuma za kujihusisha na usafirishaji wa wahamiaji haramu Raia wa Ethiopia.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Benjamin Kuzaga, amethibitisha Askari hao kukamatwa ambao ni ASP Thomas Bwire, Beda Moriss, Saimon Billia, Mohamed Ndunguru na Joseph Manumbu.
Kamanda kuzaga amesema Octoba 20 majira ya saa 10: 45 asubuhi huko kituo kidogo cha Polisi Uyole jijini Mbeya, Askari hao walikamatwa wakiwa na wahamiaji haramu sita Raia wa Ethiopia wakiwa ndani ya gari yenye namba za usajili T. 946 BTT, Toyota Cresta ambayo ni mali ya Askari Billia kufuatia taarifa kutoka kwa msiri kuwa walikuwa walikuwa wakipanga njama za kutaka kuwasafirisha wahamiaji haramu kwenda nchini Malawi kupitia mpaka wa Kasumulu Kyela.
“Natoa wito kwa Askari kuacha kujihusisha na vitendo vya usafirishaji wa wahamiaji haramu na litaendelea kuchukua hatua kali za kisheria kwa yeyote atakayebainika kufanya vitendo hivyo bila kujali cheo chake," amesema Kuzaga.
Mwisho.