mwanamama
Member
- Feb 6, 2008
- 61
- 0
Wandugu nina taarifa yenye uthibitisho kuwa jamaa aliyemuua bro Raymond Tungu Kapalata ameshikwa jana jumamosi saa saba mchana huko Iringa Tanzania, baada ya kukimbia kutoka Mwanza ambako alishiriki kwenye ugomvi. Vyanzo vyetu vya habari vinatuambia kuwa jamaa yuko mbaroni na ubalozi wa Marekani Dar umekwishataarifiwa,ili afanyiwe utaratibu wa kurudishwa Marekani kuja kujibu mashtaka ya mauaji.
Ikumbukwe kuwa ni miaka mitatu sasa toka ndugu yetu Ray alipotutoka, madhali muuaji ameshakamatwa sheria itachukua mkondo wake.
Na wale ndugu zetu ambao mko Detroit MI msisite kutoa taarifa yoyote ambayo itaelekeza kukamatwa kwa waliowaua ndugu zetu Nkya na Mazula. Kwa sababu ndugu hawa wameuliwa na watu, kwa hiyo ni lazima sheria ichukue mkondo wake.
Habari ya kukamatwa kwa muuaji wa Ray imeandikwa pia kwenye YoungAfrican.com