Mbakaji Achinjwa Kwa Jambia Saudi Arabia

Mbonea

JF-Expert Member
Jul 14, 2009
640
20
Serikali ya Saudi Arabia imemchinja kwa kutumia jambia mwanaume raia wa Yemen ambaye alihukumiwa adhabu ya kifo baada ya kupatikana na hatia ya kuwabaka wanawake wawili.

Mwanaume huyo aliyetajwa kwa jina la Suleiman bin Ali alichinjwa kwa jambia jana jumapili kufuatia hukumu iliyotolewa na mahakama ya Jeddah iliyoamuru auliwe.

Suleiman alipatikana na hatia ya kumpiga na kumbaka mke wa raia mmoja wa Saudia, ilisema taarifa ya wizara ya mambo ya ndani ya Saudia.

Suleiman ambaye alitajwa kama mbakaji aliyekuwa akitafutwa kwa makosa menhi ya ubakaji, pia anatuhumiwa kumshambulia na kumbaka mwanamke mwingine wa nchini humo.

Kuuliwa kwa Suleiman kumefanya jumla ya wahalifu waliouliwa nchini Saudi Arabia kuanzia mwezi januari mwaka huu kufikia 67.

Mwaka jana watu 102 wwaliuliwa baada ya mahakama kuwahukumu adhabu ya kifo. Mwaka 2007 jumla ya watu waliohukumiwa adhabu ya kifo ilikuwa 153.

Kwa mujibu wa sharia za kiislamu zinazotumika nchini Saudi Arabia, wabakaji, wauaji, majambazi na wauzaji au wasafirishaji wa madawa ya kulevya huhukumiwa adhabu ya kifo.

Source: http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=3817442&&Cat=2
 
Hii ingeletwa hapa Tanzania, Jambia kwa kila fisadi, tusingebaki masikini.

Mafisadi wanaachiwa ndio wanafundishana njia za kufisadi nchi, Gavana Ndulu nae, ameshafahamu njia za kufisadi. Hii ndo hatari ya kuwaacha mafisadi wakitamba mitaani

MR JK; "JAMBIA IS THE ANSWER" kama china.
 
Kuuliwa kwa Suleiman kumefanya jumla ya wahalifu waliouliwa nchini Saudi Arabia kuanzia mwezi januari mwaka huu kufikia 67.

Mwaka jana watu 102 wwaliuliwa baada ya mahakama kuwahukumu adhabu ya kifo. Mwaka 2007 jumla ya watu waliohukumiwa adhabu ya kifo ilikuwa 153.

Duuu! hawa jamaa ni kuchinjana tu hamna adhabu nyingine?
 
Ninaapa kuwa watoto wao wakibaka, sheria zitapindishwa hadi WAWAOKOE.

Mchina ana njia nyingine tofauti kabisa. Kule hata uwe TOP, ukimess up utakwenda.

Kuna tofauti kutumia DINI kuhukumu na kutumia SHERIA zilipotishwa na BUNGE lisilo na dini kuhukumu. Kwa hilo la Wachina hata mie nalipenda.
 
Hivi hakuna njia nyingine ya kutoa roho ya mtu isipokuwa jambia? Huu ni ukatili wa aina fulani maana tunaambiwa hata wanyama tunapowachinja tusiwafanyie ukatili kama vile kuwakata miguu kwanza! Kifo kama hiki kingefanywa na nchi kama Tanzania tungeambiwa ni "barbaric" lakini kwa vile ni Saudi Arabia ana petro-dollar kibao mabeberu wanaufyata! Talk about hypocricy.
 
Ndio hiyo chinja chinja, ndio maana kila mwizi saudia ana mkono mmjoa
 
Hivi hakuna njia nyingine ya kutoa roho ya mtu isipokuwa jambia? Huu ni ukatili wa aina fulani maana tunaambiwa hata wanyama tunapowachinja tusiwafanyie ukatili kama vile kuwakata miguu kwanza! Kifo kama hiki kingefanywa na nchi kama Tanzania tungeambiwa ni "barbaric" lakini kwa vile ni Saudi Arabia ana petro-dollar kibao mabeberu wanaufyata! Talk about hypocricy.

Ungekuwepo ndio ungeona !!! Huu uchafu katika jamii (wabakaji, wauaji, *******, wazinifu na wengineo wanaostahili hukumu hiyo) huondoshwa kilaiiini, yaani hata dakika haitimii washakata roho. Hii ndio the least painful of executions kulinganisha na kama sindano, risasi, kunyonga kwasababu haichukui muda ubongo "translator ya pain" inatenganishwa na body "container ya roho(soul)" inayotolewa.

Lakini kwa taarifa yako tu ni kwamba ADHABU KALI HUIPATA WALE WACHAFU WANAOBAKIA NYUMA NA WANAOONA ILE ADHABU INATOKEA" Roho zao hupata "quake" kama vile "earthquake". Wale "vi-criminals" katika jamii huachia ngazi. Kwa hiyo katika jamii ile anayeipata adhabu ile ni wale tu ma"hardcore" criminals. Usisahau vilevile adhabu zile zinaendana na misingi na mihimili imara ya mila na desturi za watu husika ambazo tayaaaaaari zinawaweka watu katika jamii actively mbaaaaaaali na kuweza kufanya uhalifu husika.

Walaji rushwa katika ku-struggle kupata cha asubuhi/chai baada ya kulala hoi TZ walistahili kupata "the same magnitude of quake" katika roho zao kwa kuona MAFISADI, ambao ndio kichwa cha matatizo ya TZ wakipata ADHABU ZA NAMNA HIZI. Nafikiri unajua kutafautisha baina ya UFISADI na Ulaji rushwa???
 
Duuu! hawa jamaa ni kuchinjana tu hamna adhabu nyingine?

Fikiria kwamba aliyebakwa ni binti yako, au dada yako, au mama yako, au mkeo. Kumbuka sheria kwa wenzetu kule Saudi, kutokana na islamic perspective, kukamatwa red-handed na confession ndio hutumika. Maana mostly ni 100% No chance for a doubt.

Sasa adhabu ya upanga imehukumiwa, na mahakama imekuchagua wewe na kuweka mabegani mwako utekelezaji wa hukumu ile (upon proper training) ili wewe upate kuridhika na kutosheka na justice. Vilevile jamii inakuangalia wewe ili uiokoe na kuenea kwa ufisadi wa namna hii. Nini itakuwa response yakoo???

Tafadhali wajulishe "msimamo na response" yako mkeo, mabinti zako, dada zako na mama yako uwasikia watasemaje.

Mimi bwanaaaaa Iwill surely take the opportunity, absolutely. Kukosa usingizi siku mbili tatu, kutakuwa balanced na pride ya kutekeleza haki na kuiondoshea jamii ufisadi.

Ole wao MAFISADI TZ.
 
Na sisi wana jamii vilevile !!!
 
Back
Top Bottom