MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,565
- 836
Naamini kabisa hakuna serikali isyo kosa mazuri yake na mabaya yake japo uwiano kati ya mazuri na mabaya ndiyo hutofautiana. Vivyo hivyo naamini serikali ya awamu ya nne haikosi mazuri yake na mabaya yake. Ningependa tupambanue na tuchambue ni yapi mafanikio ya serikali ya awamu ya nne na ni yapi imeshindwa. Binafsi nitaanza mimi kuonyesha yapi naona ni mafanikio na yapi siyo. Haimaanishi najiona nipo sahihi asilimia mia kwa mia na nipo tayari kusahihishwa.
Mafanikio:
1.Kuinua msisimko wa watu: Hakuna serikali iliyopita ambayo iliweza kuinua hisia kubwa za wananchi iwe kwa mazuri au kwa mabaya. Huwezi kuwa neutral na serikali ya JK. Ni aidha unaipenda sana au unaichukia sana. Kwa kiasi kikubwa awamu hii imeamsha wananchi washiriki zaidi au kufuatilia zaidi siasa za nchi yao. Hatukuona hii kwenye awamu zilizo pita.
2. Uwazi (transparency): Katika awamu zote hii ndiyo awamu ambayo mambo ya serikali yanaonekana na kujadiliwa wazi wazi. Najua wengi watasema ni upinzani ila pia tukumbuke pia kuwa hata awamu ya Mkapa kulikua na upinzani. Pia kumekuwa na uhuru zaidi wa vyombo vya habari na havibanwi kama awamu zilizo pita.
3. Dipolomasia: Katika diplomasia tumefanikiwa na hii inawezekana ni kutokana na historia ya JK kuwa waziri wa mambo ya nje. Hapa siongelei safari za nje! Tanzania ilipewa heshima ya kuwa mwenyekiti wa AU, raisi alichaguliwa kuwa mmoja wa wasuluhishi wa Ivory Coast na pia tuliweza kuikomboa Comoro.
Wapi wameshindwa:
1. Rushwa: Rushwa bado ni tatizo kubwa na mpaka sasa kuna watu wamekua "untouchables". Ndiyo kuna walio kamatwa na kushtakiwa kwa tuhuma mbali mbali kama wakina Basil Mramba, Daniel Yona, Mgonja nk lakini mpaka sasa ni dagaa tu wanaokamatwa na kutuhumiwa huku mapapa wakiwa bado hawashikiki.
2. Umoja: Nadhani kwa kiasi kikubwa amawu hii imeshindwa kuleta umoja. Kuanzia kwa wananchi kwa kujaribu kuhubiri udini kwa manufaa ya kisiasa mpaka mipasuko ndani ya chama chenywe ambapo kuna makundi mbali mbali. Nilikua namuona JK kama raisi atakae kuwa "The Great Unifier" ila amekua the great divider.
3. Uchumi: Labda mambo yailiyo nje ya uwezo wa serikali yamechangia ila kusema ukweli serikali imeshindwa kutekeleza ilani yake ya uchumi. Sasa hivi kila kitu kimepanda bei toka awamu ya kwanza na baadhi ya vitu muhimu vimeanza kuadimika kama umeme na mafuta nk.
4. Umeme: Mh mgao wa sasa haujawahi kuonekana Tanzania. Japo serikali ilijua tokea 2006 kuwa kima cha maji kinashuka na kitaendelea kushuka bado hakuna njia mbadala zilizo tafutwa kupunguza adha ya ukosefu wa umeme. Hakuna nchi inayoweza endelea bila nishati ya umeme. Biashara zina athirika, viwanda vina athirika na mwisho wa siku UCHUMI una athirika.
Nipo tayari kusahihishwa. Yote ni katika kujifunza zaidi kuhusu serikali yetu ya sasa.